OCD Kyela agoma kulinda helikopta ya Dk. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OCD Kyela agoma kulinda helikopta ya Dk. Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Njowepo, Oct 4, 2010.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa
  Mvutano mkubwa uliibuka jana kati ya mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kyela (OCD), aliyetambulika kwa jina moja la Male, baada ya kutoa taarifa ya kukataa kuilinda helikopta inayotumiwa na mgombea huyo.
  Mvutano huo ulianza saa 11:00 jioni jana baada ya Dk. Slaa kuwasili katika uwanja wa Mwakangale mjini Kyela kuhutubia mkutano wa kampeni.
  Mkutano huo ulikuwa ni wa mwisho baada ya kuhutubia mikutano mitano ya kampeni katika maeneo kadhaa mkoani Mbeya katika wilaya za Mbarali na Kyela. Mgombea huyo alipangiwa kulala Kyela.
  Baada ya kuhitimisha mkutano wa Kyela, Dk. Slaa aliwaeleza wananchi kwamba helikopta hiyo ingelala uwanjani hapo, lakini baadaye akawaambia kuwa alipata taarifa kutoka kwa OCD kwamba polisi hawatailinda kwa maelezo kuwa helikopta hiyo si mali ya serikali bali mali ya mtu binafsi.
  Taarifa hiyo ilimfanya Dk. Slaa aje juu na kutoa sauti kali kwamba anataka apewe taarifa hiyo kwa maandishi ili aipeleke kwa Inspekta jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema.
  Pamoja na Dk. Slaa kutaka ampe taarifa kwa maandishi, OCD huyo alimwonyesha saa akimtaka ateremke jukwaani kwa kuwa muda wa mkutano ulikuwa umekwisha hivyo ashuke akamshitaki kwa kujiongezea muda wa kampeni. Wakati huo ilikuwa saa 12:10 jioni.
  Hali hiyo ilimlazimisha mchumba wa Dk. Slaa, Josephin Mushumbusi na wafuasi wengine wa Chadema waliokuwa wamepandwa na jazba kumfuata OCD, ambaye baada ya kuona hivyo, alianza kuondoka uwanjani hapo.
  Kufuatia hali hiyo, Dk. Slaa alimuita jukwaani askari anayemlinda na kuwatangazia wananchi kuwa alipewa askari huyo na IGP amlinde wakati wa kampeni.
  “OCD anasema hatalinda ndege yetu wakati mshahara anaolipwa unatokana na kodi zetu,” alisema huku watu wakiitikia kwa kuonyesha kukerwa na kitendo hicho.
  Ilimlazimu askari anayemlinda Dk. Slaa kumfuata OCD huyo na kuondoka naye wakiteta kwa faragha.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, akizungumza kwa simu na NIPASHE kama anahusiana na tukio hilo, alisema kitendo cha OCD ni chake binafsi na hakiwakilishi Jeshi la Polisi.
  Nyombi alisema wao wana maelekezo ya namna ya kutoa ulinzi kwa wagombea wote wa urais na kuahidi kuwa itaendelea kulindwa.
  Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amesema akiingia madarakani atakagua Sh. bilioni 21, maarufu kama “Mabilioni ya JK” zilitolewa na serikali kwa wajasiliamali kila mkoa, ili kujiridhisha kama ziliwanufaisha walengwa (wananchi) au la.
  Amesema atafanya hivyo kwa vile fedha hizo ni mali ya umma na kwamba, kuna taarifa zinazodai kuwa zimewanufaisha watu wachache.
  Dk. Slaa alitoa ahadi hiyo wakati akihutubia mkutano wa kampeni za kuusaka urais wa Jamhuri ya Muungano, mjini Songea juzi jioni.
  “Rasilimali zinagawiwa ovyo tu bila mpangilio. Hizi fedha ni za umma, lakini hakuna anayejua nani kanufaika nazo. Nitazishughulikia na kuhakikisha zinarudishwa katika matumizi ya umma,” alisema Dk. Slaa na kushangiliwa na umati watu waliofurika katika mkutano huo.
  Aliitaka serikali kutaja makampuni yaliyofaidika na Sh. trilioni 1.3 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kuokoa makampuni dhidi ya mtikisiko wa kiuchumi duniani.
  CHANZO: NIPASHE
  MY TAKE:
  Naungana na Mwanakijiji kuwa hawa watu inabidi waandaliwe kisaikologia kwa mageuzi.Naona uyu OCD alikataa kuilinda iyo helicopter kwa kuwa akilini mwake akimweka JK kama raisi ata baada ya October period.Wala hafikilii kuwa Oct 31 anything can happen.Sasa kama mpaka level ya OCD mtu anabehave ivyo sasa hao subordinates si wana kazi sana.Mbaya zaidi bosi wake kamkana kuwa hayo yalikuwa maamuzi yake binafsi.Kwa nchi serious huyu OCD hafai bse he is not objective but leaning to one side.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mbona nimesoma kwamba huko Shinyanga polisi waliilinda helikopta ya JK muda wote ilipoharibika na kwamba JK mwenyewe alikuwa anakampeni zaidi ya saa 12 jioni bila kuteremshwa na polisi.

  Majibu ya RPC yanatia hasira kweli kweli.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,278
  Likes Received: 19,430
  Trophy Points: 280
  mmm kazi ipo. Huyu baada ya 31 atazimia sijui
   
 4. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  OCD hafahamu majukumu yake...
  Ni tabia isiyo ya tija...
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwa ufupi OCD huyo anashindwa kutenganisha chama na serikali, usijekuta hata hajui mwajiri wake ni nani!...Anadhani kuwa serikali ni ya ccm tu, na haiwezi kuwa vinginevyo!..Poor him, ishu hapa ni uelewa butu!
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kama OCD ana uelewa butu sasa atakuwa anawaburuza masubordinates wake?
  Imagine ndio bosi wako huyo,kaaaaaaaaaaaaaaaaazi kweli kweli
   
 7. M

  Mzee_wa_Kale Member

  #7
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 15, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inashangaza sana hii inatuonyesha wazi kuwa baadhi ya viongzi wa serikali hawajaelewa utendaji wao wa kazi katika mfumo wa vyama vingi na hasa katika kipindi kama hiki cha kampeni. Mission and Vision ya Kazi ya Police ni ulinzi wa Raia pamoja na mali zao. Huyu OCD awajibishwe pamoja na wenzake wenye tabia kama hiyo nao wapate lesson, Mzee wa Kale
   
 8. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna wengine wana kansa ya ubongo mpaka watibiwe
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna haja ya kumfuatilia kujua CV yake unaweza kuta ndo wale wazee conservative wa kidumu chama cha mapinduzi na zidumu fikra za mwenyekiti wa chama
   
 10. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Duh! namuonea huruma sana huyu, Baada ya October 31 sijui atajionaje? hivi wewe OCD hujakaa hata vijiweni ukamjua rais wako hata b4 uchaguzi?
   
Loading...