• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

OCD Ilemela mkoani Mwanza tunakuomba utende haki juu hili suala

chagu wa malunde

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
1,084
Points
2,000
chagu wa malunde

chagu wa malunde

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
1,084 2,000
Kila mtanzania hapendi uhalifu ila nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa sheria na kanuni na kufuata misingi ya katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Watuhumiwa walipigwa na kuteswa ndani ya ofisi ya mtendaji wa kata ya Kahama tarehe 26/10/2019. Kila mwananchi aliona.

Mmoja wao alifariki baadae maana mateso hayo yalifanywa na Mwanajeshi na migambo. Mke wa marehemu anaelekezwa na DAS Ilemela umsaidie apate haki ili waliojichukulia sheria mkononi wakatwe.

Wewe na mpelelezi wako mmoja mnamwambia alipigwa na wananchi tena kwenye mji wa mtu.

Kama walipigwa na wananchi tena kwenye mji wa mtu kwa nini msikamate huyo mzee ili awataje waliompiga? Huu utawala sio wa kulindana lindana. Timizeni wajibu wenu.

Mtu amekamatwa amepelekwa ofisi ya kata anapigwa. Alafu bado mke wa marehemu hamsaidii.

Basi kama alipigwa na wananchi tena kwenye mji wa mtu ambaye hata mke wa marehemu mmetajia jina basi mkamateni ili awataje waliomuua huyo mtuhumiwa.

NB: Ibara ya 13(6)(b) ya katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ipo wazi kabisa kwamba hakuna mtu atakutwa na hatia mpaka ithibitishwe na Mahakama.

Ibara ya 13(6)(e) ndio inakataza kutesa na kutoa adhabu ambazo zina madhara kwa binadamu.
 

Forum statistics

Threads 1,403,192
Members 531,106
Posts 34,416,883
Top