OCD Geita wachunguze askari polisi hawa wa Kituo cha Nyarugusu

Loftins

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
8,549
2,000
Non of ur business! Hebu pambana na yako!hujui ht kuna ishu gani! Unaparamia tu!
Ur = Your
Ht = hata
Unapoweka alama ya mshangao katika sentensi hakikisha unaacha nafasi ndipo uandike neno lingine, pia alama za mshangao haziwekwi hovyohovyo.
.
You're dumb as hell
 

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
8,798
2,000
Unataka wakale wapi? Acha unoko mkuu!!!
Mh OCD,salamu!mimi ni raia mwema ninayeishi Nyarugusu.Nalipongeza jeshi la polisi kwa kazi nzuri mnayoendelea kufanya.

Hapa kituo cha Nyarugusu kuna askari wawili wamekuwa kero kwa muda mrefu.Hawa ni Askari anajulikana kama TRUMP na mwenzie Afande Frank.

Napata mashaka makubwa na weledi wa askari hawa kwani wamekuwa na vitendo vibovu kwa muda mrefu.Mfano, ni kawaida askari hawa kuwabambikia kesi vijana wengi hapa Nyarugusu za kuwazuia kufanya kazi, kuwaingilia katika majukukumu yao nk.

Aidha, wamekuwa na tabia chafu ya kutembelea sehemu za biashara na kuwakamata wateja na wasimamizi wa sehemu hizo za biashara kwa kisingizio cha uzembe na uzururaji, kuendesha biashara kinyume cha sheria na makosa mengine mengi ya kipuuzi ya kubambikia.

Vilevile, askari hawa wanatumia nafasi zao kuwanyofoa hela watu hawa wanapokuwa wamewakamata,kuwapiga na kuwabambikia kesi, hakika watu hawa ni kero kubwa, wamezidisha unyanyasaji kwa raia wema.

Vilevile askari hawa wanajihusisha na biashara ya uchimbaji maduara, hutumia muda wao mwingi kuwa kwenye shughuli zao binafsi tofauti na ajira yao ambayo kodi zetu cc wananchi ndo zinawalipa mshahara.

Wanadiriki kuwakingia kifua baadhi ya waharifu kwa kuwa wanafanya nao kazi katika maduara yao, wote wanaokwenda kinyume cha matakwa yao, huwatafutia njama za kuwabambikia kesi na kuwadhoofisha kwa jinsi watakavyo.

Mh OCD, chukua hatua za haraka dhidi ya askari hawa, TRUMP na FRANK, waondolewe Nyarugusu wapelekwe kwingine, hawafai,wamechosha na wanakera kwelikweli!

Haina haja ya kuwasubiri Viongozi wa ngazi za juu ili kilio cha Wananyarugusu kiweze kutatuliwa.

Imani iliyopo, UTAWACHUNGUZA VIUMBE HAWA NA UTAWASHUGHULIKIA KIKAMILIFU

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom