OCD auawa kwa mshale akidhaniwa jambazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OCD auawa kwa mshale akidhaniwa jambazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Aug 5, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,485
  Likes Received: 5,721
  Trophy Points: 280
  *ALIKUWA AKIONGOZA MSAKO WA MAJAMBAZI

  Daniel Mjema, Moshi na Rehema Matowo, Hai

  MKUU wa Polisi Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro (OCD), Mrakibu Petro Mtae (43), amefariki dunia baada ya kupigwa mshale kifuani na wananchi akidhaniwa kuwa jambazi.

  Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko alithibitisha kuwa mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la Kwa Sadala, wilayani humo.

  Kamanda Ng’hoboko alisema majira ya saa tisa usiku wa kuamkia jana, watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walivamia nyumba za wafanyakazi wa shamba la maua lililopo Kikafu kwa lengo la kuwaibia.

  Kamanda alisema baada ya uvamizi huo majirani zao walipiga simu polisi na OCD huyo aliwachukua askari polisi wakiwemo askari kanzu na kwenda nao katika eneo la tukio kuwasaka wahalifu hao.

  Kamanda Ng’hoboko alieleza kuwa baada ya kufika katika eneo la tukio walikuta majambazi hayo yamekimbia, hivyo walipanga na wananchi kuwasaka kupitia daraja la Kikafu lililoko karibu na eneo la tukio wakidhani kuwa watakuwa wamejificha huko.

  Alifahamisha kuwa, OCD huyo alipanga vikosi viwili; kimoja alikiongoza yeye na kwamba walipofika eneo la Kikafu aliona mwanga wa tochi, akawaamuru wasimame akidhani ni majambazi na kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatisha.

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi, kundi la pili baada ya kusikia mlio wa risasi walidhani waliowaamrisha kusalimu amri ni majambazi, ndipo mzee mmoja aliyekuwa katika operesheni hiyo alichukua mshale aliokuwa nao na kuurusha kisha kumpata OCD kifuani upande wa kushoto.

  Alieleza kuwa baada ya tukio hilo, zoezi la kuwasaka wahalifu hao lilisitishwa na kumkimbiza OCD katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa ajili ya matibabu ambako alifariki muda mfupi kutokana na mshale kulenga eneo la moyo.

  Ng’hoboko pia alifahamisha kuwa watu watatu walijeruhiwa na majambazi hao walipovamia eneo hilo.

  Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Dixon Isaya (27), mkazi wa Kwa Sadala aliyekatwa mapanga kichwani na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Mawenzi.

  "Huyu Mkuu wa Polisi, Wilaya Hai ni mgeni kwani ni juzi tu amehamia Hai akitokea kituo cha Tarakea wilayani Rombo na alipandishwa cheo na kuwa OCD Hai," alisema Kamanda.

  Wengine waliojeruhiwa ni Peter Massawe (60) na Suzan Emmanuel (38) ambao wote walitibiwa na kuruhusiwa.

  “Hawa majambazi ni watu wanaowafahamu, maana jana wafanyakazi wa shamba la maua walipewa mishahara, hivyo majambazi hao walikuwa wakitaka kuwapora, lakini kwa bahati nzuri hawakuwa na fedha ndani,” alisema Ng`hoboko.


  Kamanda Ng’hoboko alisema OCD huyo atazikwa kwa heshima zote za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na familia yake iliyoko wilayani Same na kwamba mzee aliyerusha mshale huo, Fredrick Kitambi anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

  Wakati huo huo, taarifa za awali zinaeleza kuwa Kamanda Mtae alitabiri kifo chake saa chake kabla ya mauti kumfika.

  Habari kutoka Hai zilisema kuwa, juzi OCD huyo alikutana na viongozi wa kimila wa kabila la Kimasai maarufu kama Maleigwenai na kusema: “Ikibidi kufa lazima tufe, lakini uhalifu ni lazima utokomezwe wilayani Hai.”

  Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dk Norman Sigalla alisema kuwa, maneno hayo ya marehemu yametafsiriwa na wengi kuwa huenda alitabiri kifo chake, lakini kutokana na siri ya Mwenyezi Mungu hakufahamu.

  “Amekufa kishujaa akipambana na majambazi, nakumbuka kauli yake ya mwisho aliyoitoa jana (juzi) akiwaaambia Maleigwenai kuwa ikibidi kufa ni lazima tufe, lakini uhalifu lazima utokomezwe…kauli hii imenitia majonzi sana,” alisema.

  Alisema mbali na kauli hiyo, juzi marehemu aliagana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo kwa kuwaonyesha vifaa mbalimbali vya kupikia gongo ambavyo vilikamatwa na polisi katika operesheni ya siku tatu.

  Katika tukio hilo ambalo alilifanya saa 11:00 jioni, marehemu aliwaonyesha wajumbe wa kamati hiyo mapipa 38 ya kutengenezea gongo, 13 ya molasesi na lita 173 za pombe hiyo. Mkuu huyo wa wilaya alimwelezea marehemu kuwa ni kamanda aliyekuwa tayari saa zote kupambana na uhalifu na ndio maana hata alipopewa taarifa ya kuwepo kwa majambazi aliongoza kikosi cha mapambano akiwa mstari wa mbele
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mungu amlaze mahala pema peponi.
  Bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe. Amina.
  Poleni wafiwa poleni wana kwa Sadala poleni nyote.
   
 3. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha sana. Bwana alitoa, na Bwana ametwaa. Jina la Bwana libarikiwe, Amen.
   
 4. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  inasikitisha sana hii habari
  yote ni mipango ya mungu,ocd ametangulia tu kwani hii safari yetu sote hakuna atakayebakia katiak ulimwengu huu, kikubwa ni kujiandaa kwa hiyo safari.
  mungu ampe wepesi huko aendako.
  ameeeen.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  mola amlaze mahala panapostahiki
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  RIP Afande!
  Ulikuwa katika kusaidia jamii!
   
Loading...