Obama/ zitto kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Obama/ zitto kabwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Jun 17, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Takribuni kwa siku kadhaa sasa huku kwenye JF kulikuwa na mijadala kuhusu suala la Mh Zitto Kabwe kutogombea ubunge mwaka 2010 na pia katika utetezi wake amesema kuwa anataka kujenga chama na kuweza kupata uzoefu katika utawala, na pia kuongoza elimu yake pia.

  Lakini kwa watu ambao wana historia na uzoefu katika kuwa na uzoefu wanaweza kusema kuwa rais wa sasa wa Marekani alikuwa na uzoefu gani?? Je Rais Obama alikuwa Seneta kwa muda mfupi sana na hatimaye aliweza kushinda urais wa Taifa kubwa Duniani, na tena hata wale wapinzani waliweza kusema kuwa Obama hana uzoefu na Masuala ya Serikali, Yeye alikuwa Seneta wa Illions tu kwa vipindi viwili tu, Je Bwana Kabwe kusema kuwa anataka uzoefu kutoka wapi?? Je anajua kuwa Tatizo la kuwa na Yaani vyama ni electoral machines? ni kwa sababu ya Katiba ya Nchi na mfumo wa Kisiasa ambao una very centralized na Serikali?

  Hapa ni wao kukataa kwa ajili ya kubaki na Katiba ya sasa ambao kuna inavibangua vyama vya siasa, Rejea makala ya Mnyika katika gazeti Nipashe Jumapili.

  Sisi wote tunajua kuwa CHADEMA ni Chama Mbadala na pia katika siasa za Tanzania bila ya kuwa katika Mfumo ambao una sauti kama Bunge ni vigumu sana kusikika kama vile alivyokuwa Kabwe, Zitto yeye ni Mbunge na pia kwa hilo amefanya vizuri sana, katika hilo la kuwa vyama vya upinzania havina rasilimali watu ni kwamba, mtu aliwa mbunge yeye tayari ni rasilimali na ni vigumu sana mtu wa kawaida kufanya mambo kama mtu akiwa mbunge na kusaidia chama, kwanza anakuwa na sauti kwa ngazi zote, hapa ni kwasababu ya Katiba ,na sheria zetu kadhaa za Tanzania.

  Sasa kama Obama alishinda kwa kutokuwa na uzoefu na leo hii amekuwa rais wa Marekani, Je bwana Kabwe anasemaje kuhusu hili. Hoja yake kwamba anataka kupata uzoefu haina mantiki kwake na kwa Taifa, Sisi wote ni mashaidi wazuri ni M
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mbingu na ardhi!

  Btw unahitaji somo kwenye paragraphing...
   
 3. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Unafikiri Zitto angekuwa mbunge wa CCM angeingia mitini?
  Ukweli ni kwamba Zitto amegundua hakuna hope in the future akiwa CHADEMA, ndio maana ameona bora ajikite kwenye fani nyingine. Its a smart move, ila kudanganya watu kuwa sababu ni kwenda kusoma is senseless.
   
 4. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  His efforts where admirable in some cases... but futile... It was inevitable.. au alitaka aliliwe na popular uprising.." WE want zitto!" lol
   
 5. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hili suala la zito naona tumuacheni afuate mawazo yake, hapa ndani wapo watu wenye busara nyingi na wamesema mengi kuhusu bwana Zito kujitoa ubunge mwakani, kama ataona yana manufaa kwake basi achukue..Only fools never change their minds..!!
  lakini pia kingine bwana Zito hakuomba msaada kama vile yupo kwenye dilema, he is firm with his decision and he stands up to it....let him go, may be it s better for his personal ambitions, ila ajue kwamba ipo siku atahukumiwa na uwamuzi wake mana nina imani jimboni kwake bado wanamhitaji na pengine kambi ya upinzani inamuhitaji zaidi...
   
 6. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #6
  Jun 17, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Ni lazima uwaamini Watanzania. Kama Watanzania hawataki kuipigia kura Chadema,ambacho ujue ndicho Chama cha Zitto Kabwe,ujue kwamba hao watu hawajafikia kiwango fulani cha excellence ambacho Watanzania wanakitaka.
   
 7. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Nionavyo ni kwamba, Zito amekaa, katafakali na Kutathmini kwamba kama anaweza kuwamwagia Datas nyingi sana wapiga kura kama wa Busanda kuhusiana na mustakabari wa nchi yetu na nini CCM imekifanya tangu iingiee madarakani na bado wananchi wanazidi kuipigia kura CCM basi hata aje au ashuke Mungu na kuwaambia watanzania achaneni na CCM au msikipigie kura CCM, bado hawa wananchi watakipigia kura tu...

  Hivyo Hakuna maana au sababu ya kukaa kwenye siasa ili hali ukijua kwamba malengo ni kutaka kutimiza ahadi za maendelo ambazo huwezi kuzifikia kama hao CCM bado wanapigiwa kura, hivyo ni bora kutafuta njia mbadala ya kujiondoa kwa kisingizio chochote kile na ukiona upepo wa wananchi kuanza kutambua kwamba wakati wa mageuzi umewadia basi rudi na endelea na mikati ile uliyoiacha wakati ule...

  Zito pia kaona kwamba democrasia yetu bado ni changa sana na haiwezi kulinganishwa na nchi zinazoendela kama Iran, Thailand na kwingineko ambako wananchi wakiamua kuandamana lazima wapewe wanachotaka vinginevyo watawala hawatakaa madarakani kwa amani wala utulivu... Nadhani katumia busara ingawaje time will tell if he would be right for his decision to quit politics... asije akawa anakimbia mavi na kukanyaga mkojo!!!

  Kama kaona watu bado hawabadiliki kwa kuendelea kuipigia kura CCM basi ungekuwa si wakati muafaka wa yeye kukimbia kutoka ndani ya siasa kwa kisingizio cha kutogembea tena ubunge...au Labda amekwisha vuna za kutosha...maana hawezi kuwa kama chatu anayekula, kubugia na kulala usingizi totoro mpaka akamwatwe na binadamu maadui zake...
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Jun 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Zito akiondoka ktk siasa atakuwa history wala sii muda.. Hii ni Bongo wakuu zangu tumewaona wangapi?.. asijidanganye kabisa na habari za kazi ktk fani yake kuwa ni maamuzi ya busara..Wapo Wabongo kibao wenye elimu kama yake na katika fani hiyo wanapuyanga leo mwenzetu kalamba dume anataka kuliachia ati hakuna future Chadema... nani kawaambia!

  Natuma salaam kwa Zitto mwenyewe, akumbuke tu kwamba Mungu ndiye mjuzi wa yote na mara zote unapoona mwanga akakuongoza katika mema na ukafanikiwa usifanye mzaha ukabwaga manyanga kwani sii rahisi kabisa kufikia nafasi na Umaarufu alokuwa nao Zitto.

  Nachokiona ni kwamba anazima Utambi na atabakia kizani kwa sababu mitihani ya Mungu ni pamoja na kuwajaalia Mafisadi dhidi ya kila ufanyalo..Na hakika Zitto anaposema kazi ya Ubunge ni ngumu sana na mitihani yake ndio chanzo cha maamuzi yake..Huyu ni mtu ambaye wengine tulifikiria anaweza kukamata majukumu mazito zaidi.. awe waziri au rais leo Ubunge wa wilaya tena Kigoma umekuwa na mgumu kuliko alivyotegemea....
  Coime on Zitto, Mkuu fikiria tena na tena kabla hujafanya makosa haya.. Ni Muda mfupi sana Mwenyezi Mungu amekujalia kulijenga jina na nguvu ya hoja yako kuwa chombo chako..Elimu ulosomea inaingia moja kwa moja ktk hoja zako na kujenga sii lazima ushike vumbi mkuu..

  Na kibaya zaidi, ungejua kwamba Huku Majuu watu husomea hiki lakini 9 kati ya 10 hujikuta ktk profession nyingine kabisa basi wala usingweka madai ya fani ya elimu yako kuwa sababu..Na ajabu nitakwambia kwamba hawa wasomi wanaojikuta nje ya fani yao wengi wao hufanikiwa, wanaendelea na nchi zao zinaendelea zaidi kuliko sisi tunaotaka kila msomi abakie ktk fani yake...
  Huo ndio Upana wa elimu unavyochukuliwa nchi za magharibi..Elimu ni mwanga kama nuru kizani ambayo inakupa mweleko zaidi ya kile unachokifanya iwe hata kukata majani..
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0  riway aka DUCKTALES
  [​IMG]
  SINA LA ZAIDI

  next...!
   
 10. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Kwa nini tunataka kufanananisha Kunguru na Meza ?
   
 11. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watanzania lazima tujifunze na kusema kuwa lazima tufanye sana kazi ya Ziada kwa kufanya democrasia ya kweli, nafiria kuwa Zitto pamoja na Elimu yake ya Uchumi ni sehemu yake kwa kusema na kuchambua masula ya Watu na kujua na pia kama anataka kuwa rais wa siku zijazo za usoni asikimbie majukumu yake na kufanya au kuacha Giza nene kwa vijana wengi na pamoja na Taifa lote, Sisi hatutacha kupiga Kelele hizi maana naona kuwa hata wote wale mafisadi watasema kuwa kweli tumewaweza, Hivi kweli unaweza ukawa na elimu kubwa sana kama vile Prof Lipumba lakini bado watu wakaona kuwa bado hufai kuongoza, Tazama watu wengi na viongozi wenye Nia ya dhati,
  Rais wa Singapore ambaye aliifanya iwe ile kwenye Tigers countries alikuwa na elimu gani?? Hivi huyu kuacha Kazi yake na kuwa dominat politician maana yake nini?? Sisi tunamshauri Zitto achane Mpango wake huo na kama anataka kujimaliza afanye hivyo.
   
 12. J

  John74e Member

  #12
  Jun 18, 2009
  Joined: May 9, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kaka umemaanisha nini hapa sijakupata ndugu yangu ...!
   
 13. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #13
  Jun 18, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapana shaka anataka kukimbia majukumu yake na tena yeye hata kama akija siku za usoni ili agombee ngazi kubwa zaidi baada ya hii ya ubunge watu watasema alikimbia wakati alikuwa anatakiwa.

  Mtu akiwa mbunge na baada ya ubunge anaweza kuwa anafikiria urais kama ngazi yake ya mwisho kwa mwanasiasa wetu hivyo rejea maelezo yake ya awali kuhusu Waziri mkuu wa Canada na kuchukua Serikali, Alisema kuwa alianza kwa kufanya kazi na kujitolea na hatimaye chama chake kikashinda uchaguzi kwa muda unavyokwenda,
  Kwa kuwa Harper aliunganisha conservative people na kushinda dola na kuwa na wabunge wengi na inawezekani kabisa kwake,Hivyo nilijaribu kueleza nini hasa lengo lake kwa siku za usoni kwa Zitto?? Baada ya kumaliza Kusoma atakuja na kutaka Ubunge tena?? au Ngazi kubwa zaidi?? haya majibu anayo yeye mwenyewe??
   
 14. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa lazima arudi kugombea labda akishindwa kupata Ubunge ndio aende zake masomoni au anataka nini?? Uzoefu gani aliotaka maana amefanya kazi zote hizo mpaka Rais wa Ujeruman au vipi jamaani, kuwa Bungeni na pia kuwa Mbunge ni wajibu tosha kabisa na uzoefu mkubwa sana maana kudeal na watu kama wa Mwandiga ni kazi tosha kabisa, hivyo kusema kuwa kwenda masomoni na Chama mwachie nani??
   
Loading...