Obama: Time for big banks to help small businesses | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Obama: Time for big banks to help small businesses

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MPadmire, Oct 24, 2009.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,636
  Likes Received: 906
  Trophy Points: 280
  Watanzania wenzangu uchumi wa Tanzania utakua kivipi bila michango ya wananchi walio wengi.

  Wafanyabiashara wachache walio Tanzania, tena wengi wa hawa wafanyabiashara wanatoka nje ya nchi. Hawa wafanya biashara wakipata faida wanapeleka faida katika nchi zao, hapa wamekuja kuchuma tu.

  Tenda kubwa kubwa kabisa za serikali zinaenda kwa wafanya biashara wakubwa, wengi wao kutoka nje ya nchi. Eg matrekta Patel and u mention...

  Sasa basi, ili uchumi wa Tanzania ukue inabidi serikali ya Tanzania hasa sera za chama iwe kukuza uchumi wa taifa kwa kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja.

  Nchi tajiri maana yake ni kuwa wananchi wake wengi wana kipato cha kujitosheleza mahitaji muhimu na ziada, pia wanalipa kodi.

  Serikali au chama kiwe na sera ya kuwawezesha watanzania asilia, wazawa kwa maana faida hawataipeleka popote nje ya nchi.

  Mh Iddi Simba alishawahi kuongelea hili la wazawa, lakini vigogo wenzake wakampuuza. Hakuna utekelezaji, sera au mwamko. Walimpinga tu kwa sababu walifikiri anataka urais.

  Sasa basi Mabenki ya hapa nchini yatoe mikopo ya masharti nafuu, mikopo ya muda mrefu. Mafunzo yatolewe kwa watanzania, na wataweza. Watanzania sio wapumbafu, ila ni wajinga kwa asimia kubwa. Adui wa kwanza ni ujinga, ukishatoa elimu na wananchi wakaelimika basi tumeshinda ujinga.

  Kilimo kwanza si chochote kama watanzania wengi hawatapewa mashamba yenye rutuba, pembejeo,na miundo mbinu ya umwagiliaji.

  Tuachane na sera za kuwaita wawakezaji ambao faida watapeleka nchini mwao. Wawekezaji wataajiri watanzania kwa mshahara mdogo sana , ni unyonyaji na watanzania watakuwa watumwa ndani ya nchi yao.'

  Serikali itenge maeneo, ardhi ya kutosha kwa ajili ya wazawa na iwatangazie wale wanaotaka. Hekari 5 hadi 20 mwisho kugawiwa bure kwa wananchi watakaojitokeza, wenye nia ya kulima na kuendeleza. Wananchi wakopeshwe na wanachi wengi watafaidi nchi yao.

  Tatizo la ajira litapungua kama sio kuisha kabisa.

  Asanteni kwa kunisoma.
   
Loading...