Obama: Tanzania ni mfano wa kuigwa

Tanzania ni mfano wa kuigwa kweli...Hakuna sababu yeyote ya kutokuigwa?

Ukweli utabakia pale pale ni 'watu' wa Tanzania ndio wa kuigwa-Ustaaarabu,Utanashati,Uongozi wa hekima; Imechangia kukua kwa Siasa mbadala hapa Duniani-hususani Afrika.

Kuna mengi tu, ila nafikiri utendaji, haswa kizalendo, ndio unatupiga chenga.
 
Marekani inaweza kusifia hata mfu, inategemea uzuzu wa viongozi wake. Marekani haiwezi kusifia nchi zinazoendelea kwa ukweli haiwezi kusifia nchi ambazo zinakuza uchumi wake na kutoka kwenye utegemezi, haiwezi kusifia nchi ambazo zinaweza kupanga bei ya bidhaa zake ila zile ambazo inazipangia bei. Haiwezi kusifia nchi inayokuwa kwenye technologia ila ile inayokufa.

Kenya walikuwa washiriki wakubwa sana wa Marekani ila leo wanawaona kenge. Sadam alikuwa mshiriki wao ila alipoaanza kujitegemea kisiasa, kiuchumi na sayansi waliaanza kumwona hafai. North Korea kawa adui kwa sababu Technologia yake inakuwa.

hakuna cha ajabu kama kasifia hata Zimbabwe.
Miafrika bwana ...........................

Kikwete alifanya mkutano wa siri na Obama ikulu ya Marekani, akitoa sifa zisizo kuwepo. Bush akijua kampuni zao ambazo anahisa kubwa zinachota madini na kutoa sumu ya kuuwa watu huku JK akimwabudu unategemea marekani waseme nini? halafu wananchi wake (Tanzania) wamelala kama wote wamepewa Chloroform. Ujinga wa kupenda sifa zisizo sahihi unatupeleka kuzimu.
 
Yetu Masho !!!Hakuna masika yasiokuwa na Mbu,pia isisahaulike kuwa kadri usiku unavyokuwa mkubwa basi ni lazima kutapambazuka tu.
 
Yote tisa ngoja afike hapo Ghana ajionee mishuzi ya kiafrica mwenywe atafreez point.hicho kisichana cha hapo juu hamna kitu hapo.
 
msichokijua wengi ni kuwa marekani ina mission zake na hazitegemei rais ni nani! kama alianza Bush atamalizia Obama na ndio wako hivyo , CIA za na FBI haziburuzwi kijinga kama uwt,
 
Hongera JK na timu yako. Adui zako wataziponda sifa ulizopata toka kwa Obama lakini husijali wewe kanyaga twende, wananchi wako nyuma yako.
 
Hongera JK na timu yako. Adui zako wataziponda sifa ulizopata toka kwa Obama lakini husijali wewe kanyaga twende, wananchi wako nyuma yako.

Nafikiri mkuu hapa umekosema tena sana wananchi hawapo nyuma yake sio kweli, isipokuwa wananchi wapo Bega kwa Bega na Rais wao
 
Kwa nini asiseme nchi yake ya kuzaliwa ya Kenya ambayo iko juu kiuchumi na kihuduma kuliko sisi?
Wale kwanza shule ni bure kabisa sisi tunalipa.
Hospitali ndio usiseme hadi viongozi wetu wengine wanakimbizwa huko.
Lakini mimi sishangai maana hawa wamarekani wanasifia mahali wanapodhani watapata maslahi. Si ajabu kapewa ahadi ya mgodi hapo.
Masatu umesikia?
Sisi si wamarekani wala hatusubiri wamarekani kuja kuwa kipimo cha maendeleo mfu yetu. Sisi waliwanchi ndio hasa kipimo chenyewe. Tunapima wenyewe Sisi hasa tunaoishi danganyika hii na si watanzania mlioamua kuishi ulaya au kuila nchi. Pole kama mnadhani Obama atakuwa mpima mafanikio yetu.


Obama amezaliwa marekani na amekulia marekani/indonesia,kenya hajakaa wala kiswahili/kijaluo hajui
 
Wanaopinga mafanikio ya Tanzania hawana jipya. Ni bora kabisa tumesilkia wenyewe katika mahojiano ambapo rais Obama ameisifia nchi yetu na kuzitaka nchi nyingine ziige mfano wa Tanzania, vinginevyo wangebisha na kusema kuwa Obama hawezi kuisifia Tanzania.
Kwa vile sifa hizi zinapewa nchi yetu, basi hatuna budi tu-appreciate kazi nzuri inayofanywa na serikali ya utawala wa JK na wananchi kwa ujumla.

Ninaelewa vizuri kuwa kuna baadhi yetu hatuna msamiati 'hongera' badala yake tunajua msamiati 'kuponda' tu, anyway yote maisha, lakini ukweli utabakia kuwa ukweli siku zote, waasisi waliitengeneza nchi hii iwe mfano wa kuigwa katika Africa na sasa wakati umefika, wanasema!
 
....tunaambiwa kwamba Kanzu ya kuswalia ijumaa siku zote inaoshwa alhamisi.Mwiko kuosha ijumaa!!
 
[[/QUOTE] lakini na uranium ya huko kusini na mchuchuma inageuza viswahili vya akina obama

Mkuu fafanua vizuri hapo mana mi najua uranium ipo katikati ya nchi aka dodoma hususani BAHI, na kusini pia?
 
RAIS wa Marekani, Barack Obama, ameisifu Tanzania kuwa ni mfano wa kuigwa katika Bara la Afrika kwa kuwa na uongozi unaojali na kusaidia maendeleo ya watu wake. Obama amesema uongozi wa Tanzania umeonesha mfano kwa nia ya dhati ya kuwasaidia wananchi kwa kuboresha huduma muhimu za kijamii.

Rais huyo ambaye kesho anaanza ziara yake ya kwanza Afrika tangu kuchaguliwa kwake kuwa Rais akianzia Ghana, alisema jana kuwa kila atakakopita ataziambia nchi hizo za Afrika ziige mfano wa Tanzania. Katika mahojiano aliyofanya na waandishi wa tovuti ya All Africa, alisema nchi hiyo haitasita kuziunga mkono nchi zinazoonesha nia thabiti ya kuwainua watu wake.

Obama ambaye aliulizwa kama kuna nchi muhimu ambazo anazipa kipaumbele katika safari zake za kutembelea Afrika, alisema nchi zote ni muhimu lakini ujumbe atakaopeleka kwa kila nchi ni kuiga mfano wa Tanzania. “Msisahau, kwamba pamoja na kwamba ninatembelea Ghana, Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai na Rais Jakaya Kikwete wameshatembelea Ikulu ya Marekani.

“Bila shaka mmeona kazi nzuri iliyofanywa na uongozi wa Tanzania ya kuelekeza nguvu zake katika kutoa huduma kwa wananchi wake, na popote marafiki wanapotaka kujikwamua wenyewe, tutakuwa nyuma yao kama washirika,” alisema Obama.

Alisema anaamini Afrika ina uongozi mzuri ambao unataka kwenda mbele na Marekani inataka kwenda pamoja na Bara la Afrika katika juhudi zake za kujikwamua. Rais huyo alisema ushirika anaohitaji na Afrika si tu wa kutoa misaada bali wa kufungua fursa bora zaidi za kiuchumi kati ya Marekani na Bara hilo. “Hii ina maana ni pamoja na kuimarisha uwezo wa ndani ya nchi wa kujiendeleza na kuimarisha uhusiano baina ya Marekani na nchi moja moja,” alisema Obama.

HabariLeo | Obama: Tanzania ni mfano wa kuigwa
 
Kuna watu hapa hawataki kusikia jambo lolote zuri kuhusu Tanzania. Ndio tuna matatizo lakini huenda tu nafuu kuliko wenzetu wa nchi zingine za Afrika ambao wana hali kama ya kwetu.

Je hayo maneno yatufanye tukae na kushangilia? Hapana, ni changamoto kwamba tukiamua tunaweza kufanya yaliyo bora. Tanzania bado tuko nyuma na wananchi wetu wengi bado wanaishi kwa shida kubwa. Ila pia sio kweli kwamba serikali ya JK haijafanya chochote.

Tumuunge mkono JK badala ya kila siku kulalamika tu. Sisi wenyewe ndio tunaongoza kufisadi nchi badala ya kutumia muda wetu na resources zetu kujenga nchi yetu.
Give me a break, yaani: Botswana, Namibia, Angola, Kenya, Gabon, South Africa, Mozambique, Kenya, Ghana, Nigeria etc etc ziige Tanzania? Too general, tusijidanganye!!
 
Sawa Tanzania is better off than some or many other African countries but are we really better off. Kabla ya kuanza kufurahia sifa lazima tuangalie tume linganishwa na nani. Kwa bara letu lenye nchi kama Susan. Somali, Sierra Leon, Liberia. Congo etc. Kobe akilinganishwa na konokono ataonekana ana mbio zaidi. Sawa tukubali kupokea sifa lakini tujue tu kwamba we have been compared to countries which have hit rock bottom. Tujiangalie sisi wenyewe hali yetu ikoje si kufurahia kuwa kuna wenye hali taabani kuliko sisi.
 
Jamani asilimi 90 ya wanachama wa humu ni CHADEMA mnatagemea watakubalina na statement ya Obama?come on guys! hapa JF msilishangae hilo!waachane watumie haki yako ya kujieleza!endeleenei kumkosoa JK !
 
Nadhani Kikwete, Pinda, Ngeleja, Chenge, Ballali, na wenzao waende wakagombee uongozi wa Marekani, wawaongoze jinsi wanavyotuongoza sisi, halafu sisi Watanzania tuwasifie kwa kazi nzuri na kuwataka Waingereza wawaige wao!
 
ukisoma hiyo habari ya kiswahili, iliyoandika story hiyo na original story, i don't think these local writers are doing us good. See here!

Do you have priorities in terms of countries or regions? For instance, West Africa is extremely important in terms of oil; East Africa in terms of some of the strategic concerns of the United States?
I think the entire continent is important. And keep in mind that although I'm visiting Ghana on this particular trip, we've already had [Prime Minister] Tsvangirai of Zimbabwe in the Oval Office. We've had [President] Kikwete from Tanzania in my office. And in each case, I'm trying to send the same message. You've seen some very good work by the administration in Tanzania focusing on how to deliver concrete services to the people, and wherever folks want to help themselves, we want to be there as a partner. And I think that you've got some very strong leadership in Africa that is ready to move forward and we want to be there with them.

On the economic front, that means opening up better trade opportunities. It means that we are interested not just in foreign aid, but in how we strengthen the capacity for development internally in these countries, and we want to work in a multilateral context, as well as the bilateral strengthening of relations with many of these countries.

But as you point out, there are strategic, national security, economic, environmental reasons why we think this region is important. And part of the reason we wanted to - although we're only going to one country this time, I actually thought that it made sense for us to connect a trip to Ghana to a previous trip with the G8. We'll be meeting a number of African countries in Italy during the G8 meeting - before that, a meeting in Russia - to show that Africa is directly connected to our entire foreign policy approach; that it's not some isolated thing where once every term you go visit Africa for a while to check that box, but rather it's an ongoing part of a broader discussion about how we move many of these international challenges forward.

Full interview:
allAfrica.com: Africa: U.S. Wants to Spotlight 'Successful Models' And Be An 'Effective Partner' - Obama (Page 1 of 2)
 
Back
Top Bottom