Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Siku zote nimekuwa nikiamini kwamba Raisi wa ,,USA baby" Barack Obama yuko hapa kwa kazi maalumu, yaani maelite wamemuweka kwa lengo maalumu special mission ambayo ni yeye tu ndiyo anayeweza kuifanya bila ya kuzua msuguano!
Kama ilivyokuwa kwa Gadafi maelite siku zote walitaka kumuondoa Gadafi lkn nani angefanya hilo bila kuleta msuguano na nchi za Kiafrika? Sasa Obama ambaye anayejiita Mwafrika ndiye aliyemuua Gadafi hivyo Waafrika pmj na kulalamika lkn chuki yao dhidi ya ,,USA baby" inamezwa na mapenzi yao kwa ,,mtoto wao" Obama - mission accomplished!
Sasa ni zamu ya Saudi Arabia ,,USA baby" siku zote wamekuwa wakitaka kujitenga na nchi hiyo yaani kuondoa utegemezi wake hasa kwenye maswala ya mafuta, lkn ni nani ya kulifanya hilo bila ya kuleta msuguano na Waarabu ambao ni Waislamu? Jibu maelite wanalo ni Barack Huseini Obama ambaye kama walivyo Waafrika pia Waarabu na Waislamu wanaona kwamba wamepata muwakilishi ambaye ni Raisi wa ,,USA baby" wa kwanza Muislamu au mwenye jina la Kiislamu kumbuka hotuba ya kwanza ya Obama aliyoitoa nje ya ,,USA baby" ilikuwa ni Cairo, Misri na alijitambulisha kama Huseini Obama sasa ,,USA baby" kwa mara ya kwanza chini ya Obama inakatisha mahusiano na Saudia tayari Raisi Obama amesimamisha supply of cluster bombs kwa ufalme wa Saudia hii ni mara ya kwanza kutokea hakuna Raisi wa ,,USA baby" aliyewahi kufanya hivi hasa ukichukulia uhusiano mkubwa uliokuwepo kati ya Saudia na nchi hiyo!
Rejea mahusiano ya Cuba na ,,USA baby" ambapo siku zote Marekani walitaka kurudisha mahusiano na nchi hiyo lkn ni nani angelifanya hilo? Yaani ni Raisi gani wa ,,USA baby" ambaye Castro angeweza kumuamini? Rejea communist background ya Barack Obama ambapo inajulikana kwamba baba yake Obama senior alikuwa ni mkomunist na mama yake Ann Dunham (ambaye ni Mzungu) pia alimkuwa ni muumini wa siasa za mlengo wa kushosto leftist hivyo wanamlink Obama (Raisi) na ukomunisti hiyo imeweza angalau kumuweka Obama karibu au nisema kupata imani ya Castro, rejea Castro alivyosema siku Obama alivyoshinda uchaguzi hajawahi kuongea kitu positive kwa Raisi yoyote wa ,,USA baby" lkn kwa Obama aliongea na hivi majuzi Obama kwa mara ya kwanza alienda Cuba na bendi ya The Rollin stone ilifanya show ya kufa mtu Cuba, ikumbukwe kwamba Cuba ni muhimu sana kwa ustawi wa ,,USA baby" rejea cuba missile crisis- mission accomplished!
Ukija kwenye swala la haki za Mashoga na transgender hakuna Raisi wa ,USA baby" aliyekwenda mbali kwenye kuhalalisha haya mambo kama Barack Obama, na hapa kete kubwa ya Obama ni kwamba yeye amefika hapo kwa sababu ya watu walijitolea kuondoa/kupunguza ubaguzi ,,USA baby" hivyo kama iliwezakana kwa ,,mtu mweusi" kuwa Raisi wa ,,USA baby" pia inawezekana kwa mashoga kuishi na kuwa haki sawa kama raia mwingine yoyote yule, Sasa ni nani wa kumpinga Obama kwenye hili?
wewe mweusi ukipinga utaambiwa mbona ubaguzi dhidi yako umepunguzwa kwa nini usipunguzwe dhidi ya mashoga, transgender &Co.? Huyo ndiyo na mengine mengi tu yanakuja na tutayashuhudia kabal ya barack obama kumaliza muda wake ...