sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Sisi sote ni mashuhuda wa historia ya nchi hii kwa kumbukumbu mbalimbali ambazo leo hii zimekuwa kama hekaya kwa vizazi vijavyo.Hali ya uchumi na mfumuko wa bei ukiendelea kushika kasi huku wananchi wakiendelea kuishi chini ya dola moja ya kimarekani.
Tanzania ya leo haina tofauti sana na enzi Za akina Sultani Mangungo wa Msovero,kwa kujiona mwema na kukabidhi ardhi yake kwa wakoloni kwa kupewa shanga na nguo akimini watamsaidia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali katika ushindani wa kichifu miaka dahali iliyopita.
Ni bora sana na sultani huyo hakuwa na elimu ya kutosha japokuwa aliongozwa na fikra,kuliko viongozi wetu waliosoma lakini wakashindwa kusoma alama za nyakati na kukabidhi ardhi yetu kwa wageni wanyonyaji huku nchi ikisheheni migogoro mikubwa ya ardhi katika ya wafugaji na wakulima.
Nilishawahi kusema migogoro ya ardhi ndani ya nchi yetu italiangamiza taifa na kuwaacha waliopewa dhamana ya uongozi wakitumbua raha ughaibuni.Hali ya nchi ni tete kwasasa lakini rais wa nchi hana wasiwasi,kazi yake kukwea pipa kwenda kufanya umatonya kwa sifa ya kurudi na kibaba huku nchi ikizidi kuteketea.
Yaliyo jiri leo hii huko Ikwiriri kati ya vita ya wafugaji na wakulima ina dhihirisha hali ya nchi si shwari.Ilipoanzia Babati watu walipuuzia lakini sasa si Ubakuru huko Mbarari pekee bali moto huu unazidi shika kasi pembe zote za nchi.Hali hii inashika kasi kama moto wa petrol huku rais wa nchi akizidi kuwalika wawekezaji kuja kuwamiliksha ardhi yetu kitu ambacho kitaleta mgogoro mkubwa mwingine kama ule uliosababisha vita vya maji maji kushika kasi.
Kinacho sikitisha kwa nchi hii ni ardhi kugawiwa wageni huku nchi ikiwa na uhaba mkubwa wa chakula karibu kila mwaka.Nchi imekosa mwenyewe,kiasi kimuonekano ni kama nasi tumeuzwa tunasubiri kukabidhiwa kwa mnunuzi.
Kitendo cha rais wetu kualikwa kwenye mkutano wa G8,ni lazima tulitafakari kwa kina nini hasa makakati wa weupe hawa na ahadi zao lukuki.Tunashindwaje kukumbukla yaliyopita yaliyo wakuta machifu wetu nasi leo kuingia kwenye mtego ulel ule.Tofauti na wakati ule wakoloni walikuja wenyewe lakini leo tuna wafuata huko huko kwao na kuwakaribisha kuja kuchukuwa hata kile kilichokombolewa na mababu zetu mara baada ya kujitambua walifanya makosa.
Urafiki huu wa mashaka na weupe hawa utatufikisha wapi kama si kujichimbia kaburi letu sisi wenyewe.Tumeona yaliyotokea huko Zimbabwe,si miaka mingi lakini hatuna kumbukumbu zozote,tumekuwa vichwa panzi makamasi yametawala mpaka akili zetu.
Tuna hitaji mapinduzi ya kifikra na kuacha kuwa tegemezi hata kwa shughuli zetu za maendeleo.Jirani zetu wanapiga hatua kubwa kujikomboa kwa kujiendesha wenyewe kiuchumi wakati sisi tumeshika kasi na kuwa taifa omba omba,hali hii mpaka lini?
Ehud Barak alipotubeza kuwa sisi ni irrelevant,tulipiga sana kelele lakini leo yanayojiri ni yale yale aliyoyasemea.Tunaposutwa na kero zetu kwa weupe hawa tunalaani kwa nguvu zote,lakini tuna shindwa kupambana na wakati.Ifike mahali tupige hatua kimaendeleo bila kutegemea misaada ambayo itakuwa kero kwa vizazi vijavyo.