Obama Awa Rais wa Kwanza Marekani Kuambiwa 'Muongo' Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Obama Awa Rais wa Kwanza Marekani Kuambiwa 'Muongo' Bungeni

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Sep 12, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais wa Marekani, Barack Obama Thursday, September 10, 2009 11:14 PM
  Rais Barack Obama wa Marekani, amekuwa rais wa kwanza wa Marekani kuambiwa muongo mbele ya maseneta wa bunge la kongresi. Rais Barack Obama wa Marekani, amekuwa rais wa kwanza katika historia ya Marekani kuambiwa muongo wakati akitoa hotuba yake kwenye bunge la kongresi la Marekani.

  Seneta wa South Carolin toka chama cha upinzani cha Republican, Joe Wilson aliropoka kwa hasira "Unaongopa" kumwambia Obama wakati Obama alipokuwa akisoma hotuba yake kuhusiana na mageuzi anayotaka kuyafanya kuhusiana na masuala ya bima katika sekta ya afya ya Marekani.

  Tukio hilo lilitokea wakati Obama akiwa amefikia karibia nusu ya hotuba yake ya dakika 40 wakati alipokanusha taarifa potofu zinazotolewa na wapinzani wake kuwa mageuzi hayo katika bima za afya yatatoa mwanya kwa wahamiaji holela.

  Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph la Uingereza, Obama amekuwa rais wa kwanza wa Marekani kuambiwa muongo wakati akisoma hotuba yake kwenye bunge la kongresi la Marekani.

  Kitendo hicho cha seneta Wilson kilizua kelele za "Aibu, Aibu" toka kwa maseneta wa chama cha Democratic.

  Obama alimwangalia kwa mshangao seneta Wilsona na kusema "Sio Kweli" na kisha aliendelea na hotuba yake.

  Mke wa rais Obama, Michelle Obama, akiangalia toka jukwaani alitingisha kichwa chake akionyesha kuchukizwa na kitendo hicho.

  Hata baadhi ya maseneta wa Republican walionyesha kuchukizwa na kitendo cha Wilson kutoonyesha nidhamu kwa mkuu wa taifa hilo kubwa duniani.

  Akiongea na CNN baada ya hotuba hiyo seneta wa Arizona, John McCain ambaye alikuwa mpinzani wa Obama katika uchaguzi wa urais uliopita, alisema kuwa kitendo cha Wilson ni cha aibu na aliongeza "Hakuna nafasi ya vitendo kama hivi kwa mtu yoyote yule, lazima amuombe radhi".

  Wilson alikumbwa pia na hasira za wananchi na ilijitokeza kuwa watu wengi walianza kumsapoti mpinzani wake katika kiti cha useneta wa jimbo la South Carolin toka chama cha Democratic.

  Baadae Wilson alimuomba radhi Obama kwa kitendo chake hicho akisema kuwa alishindwa kuzidhibiti hisia zake.

  Wilson alijaribu kumpigia simu Obama kumuomba radhi lakini simu zake ziliishia kupokelewa na maafisa wa White House.

  Kwa mujibu wa mageuzi ambayo Obama anakusudia kuyaleta katika mfumo wa afya wa Marekani, serikali ya Marekani itadhamini bima ya afya kwa wananchi wake wote na wastaafu watalipiwa bima zao na serikali.

  Rais Obama kwa kukumbushia majaribio ya marais waliopita kufanya mageuzi hayo na kushindwa, alisema kuwa yeye siyo rais wa kwanza wa Marekani kujaribu kufanya mageuzi kwenye mfumo wa Afya lakini amejiandaa kuwa rais wa mwisho kufanya hivyo.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3053954&&Cat=2
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii ndio Demokrasia hata Kama hutaki ila kwa Tanzania huwezi kufanya hivi hata siku moja by the way huyu Wilson alikuwa katika hasira na ndio maana alikuwa katika hali kama hiyo
   
 3. J

  Jamil Member

  #3
  Sep 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ningependa kujua kama huyu mtu ni mweusi au mweupe na kama ni mweupe wala hata sishangazwi na kitendo hiki maana wazungu wantudharau mno wa-ngozi nyeusi pale alijisahau hakujua kuwa jamaa sasa ndie kichwa...na nafikiri hadi leo hii wengi wa ngozi nyeupe hawaamini kuwa wanatawali na ngozi nyeusi..haya ni mambo ya Mungu yasiyowezekana kwa mwanadamu...Mungu hutumia watu walodharauliwa na wanyonge katika kufanikisha mipango yake hata wewe pia yawezekana una kitu ndani yako kwaajili ya taifa lakini hujiamini napenda nikutie moyo songa mbele utafanikiwa.

  Man of People and Voice of Weaker
   
 4. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bila shaka Seneta Joe Wilson ana chembe chembe za ubaguzi ingekuwa rais ni mweupe asigethubutu kufanya utovu wa nidhamu alioufanya.
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nadhani kwa Tanzania inawezekana zaidi ya hapo,
  Umesahau mshikaji aliyemzaba Mh. Rais wa Awamu ya pili, Mh. sana Rais Ali Hassan Mwinyi?

  Aliposema hakubaliani na hotuba ya Mh. Rais Mstaafu?
   
 6. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35


  huyu hakuropoka kwa sababu mpango wa obama wa bima ya afya mbovu, bali ubaguzi na kutokukubali kama black people is now leading the state..inamuumiza moyoni na kashindwa kuvumilia
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Sep 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Wilson ni mzungu.
   
 8. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wilson mwenyewe ameshaomba msamaha hii ina maana alichofanya ni makosa.

  Demokrasia haina maana ya kuzomeana au kutukanana au kupigana mangumi.

  Nyerere alisema "Uhuru bila nidhamu ni fujo na nidhamu bila uhuru ni utumwa" Kinachotakiwa ni balance nzuri kati ya uhuru na nidhamu.
   
 9. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #9
  Sep 12, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Baada ya kelele zake tu, anayetaka kumondoa ubunge akachangisha a record dola laki nne papo kwa papo, ina maana huyu Wilson ameshajua kua hakubaliki jimboni kwake anatafuta njia ya kutokea, he is done!

  Respect.

  FMEs!
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,559
  Likes Received: 1,916
  Trophy Points: 280
  Mkuu FMES,Wilson na yeye keshachangiwa zaidi ya dola laki saba tangu amwite Obama Mwongo. Pia ni mmojawapo wa wale maconfederates,wazungu wenye siasa zenye mrengo wa kibaguzi ambaye alipiga kura za kuendeleza ubaguzi na kukeep ile bendera yao.
   
 11. J

  JokaKuu Platinum Member

  #11
  Sep 12, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  FMES,

  ..nilisoma hiyo habari kwamba mpinzani wa Wilson kachangiwa mahela kibao baada ya kitendo cha kuzomewa Obama.

  ..sasa naona wapambe wa Wilson nao wamekuja na counter move kama jmushi1 anavyotuhabarisha.

  ..inavyosemekana Obama anaweza kupitisha hizo changes bila kuwashirikisha Conservative Republicans, isipokuwa anajaribu kuwa muungwana.
   
 12. k

  kasyabone tall JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2009
  Joined: Sep 13, 2009
  Messages: 255
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 33
  "Hekima ni Uhuru" by mwalimu Nyerere
   
 13. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #13
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,617
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280

  - Kumzomea rais wa jamhuri tena mbele ya Congress, ni dalili za utovu wa adabu na kutoelewa maana ya civilization, huyu Wilson anamsaidia tu Obama kupata term ya pili easily.

  Ahsante.

  William.
   
 14. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Wilson hana lolote, kilichomjaa yeye ni chuki zidi ya watu weusi. Ujue kuna baadhi ya wazungu hadi leo hawaamini kwamba mtu mweusi ndio rais wao, na bado wana dharau kwa watu weusi.
   
 15. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Well said Mukulu.
   
 16. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #16
  Sep 16, 2009
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,617
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  House votes to rebuke Rep. Wilson

  Vote is 240-179 in the wake of ‘You lie’ outburst by S.C. Republican

  Wilson: ‘The issue is over’
  Sept. 15: Rep. Joe Wilson, R-S.C., says it's “time to move forward" after Democrats introduce resolution of disproval against him for yelling "you lie" at President Obama.

  updated 5:42 p.m. ET, Tues., Sept . 15, 2009
  WASHINGTON - Bitterly divided over an accusatory outburst — "You lie" — lawmakers voted Tuesday to admonish one of their own for his jarring interruption of President Barack Obama.

  The resolution of disapproval against Republican Rep. Joe Wilson added to the already-toxic atmosphere of partisanship in the House. Democrats said Wilson's behavior during Obama's speech to Congress last week was an egregious display of disrespect that could not be ignored. Republicans accused the majority party of hypocrisy and wasting the taxpayers' time.

  "At issue," declared House Majority Leader Steny Hoyer, "is whether we are able to proceed with a degree of civility and decorum that our rules and our democracy contemplate and require."

  Wilson, speaking after Democrat Hoyer, refused to back down. "I think it is clear to the American people that there are far more important issues facing this nation than what we're addressing right now." He said Obama had "graciously accepted my apology and the issue is over."

  The Office of the House Historian said the resolution, which passed 240-179, marks the first time in the 220-year history of the House that a member has been admonished for speaking out while the president was giving an address. A resolution of disapproval is less severe than other disciplinary action available to the House, including censure or expulsion.

  The resolution said Wilson's conduct was a "breach of decorum and degraded the proceedings of the joint session, to the discredit of the House."

  Wilson's "You lie" outburst came as Obama, during a joint session speech on health care legislation, said that illegal immigrants would not be eligible for federal subsidies to purchase health insurance.

  The shout drew gasps from other members, and Wilson, at the urging of Republican leaders, called White House chief of staff Rahm Emanuel to apologize. But he has resisted later suggestions that he go to the House floor to express further remorse.

  "I think that Mr. Wilson could have resolved this himself" by speaking directly to his House colleagues, Hoyer said.
   
 17. Brutus

  Brutus Senior Member

  #17
  Sep 16, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  We are wrong to label the Oppositions & Criticism to Democrats' Healthcare Reforms and Big spending as racial related issues. What's happening is like giving the whole town free bus tickets without adding the number of buses, and drivers. It is a mess! US healthcre needs reform, but some of the proposed reforms are ridiculous!
  It was okay to call G W Bush all the names, but when the equation is reversed now it is a crime! What a democracy!
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Sep 16, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  You tell them! These folks were happy when G.W. got a shoe thrown at him. They said they wished it had hit him. They called him every name in the book. They booed him at the 2005 state of the Union address. They camped outside his Crawford, Texas home. But when it comes to Obama, any opposition against him (his policies and decisions) it's racist. If you are white and you criticise Obama you are racist. If you are black and you criticise him you are an uncle Tom.
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Ni Raisi wa kwanza kuwa na asili ya kiafrika na huu ni mwendelezo tu wa kuendelea kukalia namba moja ya siasa za marekani
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Sep 16, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Lawmaker sorry for heckling Obama!


  [​IMG] Mr Wilson said his emotion got the better of him during the speech

  A Republican lawmaker has apologised for his "You lie!" outburst during US President Barack Obama's key speech on healthcare reform in Congress.


  Joe Wilson, a congressman from South Carolina, said: "I extend sincere apologies to the president for this lack of civility."
  Both Democrats and Republicans swiftly denounced his behaviour.
  Mr Wilson's outburst came after the president said illegal immigrants would not benefit from his healthcare plans.
  Mr Obama replied to Mr Wilson's remark "That's not true" before continuing his speech on Wednesday evening.


  '"Totally disrespectful"

  "I let my emotions get the best of me," Mr Wilson said in a statement.
  "While I disagree with the president's statement, my comments were inappropriate and regrettable."
  The lawmaker also tried to call the president to apologise personally, but ended up talking to White House Chief of Staff Rahm Emanuel instead, Mr Wilson's office said.
  House Majority Leader Steny Hoyer, a Democrat from Maryland, said the congressman "ought to apologise to the House as well".
  Mr Hoyer told MSNBC the incident was something that "in 29 years I have never heard said in a presidential speech on the House floor".
  House Minority Whip Eric Cantor, a Republican from Virginia, also criticised Mr Wilson's behaviour.
  "Obviously, the president of the United States is always welcome on Capitol Hill. He deserves respect and decorum," he told ABC.
  Vice President Joe Biden said Mr Wilson's outburst "demeaned the institution", while Senator John McCain, Mr Obama's Republican rival in the 2008 presidential polls, said such behaviour was "totally disrespectful".


  Source: http://news.bbc.co.uk/2/hi/americas/8248750.stm
   
Loading...