Obama atufunza Tanzania migomo ishughulikiwe kwa tahadhari na kuitafutia uvumbuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Obama atufunza Tanzania migomo ishughulikiwe kwa tahadhari na kuitafutia uvumbuzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 19, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Majuzi tu hapa niliweka mada inayoonyesha mgomo wa walimu huko Chicago nchi Marekani ambapo hata wanafunzi walihusishwa katika kutetea haki za walimu wao.

  Mgomo huo ambao umedumu kwa karibu wiki zima bila walimu kuingia madarasani, hatimaye meya wa jiji la Chicago ambaye awali alikuwa mshauri mkuu wa Rais Obama,
  Mstahiki Mayor Rahm Emanuel kuridhia matakwa ya walimu na hatimaye walimu kusitisha mgomo na kurejea madarasani.

  [​IMG]
  M. Spencer Green - Teacher Patty Westcott pickets outside Clissold Elementary School in Chicago, Tuesday, Sept. 18, 2012, as a strike by the Chicago Teachers Union continues into its second week. CTU members in the nation's third-largest city will pore over the details of a contract settlement Tuesday as the clock ticks down to an afternoon meeting in which they are expected to vote on ending a seven-day strike that has kept 350,000 students out of class.

  [​IMG]

  Sitthixay Ditthavong - A young girl plays a toy horn as striking Chicago teachers rally Saturday, Sept. 15, 2012, in Chicago.
  Union president Karen Lewis reminded that although there is a "framework"
  for an end to their strike, they still are on strike.

  Kwa habari zaidi soma:
  Teachers suspend Chicago school strike


  Maana yangu ya kuleta mada hii si kujadili mgomo uliotokea huko Marekani, bali serikali yetu inajifunza nini kwa tukio la mgomo wa walimu kwa wiki nzima kudai haki na masilahi zaidi , mgomo ambao ulishirikisha hata wanafunzi kutetea walimu wao,


  • Mgomo kama huko ulitokea nchini hivi karibuni, tulichoshuhudia ni:
  • Walimu kutishiwa kufukuzwa kazi
  • Walimu kunyimwa zoezi la ajira ya muda kufanya sensa
  • Kusalitiana kwa walimu
  • Serikali kutoa vitisho mbalimbali dhidi ya walimu
  • Watoto walioshiriki kuishinikiza serikali polisi waliwapiga mabomu.

  Marekani mgomo umeenda kwa utulivu huku majadiliano yakiendelea hadi walipofikia maafikiano ya serikali kuridhia madai yao, wamerudi madasani na nguvu mpya ya kuwajenga vijana kwa ajili ya kizazi kijacho.
   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Tofauti ni kwamba for the case of Chicago, mwezi June kutakuwa na masomo zaidi wiki moja kufidia muda wa mgomo.
  Mgomo umepangwa immediately baada ya likizo ili usikatishe masomo katika semester.

  Kwa Tanzania tunagoma irresponsibly, hakuna fidia au mkakati wowote wa kucatch up baada ya mgomo.

  Vilevile, mgomo wa Chicago una madai ambayo utekelezaji wake uko obvious na wagomaji wanauchambua explicitly. Ugomaji wa Bongo mwajiriwa anataka mshahara uongezwe asilimia 300 immediately, hana mchanganuo how, why etc!

  Tuna mengi ya kujifunza.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Dhahiri mgomo wa Chikago ni wa watu wa kiwango chao. Pamoja na hayo namna ya mgomo ulifanyika na mazingira mengi yanaelekea kufanana mfano watoto kushirikishwa na bila kuleta athari kwao kutoka vyombo vya dola.

  Pamoja na kwamba madai ya walimu Chikago yako wazi na rahisi kutekelezeka, sitegemei kama mengi au yote yanakubaliwa, kuna ambayo wamekubaliana na yapo ambayo serikali imeomba wawe na subira kutokana na hali halisi au kuwajulisha wazi ugumu wa utekelezajiwake.

  Ninachoona cha msingi ni jinsi amani inavyotunzwa na kuheshimiwa katika migomo ambayo haina vurugu au hatari ya uvujaji amani. Walipoandamano walimu Tanzania hwakuwa na silana na wale watoto walikuwa wanataka walimu wao wapate wanachodai ili kuwatengenezea mazingira mazuri ya elimu kama wenzao wa Chicago walivyofanya, kinyume chake Tanzania ni kulipuliwa na mabomu na kutishiwa usitishwaji wa ajira zao na mangineyo.

  Pamoja na mazingira tofauti, lakini kuja jambo la msingi ambalo hatutofautiani kwa namna ya pkee sana.
   
 4. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Sawasawa kabisa. Nimesoma maoni ya wananchi wa Chicago, inaonekana hawakuwaunga sana mkono walimu kwa sababu wanasema walimu wanalipwa vizuri na watoto wao hawasomi public schools. Pia nimeona wanawalalamikia sana polisi Chicago in general kuwa wanawaonea raia. Swala la polisi na raia inaonekana ni problem sehemu nyingi.
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Huu hapa mfano wa polisi anayeshukuru kuwa mgomo ulifanya wananchi waelekeze kwa walimu hasira ambazo siku zote huwa nazo kwa polisi. Kwahiyo polisi wakapungua kuchukiwa kwa kipindi cha mgomo.
   
 6. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Huu hapa mfano wa polisi anayeshukuru kuwa mgomo ulifanya wananchi waelekeze kwa walimu hasira ambazo siku zote huwa nazo kwa polisi. Kwahiyo polisi wakapungua kuchukiwa kwa kipindi cha mgomo.
   
Loading...