Oa au olewa na Mzanzibar ili mtoto wenu awe na hadhi + uwanja mpana wa kufanikiwa (Zanzibar citizenship privilege)

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
1638958811060.png


Soma kwa makini, hakika utakuwa umemrahisishia maisha mtoto wako, wa kuuchukua uamuzi ni wewe mzazi wake mtaajiwa.

Wengi wanaweza kudhani hii maada nimeianzisha kwasababu raisi wa sasa ni mzanzibari, la hasha!! Uraia wa Zanzibar una hadhi ya juu sana kuliko huu uraia wa Tanzania tangu zamani.

Kwanini uoe au kuolewa na Mzanzibari?

Idadi ya wazanzibari ni ndogo takribani milioni 1 na nusu, lakini muungano unawapa nguvu (power), influence, ajira, n.k kubwa sana kuzidi kundi au kabila lolote unalolijua na ndio maana nakushauri upigane kufa kupona ili mtoto wako aingie hili kundi.

Moja ya njia ya kupata huu uraia mtamu ni mtoto kuwa na mzazi moja mwenye uraia wa Zanzibar, kwa hio ukioa au kuolewa na mzanzibari, mtoto weny atakuwa raia wa kizanzibari.

FAIDA ATAZOPATA MTOTO WAKO AKIWA RAIA WA ZANZIBAR

A. Kuwa katika kundi lenye nguvu kubwa kuzidi kabila lolote

1638810914974.png


Ujumbe wangu hapa ni kwamba, nafasi ya mtoto wako kupata nafasi za uongozi aidha kwa huku bara au Zanzibar ni mkubwa endapo atakuwa ni raia wa Zanzibar maana wapo wachache takribani milioini 1 tu na wana fursa ya kupata vyeo vingi sana tofauti na huku bara kwenye watu milioni 60 wanaopambania vyeo vichache.

Ili kuwe na muungano ni lazima kuwe na mchanganyiko wa pande mbili katika uongozi, mamlaka, maamuzi na hata hizo ajira. Na ndio maana hata kwenye nafasi za uraisi au makamu wa raisi inabidi kuwe na pande mbili (Zanzibar ndio jamii pekee inayotoa rais au makamu wa rais kila mara lakini haijawai kutokea kabila flani kutoka bara kujirudia kupata hivyo vyeo kama ilivyo kwa Zanzibar wanavyojirudia miaka nenda rudi kupata Urais na umakamu ) hata kwenye vyeo vingine vikubwa lazima mzanizbari awepo, kwenye mawaziri lazima Zanzibar iwepo, uko jeshini jwtz lazima wawepo majenerali na maluteni wazanzibari, polisi inabidi kuwe na ma rpc kutoka Zanzibar, n.k. hivi ni vyeo vizito haswaa vyenye powe na influence kubwa sana. Mchaga, msukuma, mhaya, mnyakyusa, mpare, n.k wanabadilishwa mda wowote na anawekwa mwengine lakini hadhi ya nafasi ya Mzanzibari inabaki pale pale tu. Hali hii inawafanya wawe jamii yenye nguvu kubwa kuzidi kabila lolote ulijualo hapa bara, hii pia inawasaidia mno kwenye kushikana mkono, mkuu wa idara flani akiwa mzanzibari anaweza kupandisha wenzake vyeo, kuwapa wenzake kipaumbele kwenye ajira, n.k. Ukiachana na nguvu waliyo nayo huku bara, bado wana serikali yao ambayo raisi, makamu wa raisi, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugezi wa taasisi, majaji wa mahakama, wabunge, n.k ni lazima wawe wazanzibari.


B. Urahisi wa kupata ajira za bara

1638795467920.png


hapa nazungumzia ajira za muungano kuanzia wizara mbali mbali, jwtz, usalama wa taifa, ikulu, tra, benki kuu, bandari, polisi, tbs, n.k. mtoto wako ukimkazania apate hizi diploma au degree ambazo zimejaa kama utititiri kwa watu wa bara, nakuhakikishia itakuwa ni tiketi kubwa sana ya mtoto wako kula mema ya nchi kwenye ajira za muungano, katika huu muungano kuna makubaliano kwamba katika kila nafasi 100 inabidi wawepo wazanzibari 21 sawa na asilimia 21, nakukumbusha kwamba katika watanzania 100 kuna wazanzibari wawili tu, kwao hizo nafasi ni nyingi sana na kuna muda huwa hawazijazi.

huko kwenye interview kigezo kinachoangaliwa zaidi ukiwa na mtoto mzanzibari kitakuwa ni uraia wake maana kwanza wanakuwaga wachache ila kwa upande wa mtoto wa bara ushindani ni mkubwa mno usipime!! Makumi ya maelfu ya wanafunzi humaliza vyuo kila mwaka na wengi hubaki mtaani, ajira zikitangazwa ni vurugu, yani hadi upate kazi ni shughuli pevu si mchezo, utachunguzwa hadhi ya chuo ulichosomea, ufaulu wako chuoni (gpa), umejitolea kwa miaka mingapi kwenye mashirika ili upate zoefu, uzito wa cv yako, n.k. Hata huko vyuoni, mzanzibari sio wa kumdharau eti kisa ana ufaulu mdogo, hapo mkimaliza chuo, wabara waliokuwa wanafaulu vizuri wanaweza kusota sana kupata ajira lakini mzanzibari huyo huyo aliekuwa na ufaulu mdogo anapata ajira fasta tu, tena cheo kizuri tu. sasa uchaguzi ni wako kumuingiza mtoto kundi jepesi ama hili lenye mikiki mikiki.

C. kupata ajira za zanzibar ambazo raia wa bara hana sifa

1638795848755.png


Serikali ya zanzibar kuna bunge lao, wizara zao, ikulu, n.k ambako wanaajri wazanzibari tu. pia kuna ma mia ya taasisi na mashirika yao ambayo hutoa ajira kwa wazanzibari pekee, mfano tanesco yao inaitwa zeco, tra yao inaitwa zrb, tff yao inaitwa zff. Nssf yao inaitwa zssf, tbs yao inaitwa zbs, n.k.

Ukiwa na mtoto ataekuwa na uraia wa Zanzibar basi inawezekana kabisa mmoja akaajiriwa ajira za muungano Tra mkoani Mbeya na mwengine akaajiriwa taasisi ya Zanzibar kama Zrb, zff, zeco, n.k. Ukiwa na mtoto wa bara hataweza kuajiriwa hizo taasisi za Zanzibar nilizozitaja huko labda itokee hawana wataalam husika. Wala nisikuumize sana kichwa, kiufupi ni kwamba mtoto wako akiwa mzanzibari ataua ndege wawili kwa jiwe moja tu maana ajira za huku wazanzibar wana mgao wao mzuri tu wa asilimia 21 na huko kwao wana ajira nyingi ambazo zipo kwajili yao.

D. kufaidi vitu vya pande zote mbili bila vikwazo

1638962948189.png


Tukiachana na vitu ambavyo nishavizungumzia awali kama kupata ajira au nafasi za uongozi kweny serkal ya Tanzania na pia kweny serkali yao ya zanzibar pia kuna vitu vingine ambavyo mtoto wako akiwa mzanzibar atavipata huku wa bara akiteseka.

Ardhi - hapa mtoto wako akiwa mzanziabari anaweza kumiliki ardhi huko Zanzibar na huku pia anaweza kumiliki viwanja, mashamba, mapori, n.k. Endapo atakuwa mbara basi ataweza kumliki ardhi ya huku bara tu, huko Zanzibar hataruhusiwa kumiliki ardhi.

Uraia - ukiwaraia wa zanzibar basi una uraia wa pande mbili, utanzania a uzanzibari, wao wana vitambulisho vyai vya uraia wa Zanzibar na vinawapa uraia wa pande mbili, kwa upande wa kitambulisho cha mtanzania kinakupa uraia wa bara tu, hapo zamani kidogo ili kuingia Zanzibara kama unatokea bara ilibidi uwe na paspoti ili kuingia Zanzibar kama mtu anaeenda nchi nyingine lakini wazanzibar hawakuhitaji hizo paspoti kuja huku.

Leseni ya udereva - Mzanzibar anaweza kutumia leseni yake huku bara bila matatizo yoyote lakini leseni ya udereva iliyotolewa huku bara ukienda nayo kule itakupa shida.

E. Kuendeleza kizazi cha kuwa na Watoto / wajukuu wataofaidi mema ya muungano

1638727190761.png


kwa kuwa mtoto wako atakuwa ni mzanzibari, basi hata Watoto wae na wajukuu watakula mema ya huu uraia miaka nenda rudi,

...........................................................................................

Kuifupi uraia wa zanzibar una hadhi kubwa sana na pia wazanzibar wana umoja sana, wakifanya kitu basi wanahakikisha kinawfaidisha watu wao, haya mnayoana kwa sasa kwa upande wa Zanzibar ni maogo sana, mtegemee makubwa ya kushangaza maana kwa sasa wazanzibari wengi wamepata mwamko wa elimu na pia wengi sikuhizi wamehamia huku bara kula mema ya muungano.
 
Ni kuharibu mbegu ,hawa ni wavivu na legelege sana halafu wanaabudu sana uarabu na utwana
Mwenzako anapunga upepo kibarazani huku akiburudika na urojo usimuone legelege, tayari ana uhakika wa kula, mavazi, malazi, n.k. ana ndugu zake kadhaa wenye vyeo wanaomtumia hela za kujikimu, kufanya kazi ni hiari yake, wewe ukibaki kibarazani utakufa njaa aisee , katafute kibarua hata cha kupasua kokoto ilimradi upate pesa ya kula, ukimuiga mzanzibari utalala njaa tu 😂 😂

wana msemo wao sasa sijui kama ni utani au dharau....Mzigo mzito mpe mtanganyika ataufikisha tu.
 
Zanzibar ndio jamii pekee inayotoa rais wa Tanzania kila mara. Kabila lolote Tanzania bara likitoa Rais.. lijue kabisa halitajirudia kutoa Rais tenaaa.. ila wa Zanzibar wanajirudia rudia tu kupata U rais wa Tanzania kila baada ya awamu kazaa
 
Pamoja na Zanzibar kua ndogo ina asilimia kubwa ya wasomi ambao hawajaajiliwa na serikali yao badala yake wamepata kazi kwenye miradi, ambao pia kwa uwezo wao wangeweza kuisaidia sana nchi, sasa mpaka wao wakija vyuo vya bara wanatafuta kazi huku kwanini mimi nitake kua na uhusiano na Zanzibar?!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom