Nzige watangazwa kuwa janga la kitaifa Somalia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Nchi ya Somalia imetangaza uvamizi wa nzige katika maeneo mbalimbai ya nchi hiyo kama janga la kitaifa huku Wizara ya Kilimo, ikisema kuwa hatua hii imefikiwa baada ya wadudu hao kuendelea kuharibu mimea na sasa hali ii inatishia kuwepo kwa uhaha wa chakula nchini humo.

Kuna wasiwasi kuwa, huenda ikawa vigumu kudhibiti nzige hao, kabla ya msimu wa mavuno mwezi Aprili mwaka huu.

Umoja wa Mataifa umesema, huu ndio uvamizi mkubwa wa nzige kuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa kipindi cha miaka 25 hali ambayo pia imeathiri nchi jirani ya Ethiopia.

Somalia imekuwa nchi ya kwanza, kutangaza uvamizi huo kama janga la kitaifa, wakati huu nchi jirani ya Kenya ikikabiliwa pia na gali hii kwa mara ya kwanza baada ya miaka 70.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Kilimo na Chakula FAO sasa linaomba msaada wa kimataifa kukubaliana na uvamizi huu.
 
Mungu kawatuma nzige kuwaonyesha Cha mtema kuni Alshabab

Mashamba ya Alshabab yanaliwa na nzige usipime

Mimi nawaunga mkono nzige walioko Somalia.Hongereni kwa kazi nzuri ya kutafuna mashamba ya alshabab
 
Kama ndio uwezo wako wakufikiria hapa ndio umefikia mwisho pole sana ila kama unaendelea sawa.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu kawatuma nzige kuwaonyesha Cha mtema kuni Alshabab

Mashamba ya Alshabab yanaliwa na nzige usipime

Mimi nawaunga mkono nzige walioko Somalia.Hongereni kwa kazi nzuri ya kutafuna mashamba ya alshabab
Mbona ninaamini wewe ni mojawapo ya watu wenye akili hapa JF. Al-Shabaab ni mamia kama si maelfu wachache wakati Wasomalia ni mamilioni. Kwahiyo uwepo wa Panya Road unawafanya wakazi wa Dar kuwa wapuuzi na wahuni.
 
Back
Top Bottom