Nzige wakiwa ndani ya eneo la Kilometa ya mraba 1, wanakula chakula cha kuwatosha watu 35,000 kwa siku

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA, Bwana Mark Lowcock amesema “wimbi moja la nzige waliozingira ukubwa wa kilometa moja , ambalo linajumuisha nzige milioni 40-milioni 80, wanaweza kula kwa siku moja chakula ambacho kinatosheleza kulisha watu 35000”

Akitolea mfano uvamizi wa nzige hao Kaskazini Mashariki mwa Kenya amesema wimbi la nzige lilikadiriwa kuwa ni la ukubwa wa kilometa za mraba 2, 400 na nzige hao wanaweza kula chakula ambacho kinaweza kulisha watu milioni 84 kwa siku

Wimbi la nzige limevamia Pembe ya Afrika ambayo tayari ina changamoto zingine kama ukame, njaa Somalia na Sudan Kusini, mafuriko na machafuko yanayoendelea hivyo imekuwa janga baada ya janga

Na watu milioni 30 hawana uhakika wa chakula kwenye maeneo ambayo yamekumbwa na majanga hayo.

Pia amesema katika saa 24 zilizopita wimbi la nzige limevuka mpaka na kuingia Uganda. Ameongeza kuwa “Kama mjuavyo nzinge ni wadudu wa kale sana ambao uhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine na uvamizi wao unaweza kusambaratisha kabisa mazao na malisho haraka sana.”

Amesema “nzige hao sio tu kwamba wana njaa lakini wanasafiri haraka sana, nzige hao hawahusiki na masuala ya uhamiaji, au kuhitaji pasi za kusafiria na wala hawaheshimu mipaka ya kimataifa . Hili ni tatizo la kikanda na tayari tumepokea tarifa za uharibifu mkubwa wa mazao na mimea katika kanda hiyo.”

Chanzo: UN Swahili
 
Hatuwezi kuwapokea kama hawajapata namba za NIDA
 
... tulitakiwa tuwape support majirani ili waishie huko huko wasiingie nchini. Bahati mbayo ndio hivyo tena ni as if tunadhani tutawazuia wakati wa kuomba "visa".
Kweli bwana ilitakiwa tuwazuie wakiwa Ethiopia na sio kuwasubiria mpaka wameingia Kenya na sasa Kilimanjaro
 
Si mpaka kiwepo.
Umeeleewa vibay mkuu

Hapo ni kuwa hao wadudu wakienda kula majani wanakula jani lolote, Kiwango wanachokula ndicho kinachoweza kuwalisha watu hao,

Yaani kama wao nao wangekuwa selective, let say wanakula mchicha, mahindi, mpunga, mtama, uwele na ngano. Basi tungekufa mapema, ila wanakula jani lolote so inapunguza kasi yao kutudhuru japo utengenezaji/uharibifu wao uko palepale
 
Mpaka yawepo.

Tanzania hata majani yetu tuliyonayo hayawezi kulisha watu 35000 kwa eka licha ya mazao tunayokula. In fact hayawezi kulisha hata ng'ombe 1000 tu.

"Analysis" zingine hazina uhalisia.
 
Mpaka yawepo.

Tanzania hata majani yetu tuliyonayo hayawezi kulisha watu 35000 kwa eka licha ya mazao tunayokula. In fact hayawezi kulisha hata ng'ombe 1000 tu.

"Analysis" zingine hazina uhalisia.
Twende taratibu, nipe makadirio, Watu 35000 wanaweza tumia kiasi gani cha chakula kwa siku?
 
Twende taratibu, nipe makadirio, Watu 35000 wanaweza tumia kiasi gani cha chakula kwa siku?
Kila mtu mmoja kwa uchache nusu kilo kwa mlo mmoja (chakula na kitoweo) Milo mitatu kwa siku ni kilo moja na nusu Kwa mtu mmoja kwa uchache.

Kumbuka tu, kitoweo chenu Watanzania ndiyo chakula kwa nchi za Dunia ya Kwanza, na chakula chenu ndiyo kitoweo chao na "vice versa".
 
Sawa, twende na hiyo kilo na nusu, unadhani hawa wadudu wanaokula non-stop wanaweza kuipeleka kilo na nusu ndani ya muda gani wakiwa elf 50 tu.

Then weka kwenye km 1 ya mraba huwa wanakuwa milioni 40 hadi 80 wanaweza peleka kilo ngapi, je?
 
Sidhani kama wanamaanisha chakula kama chakula.
Nafikiri mazao wanayoharibu ndio yanaweza kulisha idadi hiyo ya watu yakikomaa na kuvunwa.
Maana panzi hula majani tu.
 
Kwenye huu uzi mi naona watu wengi wameshindwa kuelewa hili.."km 1² yanzige kula chakula cha watu 35,000 siku"

Nzige wanakula majani ya mimea hivo nzige kuharibu hecta moja ya mimea labda mahindi kwa siku moja ni rahisi tu, na kwa maana hiyo wanakuwa wameharibu chakula chote ambacho kingezalishwa ktk shamba hilo"

Na sio kwamba wingi wa chakula walacho watu 35,000 siku ni sawa na chakula walancho nzige walio kwenye km 1² siku.

Sent using Redmi Y2
 
Hapa ni hesabu tu, ngoja niangalie mnyukano,naona FaizaFoxy, anarudishwa Analogia, kwa wana Malenga
 
Kwenye huu uzi mi naona watu wengi wameshindwa kuelewa hili.."km 1² yanzige kula chakula cha watu 35,000 siku"

Nzige wanakula majani ya mimea hivo nzige kuharibu hecta moja ya mimea labda mahindi kwa siku moja ni rahisi tu, na kwa maana hiyo wanakuwa wameharibu chakula chote ambacho kingezalishwa ktk shamba hilo"

Na sio kwamba wingi wa chakula walacho watu 35,000 siku ni sawa na chakula walancho nzige walio kwenye km 1² siku.

Sent using Redmi Y2
Umeelewa vyema kabisa, wengine walidhani kwamba wanakula unga wao
 
Back
Top Bottom