Nzega makundi ndani ccm yammaliza dr. Kigwangala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nzega makundi ndani ccm yammaliza dr. Kigwangala

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ilulu, Oct 16, 2010.

 1. Ilulu

  Ilulu Senior Member

  #1
  Oct 16, 2010
  Joined: Mar 22, 2008
  Messages: 161
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimearifiwa kuwa hatimaye Mh. Sophia Simba aliwasili Nzega jana [16.10.2010] na Kufanya Mkutano wake katika Ukumbi wa Check Point.
  Mengi yalijitokeza lakini zifuatazo ndizo dondoo za Kikao hicho na mengineyo;
  · Kundi La Mhanga Hussein Bashe lilitawala Mkutano kwa kutoa dukuduku zao dhidi ya Mwenyekiti wao wa Chama Taifa [CCM] kwa kitendo chake cha kushindwa kuwasiliza au kuzungumza nao alipofika kwa Kampeni.
  · Walitama Mwenyekiti wao angefanya kama alivyofanya IRINGA kwa Mhanga Mwakalebela kwa kumkaribisha Bashe jukwaani.
  · Dr. Kigwangala akacha Mkutano huo wa jana na mmoja wa wajumbe alitoa taarifa ya kuwa yeye binafsi alimfuata na kumwomba ajumuike katika mkutano lakini hakufanya hivyo.
  · Makundi bado yatafunana, Kundi la Bashe, Selelii na la Dr. Kigwangala bado hayapikiki sahani moja
  · Alichofanikiwa ni kutoa tamko la kutomhamisha kiongozi mmoja aliyekusudiwa na moja ya makundi yaliyopo ang’olewe. Simba alisema hamwondowi.
  · Hadi kufikia ziara hii ya jana, tayari Jimbo la Nzega limetembelewa na viongozi wa Chama tawala lukuki kama vile Mwenyekiti Taifa ( mgombea Urais), Mkewe, Dr. Bilal, Beno Malisa, Makamba, Mwenyeki ti na katibu wa Mkoa ( kwa agizo la JK baada ya ziara yake) na hatimaye Mh. Simba na bado makundi yapo na kuendeleza uhasimu wao.
  Hata hivyo pamoja na ziara hii, kuna taarifa kuwa kuna jopo kubwa la watu au viongozi wa Serikali wanaopita mashuleni kuwaomba waalimu kumchagua JK na pia kujaribu kuwashawishi kuwa JK hana tatizo na Waalimu na hivyo wampe kura zao.
   
 2. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vipi kuhusu Chadema wanaeleweka au ndiyo nako bado?
   
Loading...