Nzega: Hubasha Ngasa ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kumbaka mjukuu wake mwenye miaka minne

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilayani Nzega mkoani Tabora, imemhukumu kifungo cha maisha Hubasha Ngasa (62) mkazi wa Kijiji cha Ngonho baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumbaka mjukuu wake mwenye umri wa miaka minne.

Awali Mwendesha Mashtaka wa Jeshi la Polisi, Melito Ukongoji, aliieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa la kumbaka mtoto huyo Aprili 24 mwaka 2016 baada ya kuachwa na wazazi wake walipokwenda shambani kulima.

Ukongoji alisema, “Baada ya muda wazazi wa mtoto huyo wakiwa shambani walisikia kelele za mtoto na walipokwenda kuangalia nini kimetokea, walikuta tayari mshtakiwa amembaka na kumjeruhi sehemu zake za siri.”

Akisoma hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Serafina Nsana, alisema adhabu hiyo imetolewa baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliowasilisishwa na upande wa mashtaka.
 
Aiseh! 62yrs! Any way atleast ameiona dunia may be hatokuwa na machungu! Ila namwonea huruma mtoto coz anahitaji effective psychology canceling!
 
Kwenye kesi za aina hii (Mzee miaka 62) nafikiri ingekuwa vyema pia mtuhumiwa kupimwa akili kabla ya kupewa hukumu. Inawezekana kabisa jela zikajaa vichaa zaidi ya Watukutu.
 
Hivi mtu anayetumia cheti kisichokuwa chake anaweza kuhukumiwa kwenda jela miaka kama mingapi hivi?
 
Back
Top Bottom