Utunzaji wa nywele za asili

Wana Bodi ya Urembo na mitindo
nina nywele Kipilikipili nimetumia mafuta aina ya Oliver oil bila mafanikio.
yaan unachana baada ya masaa mawili zinarudi kuwa Kipilikipili na hazijajaa vizuri nitumie mafuta gani. please wenye uelewa watusaidie najua tupo wengi
wenye shida hiyo.
Kwanini usitafute mafuta ya kukiboresha kipilipili chako mkuu na sio kukibadili
 
Wana Bodi ya Urembo na mitindo
nina nywele Kipilikipili nimetumia mafuta aina ya Oliver oil bila mafanikio.
yaan unachana baada ya masaa mawili zinarudi kuwa Kipilikipili na hazijajaa vizuri nitumie mafuta gani. please wenye uelewa watusaidie najua tupo wengi
wenye shida hiyo.
Baada ya masaa mawili zinarudi kuwa kipilipili? Kwa hayo masaa mawili zinakuwa sio kipilipili?

Jikubali kuwa una kipilipili au zibadili ziwe straight hakuna janjajanja!
 
Baada ya masaa mawili zinarudi kuwa kipilipili? Kwa hayo masaa mawili zinakuwa sio kipilipili?

Jikubali kuwa una kipilipili au zibadili ziwe straight hakuna janjajanja!
Hapo alimaanisha akizichana zinanyooka ila baada ya masaa mawili zinarudi kujiviringisha tena,

Ndio tabia kuu ya nywele za kipilipili hata kuzichana kwake wengi mpk atie maji kichwani bila hivyo akichana ni kama vile anaondoka na kichwa.
 
Wana Bodi ya Urembo na mitindo
nina nywele Kipilikipili nimetumia mafuta aina ya Oliver oil bila mafanikio.
yaan unachana baada ya masaa mawili zinarudi kuwa Kipilikipili na hazijajaa vizuri nitumie mafuta gani. please wenye uelewa watusaidie najua tupo wengi
wenye shida hiyo.
Nyoa
 
Wana Bodi ya Urembo na mitindo
nina nywele Kipilikipili nimetumia mafuta aina ya Oliver oil bila mafanikio.
yaan unachana baada ya masaa mawili zinarudi kuwa Kipilikipili na hazijajaa vizuri nitumie mafuta gani. please wenye uelewa watusaidie najua tupo wengi
wenye shida hiyo.
Ni mafuta mazuri sana sana.... na bei yake pia ni nzuri sana.
 

Attachments

  • 7faa60830801551e107337c2fd6f0468.png
    7faa60830801551e107337c2fd6f0468.png
    58.7 KB · Views: 158
Dawa ya kipilipili ni conditioner ...kuna ile deep conditioning unapakaa unavaa kofia ya plastic then after 30mins unaosha..baada ya nywele kukauka kidogo imean ziwe na unyevu kwa mbali paka sasa leave in conditioner yako ambayo hii unakaa NATO tu kama mafuta yaani hata uwe na kipilipili vipi nywele inakua laini ..cha muhimu tu ni consistency yaani kama unafanya kula baada ya wiki basi iwe hivyo sio unafanya Leo afu unarudia tena baada ya mwezi hautapata matokeo mazuri ..product ambazo Mimi huwa kutumia ni aunt Jackie's (conditioners) na cantu(shampoo) ..
Thanks luvie.. Yaani kesho shopping. Weekend nafanya mambo na kipilipili changu
 
Mimi nina rules kadhaa nimejiwekea kwa nywele zangu natural na nimeona maendeleo kwa kweli...mwanzo ilikuwa zikirefuka tu nanyoa ili ziwe fupi iwe rahisi kuchana na kustyle...lakini nimejifunza cha kufanya ili nywele ziwe laini, zichanike vizuri na kunyooka

1. Fanya conditioning (tunaitaga steaming)
Nywele zinafubaa kwa kukosa matunzo jamani. Fanya deep conditioning kila wiki mara 1 na kila unapotaka kusuka fanya deep conditioning kabla. Deep conditioner zinauzwa madukani au unaweza kufanya ya asili kwa kutumia mix ya ndizi, parachichi, asali, yai na mafuta ya nazi.

Conditioner unakaa nayo dk 30 hadi 40 then unaosha.

2. Mafuta hayazipi nywele unyevu bali yanasaidia kuhifadhi unyevu. Kitu kinachofanya nywele zinakuwa ngumu na kupata tabu kuchanika na kunyooka ni kukosa unyevu.

Kosa tunalofanya wengi ni kudhani mafuta yatazipa nywele zetu unyevu. Unyevu unapatikana kwenye maji au kuna bidhaa zinauzwa zenye kutoa unyevu kwa nywele (Moisturizers au leave in conditioners)

Hivyo kama mzururaji juani kama mimi hakikisha kila asubuhi au jioni unanyunyizia nywele yako maji au unapaka moisturizer yako au leave in halafu unapaka mafuta ya chaguo lako kwa juu ili kuhifadhi unyevu. Achana na habari za nywele ukiweka maji zinanuka, ni myth tu labda ziwe chafu. Kama si mzururaji unaweza kufanya hivi kila baada ya siku 2 au 3...

3. Chana nywele kwa kuzigawa kwenye mafungu. Jamani mimi nilikuwa kinara wa kusema "nywele zangu hazichanikiii". Lakini tatizo lilikuwa ni kulazimisha kuzichana tu randomly mara chana imeingia hapa imetokea kule.

Gawa nywele zako hata sehemu zisizopungua 4 kisha kwa kila fungu paka leave in yako na mafuta yako, chana. Ukimaliza suka kisection chako au kibane kisivurugike hamia kwingine.

Maisha mepeeesiiiii

4. Usilale na nywele natural bila kuzisuka mabutu. Hutokufa, utaamka nazo lakini huo mfungano utakaokutana nao asubuhi utazichukia.

Zisuke mabutu nywele zako kabla hujalala hasa kwa wenye ndefu, atleast wenye fupi wanaweza kulala nazo hvohvo. Kisha jifunge kitambaa au vaa kofia.

5. Google jinsi ya kuzistyle nywele zako wewe mwenyewe. Jamani mimi naamini katika theory ya mkono mbaya. Kuna watu wana mikono mibaya kwa nywele, akikushikashika nywele zinadhoofu.

Minimize ishu za saluni, style nywele zako mwenyewe.

Na kuna styles nyingi nzuri sana kwa nywele za asili, Hebu cheki hizi hapa chini

View attachment 640374

View attachment 640375

View attachment 640918

NB:

Nimeona kuna mtu hapo juu anasema ukipaka leave in au products za Aunt Jackies nywele zako zinakuwa kama umeweka dawa; Sijui ana nywele aina gani ila kwa wenye kipilipili kile concord chenyewe naomba nipingane nae, ni nzuri, zinarahisisha uchanaji na nywele zinakuwa laini ila sio kama umeweka dawa; asije fanya watu mkawa na matarajio ya juu sana halafu mkaja kumuita muongo.

Natumia Leave In Conditioner yao inaitwa Quench, Kuna Leave-in detangler ya watoto inaitwa Knot having it(hii nilinunua tu kwa kupenda rangi ila kwakweli haina ulazima), natumia na detangler inaitwa Knot on My Watch na Defining Curl Custard yao ya Curl La La.

Hizi products ni NZURI SANA. Yani nywele unachana vizuri, ukitaka kufanya style zile za kusokota halafu unafumua zinabaki na mawimbi, ukitaka kupaka tu halafu unaacha nywele zinaonekana mawimbi yake ya asili, ni wewe tu na bei zake ni affordable sana 15000 tu.

Kwa mnaopenda kunyoosha nywele bila kutumia blow dryer angalieni video hiyo..



Wasalaam.

ubarikiwe, mpenzi. Thanks for sharing. Shule nzuri kwa sisi naturalista
 
Back
Top Bottom