Utunzaji wa nywele za asili

Mwinga

Member
Jul 28, 2011
15
6
Kwa wale ambao tuna nywele asilia a.k.a natural hair, tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo. Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia, karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu

Katika mada ya leo,nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi. Je,unazifahamu nywele zako vizuri? Una nywele za aina gani? Zina tabia gani? Zinataka nini?

1. Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda.
Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi. Mwingine oh.. nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwani…hazishikiki.Tatizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako. Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri hivyo jambo la msingi la kuzingatia katika nywele zako ni kujenga mahusiano mazuri tu na nywele zako ,zielewe, ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua.

2. Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe.
Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele. Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri. Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki( ‘friendly’) . Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi. Unapoziacha chafu, ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia, kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri.

3. Linda unyevu wa nywele zako
Kila mtu akisikia kiu hunywa maji. Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu. Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu. Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri, na zikikauka zinakua kavu sana. Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri, ukazi-’condition’. Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache, pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.

4. Zifahamu nywele zako
Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi. Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu. Unajuaje?

Chukua kikombe,kijaze maji safi.Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi.

Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi.

Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa. Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida .(Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka.

Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita.

Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya vuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana.

Mimi nina aina gani?..Nina nywele zinazonyonya unyevu haraka.

5. Mafuta ya Kupaka kichwani.
Ni ya muhimu mnoo!.Nimefanya utafiti wa kina nimeona mafuta ya nazi yanaweka afya nzuri kwa nywele aina nyingi hivyo na mimi nikaanza kuyatumia. Kwangu mimi,mafuta ya nazi ya kutengeneza mwenyewe yamenikubali sana. Japo huwa nanunua pia mafuta kama ya olive(extra virgin) na ya tea tree.

6. Kuzichambua vizuri kabla ya kuchana.
Uwe mkarimu na mwenye subira kwa nywele zako. Mimi zikijifunga huwa nazichambua kwa mikono taratibu wakati mwingine nazilowesha na maji kwa mbali halafu nachana kwa chanuo lenye mapana sio ambalo reli zake zimebanana. sio kitana. Chanuo kubwa(wide toothed comb).

7. Usizisumbue mara kwa mara na usuke mitindo ya kuzitunza zikue.
Kama unataka zikue haraka,usizisumbue sana.Unaweza ukasuka mitindo mizuri tu ukakaa nazo wiki nzima au kadri zitakavyodumu. Au upunguze kuzichana mara kwa mara lakini utafute siku kama wikiendi ukae uzichambue taratibu na vidole kuondoa mafundo.Kuchana mara kwa mara zinapukutika,zinaanguka. Zitakua lakini sio kwa kasi ya kama ukizisuka ukaziacha kwa muda.

8. Punguza matumizi ya vitu vya moto kwenye nywele zako kama pasi ya nywele na vingine vya hivyo.


Sababu hizi hupelekea nywele kukatika

Hilo ni tatizo linalowakumba, siyo kinamama pekee, pia wanaume. Hata bidhaa nyingi za vipodozi hazijaweza kuleta matokeo makubwa katika kukabiliana na hali hiyo.

Kulikoni nywele zinapotea?

Zipo sababu mbalimbali zinazochangia kupotea nywele nyingi vichwani.
Kupotea au kunyonyoka kwa nywele, kumekuwa kukielezwa na wataalamu wa viumbe, kwamba ni matokeo ya misukosuko inayovipata viumbe vyote. Sababu zinazotajwa zinajumuisha zifuatazo:-\

  • Kuwepo shida za kila mara, au za muda mfupi, lakini athari zake ni kubwa.
  • Magonjwa ya kisaikolojia ya muda mrefu.
  • Uvuta sigara.
  • Kinga ya mwili kuwa chini; magonjwa yatokanayo na virusi; mabadiliko ya homoni katika mwili; masuala yanayohusu mazingira; mabadiliko ya mzunguko wa damu katika kichwa;
  • Sababu nyingine kurithi, kuwekewa ganzi wakati wa matibabu, mlo usio sahihi; ujauzito na kunyonyesha; tabia mbaya; magonjwa ya kichwani.
  • Kukatika nywele na ujauzito
Kwanini nywele za wanawake walio wengi hukatika sana wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua? Ni tatizo linalomkumba takriban kila mjamzito.

Wakati wa ujauzito, inaelezwa kuwa virutubisho vya afya ya mwili huchukuliwa na mtoto na kumwachia mama kiasi kidogo. Ni hali inayomuachia mama huyo uchovu.

Lakini swali la kujiuliza ni, kwanini kukatika kwa nywele hukuishii kipindi cha mimba tu, bali inaendelea hata baada ya kuzaliwa mtoto?"

Mwili wa mama baada ya kuzaliwa mtoto, unafanya kazi ya uzalishaji maziwa. Ni hali inayompunguzia mama nguvu zake.

Kwa mantiki hiyo, wataalamu wa afya wanasema, mabadiliko makubwa ya homoni katika mwili wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua huchangia madhara kwa mama kupoteza nywele.

Sababu za wanawake kupoteza nywele nyingi, pia inaweza kusababishwa na mambo yafuatayo;-


  • Upungufu wa vitamini zaidi ya aina moja mwilini (Avitaminosis) kwa muda mrefu; Yafaa kupata hasa vitamin ‘E’ na ‘A’ wakati wa ujauzito, ili kuepuka nywele kukatika.
  • Hali mbaya ya hewa, kwa mfano joto lililopotiliza.
  • Kuwepo kemikali kali za rangi zilizoko chini ya nywele bandia za bei nafuu, vidonge vya mara kwa mara vya kemikali, matumizi ya vifaa vya kukausha nywele, bila ya kutumia vifaa vya kinga.
  • Mimba na mchakato wa kuzaliwa.
  • Pia, kupoteza nywele nyingi kunaelezwa kunachangiwa na matokeo ya matumizi ya muda mrefu ya dawa. Kwa mfano, dawa zinazosababisha kuchanganyikiwa au kupatwa ‘maruweruwe’ zijulikanazo kama ‘narcoleptics.’ Vitu vinavyozuia kukua na
    kugawanyika chembe baadhi ya aina za dawa zinazozuia kifafa na ukosefu mkubwa wa vitamini A.
    Urejeshaji nywele

Haijalishi umepoteza nywele nyingi kiasi gani, lakini ni muhimu kuanza mchakato wa tiba mara moja kwa kushauriana na daktari kupata suluhisho.Mchakato wa kurejesha nywele unahitaji muda wa kutosha, utaratibu na uvumilivu sahihi.Hivi sasa, njia za kurejesha nywele zilizopotea zinapatikana kupitia baadhi ya njia zifuatazo:
  • Ulaji wa baadhi ya vitamin.
  • Baadhi ya vifaa vya tiba vinavyoondoa madhara, tiba ya uso na ngozi.
  • Matumizi ya vipodozi maalum na dawa za tiba za kienyeji ambazo ni za nyumbani, ambazo hupikwa kulingana na mapishi ya wanafanilia wanaozifahamu kwa kina.
Aidha, baada ya upotevu wa nywele, inaelezwa ni muhimu kuanza mara moja kuchukua hatua zinazozingatia mambo kadhaa:
  • Kuboresha lishe ya vifuko vinavyoshikilia mizizi ya nywele na kimetaboliki kwa jumla.
  • Kuboresha mzunguko wa damu kwenye mishipa midogo ya damu katika nywele.
  • Kuondoa ukavu kichwani.
Kumbuka kwamba, kupoteza nywele kwenye sehemu za mwili hutokea kwa muda fulani.
Hiyo, imekuwa ikimaanisha kwamba; kwanza unahitajika utunzaji viungo vyote vya mwili kwa ujumla.
Pili, ili kurejesha hali ya zamani ya nywele na itachukua muda, wakati mwingine zaidi ya vile tunavyodhania. Lakini, kwa njia ya kawaida, japokuwa ni ngumu bado inawezekana kurejesha nywele zilizopotea.

Wanawake wengi wanaona jinsi nywele zao zinavyokatika kwa wingi, bila ya kujali baadaye itakuwaje kimwili na kihisiaNywele zinazopotea. Ikiwa kila siku mtu anapoteza nywele kati ya 50 na 150 kulingana na ulaini wa kichwa, ikiwa ni jambo la kawaida.

Kumbuka kwamba, mifuko midogo inayoshikilia nywele kichwani, hubadilika kila mara na hawezi kabisa kuzuia upoteaji wa nywele.

Inashauriwa kwamba, iwapo mtu anaona nywele zake zinapotea sana, ni muhimu akawa na wasiwasi juu ya dalili za kuwepo walakini wa afya yake.

Unajuaje nywele zinapungua?

Wanawake wengi wenye nywele ndefu wanaweza kugundua uzito wa jumla umeshuka, ila wasijue kinachoendelea.

Lakini, ili kuwa na uhakika kabisa kwamba kichwa chako kimepungua nywele kwa uwiano, hesabu idadi ya nywele zilizoanguka wakati wa mchana.

Mtu akitaka kupata matokeo sahihi zaidi, inapendekezwa kwamba asikilize kichwa chake, kwa siku moja au mbili kabla ya jaribio.

Saa za asubuhi, mtu anaweza kuhesabu nywele zilizobaki juu ya mto baada ya kulala.

Kisha hatua inayofuata, ni kwamba mtu ananyunyiza nywele kwenye chombo kisafi na ahesabu wingi wa nywele fupi nene zinazobakia. Hapo ndipo, mtu anarekodi matokeo katika kidokezo maalum.

Nyakati za mchana, kila baada ya kuchana nywele, angalia nywele ngapi zinazopotea zaidi.

Mwishoni wa siku, mtu anatakiwa asafishe kichwa chako. Nywele zinazobaki bafuni au mikononi mwako, inapaswa pia kuhesabiwa. Huo ni mchakato mbadala.

Kwa njia hiyo, mtu anajua usahihi kabisa ni kiasi cha nywele anachopoteza kila siku.
Nywele na umri

Swali lingine ni je, uliwahi kujua kwamba, kulingana na umri, matatizo ya mabadiliko ya homoni na rangi ya nywele, kiwango cha kila siku cha kupoteza nywele kinaweza kutofautiana?

Kwa vijana, hadi asilimia 10 ya vifuko vinavyoshikilia nywele juu ya kichwa, hufa wakati wa kipindi cha kupevuka.

Kwa hiyo, swali la kuulizwa daktari, ni kwamba ikiwa nywele zimekatika kwa mtoto, inapaswa kuzingatia mazingira anayoishi na utendaji wa chembe ndani za mwili wake. Usiogope kabla ya wakati, ikiwa unapambana kukabili afya ya mtoto wako.

Wakati wa makuzi ya watoto (umri kati ya miaka mitatu hadi saba), balbu nyingi za nywele ziko katika awamu utendaji kazi.

Iwapo binti yako mwenye umri wa miaka 10 bado ana upotevu mkubwa wa nywele, hiyo ni nafasi ya kufanya miadi na daktari bingwa wa eneo hilo (dermatologist) kwa ajili ya kusaidia kuondokana na tatizo hilo.

Ikumbukwe, mpito wa umri wakati wa marekebisho ya homoni, huongeza tena kiwango cha wastani cha kupoteza nywele.

Nywele na rangi
Kulingana na rangi ya asili, kila mwanamke anapoteza nywele kwa kiasi tofauti kila siku. Kwa mfano, nywele rangi ya asili zina balbu zaidi juu ya vichwa vyao - hadi 150,000.

Nywele zao ni nyembamba za kutosha nyeusi na zenye uzuri zaidi kuliko zinazojulikana kama ‘braunettes’ au rangi nyekundu.

Kiwango cha upotezaji ya wenye nywele za asili, ni kati ya nywele 100 hadi 150 kwa siku. Nywele nyekundu pia zinamilikiwa na wanawake vijana wenye rangi nyekundu-‘maji ya kunde.’
Kichwani kwa mnyama mwenye kichwa chekundu, kuna

Vifuko vinavyoshikilia nywele (follicles) 80,000. Kwa hiyo, kiwango cha kupoteza manyoya kwao hutofautiana kutoka nywele 70 hadi 90 kila siku.

Kiwango cha hasara ya kila siku kinawekwa kwenye nywele karibu 80 hadi 110.
Ushauri

Nywele zikibaki katika hali ya asili kupumua, ni bora kwa ngozi. Kwa sababu hiyo, ukitaka uwe salama, ni muhimu kuepuka mitindo ya nywele iliyokaza sana.

Mambo kadhaa muhimu katika usalama wa chakula:
Chakula kisicho sahihi. Kwa kazi ya kawaida, balbu juu ya kichwa zinahitaji nguvu si tu kutoka nje, pia ndani.

Kwa hiyo, wanawake waliozoea mlo usio na lishe nzuri, mara nyingi wanakabiliwa na tatizo la kupoteza nywele, tofauti na wale wanaokula chakula bora.

Isisahaulike kwamba, kuimarisha mlo kwa mboga, matunda na multivitamini.






1580386246703.png


Namna ya kujaza nywele kwa njia za asili

Hilo linawezekana kwa kufanya yafuatayo.
  1. Chukua parachichi kubwa moja, asali vijiko vitatu na kiini cha yai.
  2. Osha nywele zako kwa shampoo na uzikaushe.
  3. Ponda ponda parachichi mpaka lilainike kabisa. Chukua vijiko vitatu vya asali na kiini cha yai kisha changanya yote kwa pamoja.
  4. Paka mchanganyiko huo kaa nao kwa muda wa dakika 15 kisha osha.
  5. Fanya hivyo kwa muda wa wiki moja hadi mbili na utaweza kuona matokeo mazuri katika nywele yako.


Chanzo: muungwana

Njia za asili za kuandaa chakula cha nywele

Tumia Asali katika Urembo wa Nywele na Ngozi yako

Asali hutumika kulainisha Ngozi
Asali ina asili ya kuvuta unyevu kutoka kwenye hewa na kuipa ngozi uwezo wa kuhifadhi unyevu hivyo ni faida kwa mtu mwenye ngozi kavu.

Jinsi ya kuandaa
Chukua asali mbichi kijiko kimoja cha chai kisha paka usoni, kaa nayo kwa dakika 15 hadi 20 kisha safisha uso wako.
Asali katika kusafisha ngozi, kutibu na kuzuia chunusi

Kutokana na uwezo wa asali katika kuua bacteria na kuvuta uchafu katika matundu ya ngozi asali itakusaidia kutatua tatizo la chunusi.

Jinsi ya Kuandaa
Chukua asali mbichi Kijiko kimoja cha chakula changanya na mafuta ya nazi vijiko viwili changanya mchanganyiko uwe mlaini kisha paka usoni huku ukisugua taratibu kwa kufanya kama viduara huku ukiepuka kufikisha machoni. ukimaliza kusugua uso na mchanganyiko wako osha uso wako.

Jinsi ya kuandaa kama kisafisha ngozi, exfoliator

Changanya kijiko kimoja asali na kijiko kimoja baking soda. tumia mchanganyiko huu kusugua ngozi yako. Asali inaongeza lishe na chembe chembe kuzuia madhara yanayotokana na sumu za hewani zinazozeesha ngozi. Baking soda inasaidia kusafisha matundu ya ngozi.
Asali inasaidia ngozi iliyoungua na jua kujirudi na kung'aa.

Jinsi ya kutumia asali katika nywele
Asali inatibu nywele kavu zilizopauka, na kulainisha ngozi kavu ya kichwa na kutibu muwasho kichwani.

Jinsi ya kufanya
Changanya kijiko kikubwa cha asali na maji ya uvuguvugu kisha paka kichwani Acha kwa muda wa saa 1 iwe kama conditioner kisha safisha nywele zako.

Unaweza kuchanganya asali kiasi cha kijiko kimoja mpk viwili katika maji vikombe vitano kisha safishia nywele zako taratibu, yaani yapitishe tu hayo maji kwenye nywele zako ambazo ni safi.

Tahadhari: Asali kwa kiasi kikubwa hupausha weusi wa nywele kutokana na Hydrogen Peroxide inayopatikana ndani ya asali.

Ni vema ukatumia asali mbichi kujihakikishia faida za asali katika mwili wako.

Iwapo unavutiwa na matumizi ya kitu cha asili katika urembo wako unaweza kuongeza kitu hicho katika kitu kingine unachotumia mfano katika steaming yako au scrub unayotumia.

JINSI YA KUTENGENEZA SHAMPOO YA KUKUZA NYWELE HARAKA NA KUFANYA ZIWE NA AFYA.

vifuatavyo ni vitu vya asili ambavyo utachanganya vyote kupata shampoo yako.

1. ALOVELA GEL
Chukua ute WA alovera vijiko kadhaa weka kwenye chupa yako. Tikisa vizuri
Alovera inatabia ya kuifanya nywele ikue haraka, iwe yeñye afya, inaondoa mba na muonekano WA asili zaidi.

2. ASALI
Inatabia ya kupambana na bacteria na fangasi wanakua kwenye nywele hivyo kuondoa miwasho kwenye nywele, inasaidia nywele zilizokatika zijae vizuri na kukua Kwa haraka. Lakini pia inasaidia nywele kua na harufu nzuri na kua laini ya kupendeza.
Ongeza vijiko kadhaa kwenye mchanganyiko wako WA alovera

3. MAFUTA YA MNYONYO( CUSTOR OIL)
Ni moja ya mafuta mazuri Sana Kwa nywele , yanafanya nywele kua nzito, kukua haraka na kusaidia nywele iliyonyonyoka.
Pia ongeza vijiko kathaa vya mnyonyo kwenye mchanganyiko wako na tikisa vizuri

4. NDIMU
Ukitaka nywele yako ing'ae Kwa mda mfupi na kukua haraka basi kwenye shampoo yako isikose ndimu. Tumia ndimu mbili kubwa kuongeza kwenye mchanganyiko wako WA shampoo na uanze kuona matokeo kuanzia week mbili.

5.MAJI YA UA ROSE
Haya yataifanya nywele yako inukie vizuri, lakini pia inasaidia kupambana na mba. Hufanya maotea ya nywele kukua vizuri na kua na nguvu. Ongeza vijiko vichache kwenye mchanganyiko wako.

KUMBUKA
sio lazima kua na vitu vyote hivyo Kwa wakati mmoja. Vichache utakavyopata vinatosha kutengeneza shampoo(sabuni ya nywele)
 
Nenda pale sh amon ... posta kuna dawa inaitwa kaminomoto ipo kwenye chupa ya kioo ndefu kidogo
Siyo ya china ila ni nzuri san but bit expensive
 
Msaada jaman nahitaji dawa ya kurefusha nywele. Napenda sana kuwa na nywele ndefu. Je kuna dawa ya mchina kwa ajili ya kurefusha nywele?

Kwa hiyo unataka dawa ya mchina tu? Ngoja unyonyoke nywele zote baada ya kutumia hizo dawa ndo utaiona raha ya mchina.
 
Nywele!!!!!!!!!!!!!! hizi nnazozijua mm??!!!! suka mabutu punguza blich na kubandika les weg!
 
Dawa inategemea na aina ya nywele zako. Tafuta washauri waangalie nywele zako ndio wakushauri.

Lakini kusuka ni dawa rahisi ya kunarefusha nywele.
 
Unajua mmea wa ALOVERA???? Kata kama majani yake mawili au matatu - saga kwenye blennder - halafu osha nywele zako ziwe safi - paka maji maji ya alovera ulioysaga - vaa cap yako na funga towel juu yake. - Stay for half an hour - Halafu osha vizuri. Paka mafuta unayotumia kwenye ngozi na suka - rudia tena kila mara unapofumua nywele zako.

Ukifanya hivyo frequently - nywele zako zitakuwa, zitakuwa strong.
 
Ukuaji wa nywele ni issue ya cell division (haina tofauti na ukuaji wa nwili). Na inahusisha viasili/genes. Kuna chemicals zinatumika kulazimisha cell division, lakini long term effects kansa ni mojawapo (abnormal cell division).otherwise nywele ni majaaliwa,wasaidie wanao kwa kuolewa na mwanaume ambao dada zake wana nywele,lol
 
nenda pale sh amon ... posta kuna dawa inaitwa kaminomoto ipo kwenye chupa ya kioo ndefu kidogo
siyo ya china ila ni nzuri san but bit expensive

SH Amon??? Niliwahi kwenda nikawekwa kwenye mashine kuangalia aina ya nywele zangu nikapewa mafuta, madawa ya kutumia kwa gharama kubwa sana lakini hakukuwa na mabadiliko yoyte usiende kabisa hapo
 
sha mon ni mazushi dadangu watakulia pesa tu rafiki yangu suka sana nywele ambazo sio ndogondogo tumia steaming nzuri na dawa nzuri pia lakin inategemea na asili ya nywele zako
 
Mwambie hazbendi wako awe anakuvuta manywele sana wakati wa kiduku cha usiku, wiki 2 tu utakuwa kuliko marehem bob male.
(haijasibitishwa rasmi, fanya utuletee ushuhuda)
 
Asante kwa ushauri wenu nitafanyia kazi. Na kuwapa matokeo ni njia ipi ilonisaidia.
 
SH Amon zamani ndio walikua na vitu vizuri sikuizi madudu matupu mie nakupitia mbali nakuona kama kituo cha polisi...
 
Dawa zingine zinataka moyo:

[h=2]Excrement[/h] A number of hair loss treatments over the years have included the use of animal excrement. The Legends of America website notes that people were once told to smear their heads with fresh cow manure to treat baldness or thinning hair. Helium.com notes that the Vikings had a prescription for baldness that called for rubbing goose droppings into the scalp.

It reports ancient Egyptians had a hair treatment that used a mix of honey, beer, boiled wheat and goat dung. The website reports that goat dung was added to the mixture in an effort to fool the gods into believing you were a goat to save your hair.


Read more: Old Time Hair Growth Remedies | LIVESTRONG.COM
 
Pamoja na yote lazima upate lishe bora, ikiwa na matunda ya kutosha, kunywa maji mengi na fanya mazoezi, hakuna shortcut bali mjumuiko wa mambo mengi utasaidia kuwa na nywele bora. Epuka madawa makali make ukiyaacha tu, utaona mvi nyingi kichwani mwako. Baada ya hapo unakuwa mtumwa wa hayo madawa, huwezi kuyaacha tena.
 
Back
Top Bottom