Nywele za kipilipili tukutane hapa tushauriane


Miss Natafuta

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Messages
21,708
Likes
36,025
Points
280
Miss Natafuta

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2015
21,708 36,025 280
Nywele natural ila kipilipili cha hatare nataka zinyooke ukiweka dawa zitaota tena?


Mimi nina rules kadhaa nimejiwekea kwa nywele zangu natural na nimeona maendeleo kwa kweli...mwanzo ilikuwa zikirefuka tu nanyoa ili ziwe fupi iwe rahisi kuchana na kustyle...lakini nimejifunza cha kufanya ili nywele ziwe laini, zichanike vizuri na kunyooka

1. Fanya conditioning (tunaitaga steaming)
Nywele zinafubaa kwa kukosa matunzo jamani. Fanya deep conditioning kila wiki mara 1 na kila unapotaka kusuka fanya deep conditioning kabla. Deep conditioner zinauzwa madukani au unaweza kufanya ya asili kwa kutumia mix ya ndizi, parachichi, asali, yai na mafuta ya nazi.

Conditioner unakaa nayo dk 30 hadi 40 then unaosha.

2. Mafuta hayazipi nywele unyevu bali yanasaidia kuhifadhi unyevu. Kitu kinachofanya nywele zinakuwa ngumu na kupata tabu kuchanika na kunyooka ni kukosa unyevu.

Kosa tunalofanya wengi ni kudhani mafuta yatazipa nywele zetu unyevu. Unyevu unapatikana kwenye maji au kuna bidhaa zinauzwa zenye kutoa unyevu kwa nywele (Moisturizers au leave in conditioners)

Hivyo kama mzururaji juani kama mimi hakikisha kila asubuhi au jioni unanyunyizia nywele yako maji au unapaka moisturizer yako au leave in halafu unapaka mafuta ya chaguo lako kwa juu ili kuhifadhi unyevu. Achana na habari za nywele ukiweka maji zinanuka, ni myth tu labda ziwe chafu. Kama si mzururaji unaweza kufanya hivi kila baada ya siku 2 au 3...

3. Chana nywele kwa kuzigawa kwenye mafungu. Jamani mimi nilikuwa kinara wa kusema "nywele zangu hazichanikiii". Lakini tatizo lilikuwa ni kulazimisha kuzichana tu randomly mara chana imeingia hapa imetokea kule.

Gawa nywele zako hata sehemu zisizopungua 4 kisha kwa kila fungu paka leave in yako na mafuta yako, chana. Ukimaliza suka kisection chako au kibane kisivurugike hamia kwingine.

Maisha mepeeesiiiii

4. Usilale na nywele natural bila kuzisuka mabutu. Hutokufa, utaamka nazo lakini huo mfungano utakaokutana nao asubuhi utazichukia.

Zisuke mabutu nywele zako kabla hujalala hasa kwa wenye ndefu, atleast wenye fupi wanaweza kulala nazo hvohvo. Kisha jifunge kitambaa au vaa kofia.

5. Google jinsi ya kuzistyle nywele zako wewe mwenyewe. Jamani mimi naamini katika theory ya mkono mbaya. Kuna watu wana mikono mibaya kwa nywele, akikushikashika nywele zinadhoofu.

Minimize ishu za saluni, style nywele zako mwenyewe.

Na kuna styles nyingi nzuri sana kwa nywele za asili, Hebu cheki hizi hapa chini

View attachment 640374

View attachment 640375

View attachment 640918

NB:

Nimeona kuna mtu hapo juu anasema ukipaka leave in au products za Aunt Jackies nywele zako zinakuwa kama umeweka dawa; Sijui ana nywele aina gani ila kwa wenye kipilipili kile concord chenyewe naomba nipingane nae, ni nzuri, zinarahisisha uchanaji na nywele zinakuwa laini ila sio kama umeweka dawa; asije fanya watu mkawa na matarajio ya juu sana halafu mkaja kumuita muongo.

Natumia Leave In Conditioner yao inaitwa Quench, Kuna Leave-in detangler ya watoto inaitwa Knot having it(hii nilinunua tu kwa kupenda rangi ila kwakweli haina ulazima), natumia na detangler inaitwa Knot on My Watch na Defining Curl Custard yao ya Curl La La.

Hizi products ni NZURI SANA. Yani nywele unachana vizuri, ukitaka kufanya style zile za kusokota halafu unafumua zinabaki na mawimbi, ukitaka kupaka tu halafu unaacha nywele zinaonekana mawimbi yake ya asili, ni wewe tu na bei zake ni affordable sana 15000 tu.

Kwa mnaopenda kunyoosha nywele bila kutumia blow dryer angalieni video hiyo..


Wasalaam.
 
Senee

Senee

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2015
Messages
959
Likes
1,020
Points
180
Senee

Senee

JF-Expert Member
Joined Nov 16, 2015
959 1,020 180
My dear ukiweka dawa lazima new growth itokee, kwa hiyo itakulazimu uweke tena dawa

Ila kama hutaki nywele za dawa siku hizi kuna products nzuri za natural hair, try za cantu ila za auntie jackie naona zipo cheaper kidogo
 
Lissa lee

Lissa lee

Senior Member
Joined
Jul 18, 2017
Messages
184
Likes
203
Points
60
Lissa lee

Lissa lee

Senior Member
Joined Jul 18, 2017
184 203 60
nina nywele natural ila kipilipili cha hatare.nataka zinyooke .ukiweka dawa zitaota tena?
mmmh ucjaribu kuwekaa dawa,, utabaki kipara,, zangu nikiweka dawa zina katika zote nabaki na kipara,, weka steaming,, hina ya majani changanya na yai la kienyejii kwa mwezi mara mbili , paka kwenye mizizi ya nywele,, utanipa matokeo
 
mommythebest

mommythebest

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Messages
516
Likes
592
Points
180
mommythebest

mommythebest

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2015
516 592 180
My dear ukiweka dawa lazima new growth itokee, kwa hiyo itakulazimu uweke tena dawa

Ila kama hutaki nywele za dawa siku hizi kuna products nzuri za natural hair, try za cantu ila za auntie jackie naona zipo cheaper kidogo
Auntie Jackies ni bei poa ila nzuri sanaaaa... Tena ukiwa na seti nzima utapenda. Mii nina dry hair lakini with aunt Jackies zimekuwa laini hadi nazionea raha. Try that maa
 
mommythebest

mommythebest

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Messages
516
Likes
592
Points
180
mommythebest

mommythebest

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2015
516 592 180
Afu jaribu kufollow page za wale ma expert wa natural hair kule insta, wanatoaga ushauri na maelekezo mazuri. Wanasaidia sana... Kina Adel_naturals, naturalhairtz, mimis_hair na wengineu
 
Rahabu

Rahabu

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2014
Messages
5,505
Likes
2,624
Points
280
Rahabu

Rahabu

JF-Expert Member
Joined Jan 21, 2014
5,505 2,624 280
Maana ninakipilipili sio cha nchi hii ukichana mbele nyuma zimejirudi ukimaliza nyuma mbele zimevurugika nilijaribu kueka dawa zinakatika nikisuka rasta za aina yeyote baada ya mtindo labda ninyoe nianze upya maana zinazunguka kukatika mateso ya nini nimejiekea dread hapa aaaaaa nakula bata tuu
 
Mr Miller

Mr Miller

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Messages
10,482
Likes
22,786
Points
280
Mr Miller

Mr Miller

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2017
10,482 22,786 280
Maana ninakipilipili sio cha nchi hii ukichana mbele nyuma zimejirudi ukimaliza nyuma mbele zimevurugika nilijaribu kueka dawa zinakatika nikisuka rasta za aina yeyote baada ya mtindo labda ninyoe nianze upya maana zinazunguka kukatika mateso ya nini nimejiekea dread hapa aaaaaa nakula bata tuu
Mimi kipilipili changu ni dread toshaa, naziosha na kuzipaka mafuta basi nasepa zangu....watu wanauliza dread nimetengenezea wapi kumbe ni asili tu, kipilipili cha kisomali
 
I

ivanaGIZ

Senior Member
Joined
Aug 18, 2017
Messages
102
Likes
34
Points
45
I

ivanaGIZ

Senior Member
Joined Aug 18, 2017
102 34 45
Ntapataje hayo mafuta ya aunt Jackie msaada plz
 
kenzi

kenzi

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Messages
377
Likes
366
Points
80
kenzi

kenzi

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2015
377 366 80
Ntapataje hayo mafuta ya aunt Jackie msaada plz
Sio mafuta. Inaitwa leave in conditioner ambayo jackies ni kampuni. kuna leave in conditioner nyingi za kampuni tofauti.

Kupata hiyo jackies nenda mwenge ulizia leave in conditioner ya jackies au kama hamna ulizia ya mega growth ni nzur pia.

Usiulizie mafuta ulizia leave in conditioner
 
Spalulu

Spalulu

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Messages
292
Likes
121
Points
60
Age
35
Spalulu

Spalulu

JF-Expert Member
Joined May 5, 2013
292 121 60
Mi nnachojua ni kwamba aunt Jackie ana products nyingi, so mnatushauri tuchukue zote au hiyo conditioner pekee?
 
kenzi

kenzi

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Messages
377
Likes
366
Points
80
kenzi

kenzi

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2015
377 366 80
Mi nnachojua ni kwamba aunt Jackie ana products nyingi, so mnatushauri tuchukue zote au hiyo conditioner pekee?
Unaweza chukua zote. But kama ni kuhusu kuchana nywele kwasbb ya kipilipili bas chukua leave in conditioner peke ake. unaweza ukachanganyia na product nyingne za shampoo au mafuta.

Pia kwa matokeo mazur ununue na shea butter ya nywele. Ni mafuta mazito kwa ajili ya nywele unapaka kwenye nywele yanasaidia nywele ambazo ni kavu zikae na mafuta mda mrefu.

Ukipaka leave in unachana unakuja unapaka shea butter ndo yanakuwa mafuta yako ya nywele lakini pia hata mwilini yanatumika. Ni mafuta mazur sana
 

Forum statistics

Threads 1,250,502
Members 481,371
Posts 29,735,823