Nyumbu amshambulia mzungu kwenye baiskeli na kumgalagaza

Askari Kanzu

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,598
1,233

Wakati mwendesha baiskeli yuko bize kwenye mashindano ya kuendesha baiskeli mwituni, nyumbu mmoja alitokea kusikojulikana na kumpiga daflao la nguvu na kumwangusha kisha kumgalagaza chali mwendeshaji huyo pamoja na baiskeli yake. Jamaa ana bahati aliponea chupu chupu sababu alikuwa amevaa helmet (kofia ya chuma).

Tukio hilo limetokea jana huko uswazi (South Africa).
 
Last edited by a moderator:
Niliona hii jana, jamaa ana bahati sana maana angeweza kujeruhiwa sana au hata kufa kama ile ndoo ya Nyumbu ingempata kisawasawa.
 
Niliona hii jana, jamaa ana bahati sana maana angeweza kujeruhiwa sana au hata kufa kama ile ndoo ya Nyumbu ingempata kisawasawa.
Ni kweli aisee, waswahili wanasema jamaa ana kismati! Nadhani pia kuna wajanja wataitumia hiyo clip kutengeneza matangazo ya kupromoti helmet!
 
haya nimesha wasoma, hapa hoja iko wapi? au tunajaribu kukumbushia umuhimu wa helment kwa wapanda pikipiki?
 
haya nimesha wasoma, hapa hoja iko wapi? au tunajaribu kukumbushia umuhimu wa helment kwa wapanda pikipiki?
Haswa, nadhani kuna huo umuhimu. Hata kanali Gaddafi (huyo kwenye hiyo avatar yako) hivi sasa inabidi abadili kibaragashia na kutumia kofia ya chuma manaake jamaa wanamuwinda na risasi za moto, teh teh teh!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom