VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Jana jioni,nilimtembelea Jaji Gabriel Rwakibalira,aliyemvua ubunge Godbless Lema, nyumbani kwake Kimara.Ni kweli amepooza kwa kiasi fulani.Si yule. Kwa ufupi mazungumzo yetu yalikuwa hivi:
Yeye(akinyanyuliwa ili akae kwa mazungumzo): Karibu Wakili!
Mimi: Asante Mh.Jaji,Shikamoo!
Yeye: Marhaba! Haya lete habari...hawajambo nyumbani kwako?
Mimi: Hawajambo Mh. Jaji,wanakusalimu wote. Pole kwa matatizo yanayokukabili
Yeye(akilengwalengwa na machozi) : Asante Wakili. Namshukuru Mungu kwa kila jambo
Mimi(nikamdokeza kinachoendelea kuhusu rufaa ya Lema halafu...) : Unaionaje?
Yeye: Anaweza kushinda.Yawezekana nilifanya makosa. Lakini,kwenye ujaji hakuna ukamilifu...hakuna kabisa
Mimi : Ni kweli. Mh. Jaji, matibabu yanaendeleaje lakini? (kwakuwa bado hatembei-amepooza kiasi fulani)
Yeye : Nilikwenda India,halafu nikarudishwa nchini.Naendelea vyema kwasasa. Lakini,kazini siendi. Unadhani nitaweza kwa hali hii kweli?(Akacheka)
Mimi: Hapana Mh.Jaji.
Baada ya hapo tuliendelea na mazungumzo mengine ya kifamilia pamoja na ndugu,jamaa na marafiki waliojumuika nasi.