Nyumbani kwa JAJI Rwakibalira

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Jana jioni,nilimtembelea Jaji Gabriel Rwakibalira,aliyemvua ubunge Godbless Lema, nyumbani kwake Kimara.Ni kweli amepooza kwa kiasi fulani.Si yule. Kwa ufupi mazungumzo yetu yalikuwa hivi:

Yeye(akinyanyuliwa ili akae kwa mazungumzo): Karibu Wakili!

Mimi: Asante Mh.Jaji,Shikamoo!

Yeye: Marhaba! Haya lete habari...hawajambo nyumbani kwako?

Mimi: Hawajambo Mh. Jaji,wanakusalimu wote. Pole kwa matatizo yanayokukabili

Yeye(akilengwalengwa na machozi) : Asante Wakili. Namshukuru Mungu kwa kila jambo

Mimi(nikamdokeza kinachoendelea kuhusu rufaa ya Lema halafu...) : Unaionaje?

Yeye: Anaweza kushinda.Yawezekana nilifanya makosa. Lakini,kwenye ujaji hakuna ukamilifu...hakuna kabisa

Mimi : Ni kweli. Mh. Jaji, matibabu yanaendeleaje lakini? (kwakuwa bado hatembei-amepooza kiasi fulani)

Yeye : Nilikwenda India,halafu nikarudishwa nchini.Naendelea vyema kwasasa. Lakini,kazini siendi. Unadhani nitaweza kwa hali hii kweli?(Akacheka)

Mimi: Hapana Mh.Jaji.

Baada ya hapo tuliendelea na mazungumzo mengine ya kifamilia pamoja na ndugu,jamaa na marafiki waliojumuika nasi.
 
Duh wadau kumbe Mh.Jaji alipooza kweli mm nilijua uzushi wa kibongo aise inasikitisha sana lakini kila kitu kinatokea kwa sababu
 
[ QUOTE=Kichwani-Kichwa;5200020]Jana jioni,nilimtembelea Jaji Gabriel Rwakibalira,aliyemvua ubunge Godbless Lema, nyumbani kwake Kimara.Ni kweli amepooza kwa kiasi fulani.Si yule. Kwa ufupi mazungumzo yetu yalikuwa hivi:

Yeye(akinyanyuliwa ili akae kwa mazungumzo): Karibu Wakili!

Mimi: Asante Mh.Jaji,Shikamoo!

Yeye: Marhaba! Haya lete habari...hawajambo nyumbani kwako?

Mimi: Hawajambo Mh. Jaji,wanakusalimu wote. Pole kwa matatizo yanayokukabili

Yeye(akilengwalengwa na machozi) : Asante Wakili. Namshukuru Mungu kwa kila jambo

Mimi(nikamdokeza kinachoendelea kuhusu rufaa ya Lema halafu...) : Unaionaje?

Yeye: Anaweza kushinda.Yawezekana nilifanya makosa. Lakini,kwenye ujaji hakuna ukamilifu...hakuna kabisa

Mimi : Ni kweli. Mh. Jaji, matibabu yanaendeleaje lakini? (kwakuwa bado hatembei-amepooza kiasi fulani)

Yeye : Nilikwenda India,halafu nikarudishwa nchini.Naendelea vyema kwasasa. Lakini,kazini siendi. Unadhani nitaweza kwa hali hii kweli?(Akacheka)

Mimi: Hapana Mh.Jaji.

Baada ya hapo tuliendelea na mazungumzo mengine ya kifamilia pamoja na ndugu,jamaa na marafiki waliojumuika nasi.[/QUOTE]
#Mungu amponye sana mh jaji, ili kama alipata maagizo toka kwa mkubwa ktk kutoa hukumu abaki hivyo hivyo!
 
Very unprofessional journalism!! Ni aibu kuwa na mwandishi wa aina yako, sababu zangu ni hizi:

a) Kama unafahamiana nae na ulikwenda kumsabahi, ungeelewa maumivu yake na ukaishia hapo tu. Kama mgonjwa ana haki ya kutotaka kufahamika kwa hali ya ugonjwa wake!!
b) Kuzungumzia kesi ya Lema ambayo ni yeye aliamua ni kosa kimaadili tu, bali ni kumchokoza. Ulitaka maoni yake ili iwe nini? Hili si swala la maoni, ni swala la facts na sheria.

Lakini ungekuwa jasiri, usingemfuata mgonjwa. Hebu waliuze akina EL, EC, JK et al. kuhusu EPA, Radar tupate kusikia "maoni" yao.

Usipokaribishwa tena kwenye nyumba ya Jaji Rwakibarila, usiseme kakuonea au ni mtu mbaya. Watu wa aina yako ndio huitwa wazandiki!!!
 
Get well soon Hon. Judge ... Mungu anawapenda wanaokiri makosa....... huwasamehe.... na kuwafanya wale wanaopenda kufanya makosa ya MAKUSUDI kujifunza kwa wanaokiri makosa maana hawatafanya makosa tena ...............kwa kuwa wameona na kujifundisha kutoka kwa waliofanya makosa ya makusudi....... hukumu na kutoa haki na haki kuwa haki..ni thawabu kubwa kwa Mungu.......
 
Masikini pesa aliopewa kuhukumu bila haki itatosha kweli kumtibu?naamini malipo ni hapahapa duniani,MUNGU si kikwete,jaji tubu mbele ya umma kuwa ulifanya zambi utapokelewa mbinguni.
 
Mnh! ulienda kumtembelea kama "Wakili" au mwanafamilia? Ulienda kufanya mazungumzo na Jaji kuhusu kesi ya Lema au ulienda kusalimia mgonjwa? Ila vyovyote iwavyo huna ustaarabu hata kidogo!
 
Wewe si mtu makini, kama kweli ulienda kumjulia hali Jaji, kulikuwa na haja gani ya kuyaweka mazungumzo yenu hapa? Wewe ni msaliti kweli kweli.
Mkuu Mwitongo huyo Jaji ni mtu muhimu saana kwa kubadili mwelekeo wa siasa za Arusha, hivyo si vibaya tukajua baada ya hukumu aliyoitoa yeye ya kumvua ubungwe Mhe Lema yeye anaendeleaje???? Madarasa yako mengi tuu ingawa labda hutokubaliana na mimi!!!

Mhmm! Haya ndg zangu. Kunya anye kuku, akinya Batavia Maharishi. Mwenye thread hii kachemsha sanaaaaaaa
 
Wewe si mtu makini, kama kweli ulienda kumjulia hali Jaji, kulikuwa na haja gani ya kuyaweka mazungumzo yenu hapa? Wewe ni msaliti kweli kweli.

Ubaya uko wapi ametusaidia wana JF kujua kwamba kweli amepooza,make taarifa zilikuja hapa,watu wakasema kapooza wengine wakasema hapana ,kumbe kweli amepooza tumuombee apone na kesi ya Lema iwe fundisho kwake kutenda haki mbele za jamii na mbele za Mungu atapona ili aweze kugeuka nyuma na kusema sitakuwa mtumwa tena
 
Wewe si mtu makini, kama kweli ulienda kumjulia hali Jaji, kulikuwa na haja gani ya kuyaweka mazungumzo yenu hapa? Wewe ni msaliti kweli kweli.
Mbona unatokwa na povu lote hili la nini? Mbona wewe ndio Msaliti namba moja kwa Watanzania kwa kutumia kalamu ambayo ndio mtaji wako?
 
Very unprofessional journalism!! Ni aibu kuwa na mwandishi wa aina yako, sababu zangu ni hizi:

a) Kama unafahamiana nae na ulikwenda kumsabahi, ungeelewa maumivu yake na ukaishia hapo tu. Kama mgonjwa ana haki ya kutotaka kufahamika kwa hali ya ugonjwa wake!!
b) Kuzungumzia kesi ya Lema ambayo ni yeye aliamua ni kosa kimaadili tu, bali ni kumchokoza. Ulitaka maoni yake ili iwe nini? Hili si swala la maoni, ni swala la facts na sheria.

Lakini ungekuwa jasiri, usingemfuata mgonjwa. Hebu waliuze akina EL, EC, JK et al. kuhusu EPA, Radar tupate kusikia "maoni" yao.

Usipokaribishwa tena kwenye nyumba ya Jaji Rwakibarila, usiseme kakuonea au ni mtu mbaya. Watu wa aina yako ndio huitwa wazandiki!!!
mara ngapi tumeenda kwa ndugu na jamaa kufuatlia wagonjwa tukajikuta tunaongea mambo mbalimbali nadhani alifanya vizuri kutaka kujua kama anajua kinachoendelea si ni yeye alitoa hukumu kwani kuna ubaya gani mulitaka afanye siri wakati mambo yako hadharani,
 
Mnh! ulienda kumtembelea kama "Wakili" au mwanafamilia? Ulienda kufanya mazungumzo na Jaji kuhusu kesi ya Lema au ulienda kusalimia mgonjwa? Ila vyovyote iwavyo huna ustaarabu hata kidogo!
Angekosa ustaarabu kama angetueleza phyisical appearance ya judge yaani kama angesema alivaa nguo imechanika,uso umemshuka,ana aibu n.k lakini amejumuisha tuu hana kosa
 
Back
Top Bottom