BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,083
...bila kujali kama zimelipiwa au la, maana ziliuzwa katika mazingira ya kutatanisha
Posted Date::10/15/2007
Wasiolipia nyumba za serikali kunyanganywa
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi
SERIKALI imetangaza kuzirejesha nyumba zake zote, ambazo zitakuwa hazijalipiwa ndani ya kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa.
Nyumba hizo ni zile ambazo ziliuzwa kwa baadhi ya wafanyakazi chini ya serikali ya awamu ya tatu.
Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, alithibitishia jijini Dar es Salaam jana kuhusu mpango huo wa kutaka kuzirejesha nyumba ambazo hadi sasa hazijalipiwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA), kila aliyeuziwa nyumba anatakiwa kulipa fedha hizo au kumaliza deni lake.
Taarifa hiyo iliongeza kwamba, wote waliouziwa nyumba wamepewa wiki mbili kuhakikisha wanalipa fedha hizo.
"Fedha hizo zinapaswa kulipwa katika maeneo ambayo yametajwa, kupitia akaunti za benki".
Akizungumzia zaidi suala hilo, Chenge alisema pamoja na mpango mwingine wa serikali kuongeza ujenzoi wa nyumba zake, hizo ambazo ziliuzwa zitarejeshwa iwapo wahusika watashindwa kulipa na kisha kuuzwa kwa wafanyakazi wengine wenye uwezo.
Chenge alifafanua kwamba, kwa wale ambao pia watakuwa wameanza kulipa kidogo, serikali itataka kuona mipango yao ya kulipa ikoje kwa mujibu wa mikataba ili kama hatua zikichukuliwa zifanyike kwa mujibu wa makubaliano.
Alisema hatua zote zitachukuliwa kwa mujibu wa mikataba na kusisitikza kuwa wale ambao hawaanza kuliupa nyumba zitachukuliwa na kuwapa wengine wanaozihitaji wenye uwezo wa kulipa.
"Wapo ambao wanahitaji na wana uwezo wa kulipa, tunajua mishahar a yetu ni midogo, lakini tutaangalia zaidi mikataba inasemaje, ndipo tutachukua hatua," alisema Chenge.