Nyumba zote zilizouzwa zirudishwe serikalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba zote zilizouzwa zirudishwe serikalini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 12, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  Serikali yazirejesha nyumba 120 zilizouzwa

  2009-02-12 10:35:12
  Na Boniface Luhanga, Dodoma​

  Serikali imefuta miliki ya nyumba zake zaidi ya 120 ambazo waliuziwa watumishi wake, taasisi na watu binafsi.

  Kufuatia hatua hiyo, serikali sasa italazimika kuwalipa watu hao mamilioni ya fedha kama fidia kutokana na wamiliki hao wapya kuziendeleza huku wengine wakijengewa nyumba nyingine.

  Hayo yalitangazwa jana bungeni na Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa alipokuwa akiwasilisha taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya uuzwaji wa nyumba za serikali.

  Pamoja na mambo mengine, Bunge liliazimia na kuiagiza serikali kuzirejesha kwenye miliki yake nyumba zote zilizouzwa kinyume cha utaratibu.

  Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa azimio hilo, Dk. Kawambwa alisema serikali imekamilisha tathmini ya maendeleo yaliyofanywa katika nyumba zote na sasa mikataba imefutwa.

  Alifafanua kuwa, kwa nyumba zilizoko kwenye makambi kwa wanaoishi humo hadi sasa ni watumishi wa umma wenye stahili ya kupewa nyumba na serikali, wameandikiwa barua kuwajulisha kuendelea kuishi humo kama wapangaji kwa mujibu wa stahili zao za kiutumishi.

  Alisema pamoja na hayo, bado hatua za kuwarejeshea fedha zao zinaendelea.

  Waziri Kawambwa alizitaja nyumba hizo ambazo zimerejeshwa kwenye miliki ya serikali na wamiliki wake watalipwa fidia zao kuwa ni 53 zilizopo kwenye makambi ambazo hazikupaswa kuuzwa, nyumba 27 za taasisi mbalimbali zilizouzwa kwa watumishi wa serikali na nyumba 35 zilizouzwa ambazo zipo kwenye maeneo nyeti ya serikali.

  Pia alizitaja nyumba nyingine kuwa ni nyumba nne zilizouzwa kwa watu ambao si watumishi wa serikali na familia sita na watumishi wanne waliouziwa nyumba zaidi ya moja.

  Hata hivyo, alisema waliouziwa nyumba hizo, watalipwa fidia kutokana na kwamba walikuwa tayari wameziendeleza huku baadhi yao wakijengewa nyumba nyingine.

  Watu hao watalipwa fidia ya kati ya Sh. milioni 13 na Sh. milioni 223 kutegemeana na mhusika alivyokuwa ameifanyia ukarabati nyumba husika.

  Kuhusu utekelezaji wa maazimio juu ya mkataba wa Kampuni ya Kupakia na Kupakia Makontena (TICTS), Waziri Kawambwa alisema hatima ya kampuni hiyo sasa iko mikononi mwa Baraza la Mawaziri.

  Alisema wizara yake imeandaa Waraka kwa Baraza la Mawaziri ili kupata maamuzi ya juu ya serikali kuhusu suala hilo.

  Aidha, kuhusu suala la Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Dk. Kawambwa alisema serikali kwa sasa inapitia ripoti ya kikundi-kazi na kuona namna ya kuyafanyia kazi mapendekezo ya ripoti hiyo kwa lengo la kuimarisha shirika hilo.

  Kuhusu suala la Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) alisema serikali imeunda kamati ya majadiliano ya kurekebisha mikataba ya ukodishaji na wanahisa.

  Alisema kamati ya serikali imewasilisha mapendekezo mbalimbali ya kurejea vipengele mbalimbali katika mkataba wa ukodishaji.

  SOURCE: Nipashe
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  Waungwana, katika mkataba wa wale waliouziwa nyumba inasemekana kulikuwa na kipengele kinachosema wasizifanyie ukarabati nyumba walizouziwa kwa miaka kadhaa. Sasa kama walizifanyia ukarabati ambapo ni kinyume na makubaliano ya mkataba, kwanini tena serikali iwalipe!?
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tunaondoa bomu moja na kutengeneza matatu.....hii issue inaweza kuwa ni deal juu ya deal....watu hapa watalipwa kodi zetu bure kabisa.....! nani atafanya tathmini kujua thamani halisi ya ukarabati uliofanyika? na kama mikataba iliwataka wanunuzi wasifanye ukarabati, kwa nini kuhangaika kuwalipa hao jamaa?
   
 4. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Potelea mbali, si 120 tu bali zote zirudishwe. NT, wala hatutengenezi mambo matatu, yaani nyumba zote za serikali ziko kwenye prime areas, na walichofanya wakulu wa nchi si kutaka nyumba isipokuwa viwanja ambavyo vyote viko mahali pazuri sana. Hebu firikira kiwanja cha Oysterbay ambacho hakijajengwa kina thamani gani.

  Mimi sioni tatizo hata kama watawalipa basi wawalipe zile gharama halisi za ujenzi wa hizo nyumba zilizoendelezwa na si kwa bei ya viwanja.
   
 5. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama kweli nia kuzirudisha hizo nyumba na wako tayari hata kutoa fidia, kwanini wasiwaachie then wao wakajenge nyumba nyingine kwa kutumia hiyo hela ya fidia? Otherwise mimi naona ni mchezo mchafu tu.

  Am I missing something?
   
 6. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hizo 120 ni ulaji mwingine...fidia ya Mil 13 hadi 223 si ni bora wangejenga nyimba nyingine..!!! Hizi siasa za kutafuta umaarufu zinatugharimu sana.
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  You are really missing something! Where will you get beautiful plots like those in Oysterbay and other prime areas?

  It is true that these guys are going to make a hell of money. But if we had credible and clean people to handle the matter, the saving would justify the process! I can't imagine who will be doing it since most of the big guys are involved. Labda waamue kujilipua kama HAMAS!:confused:
   
 8. Mchola

  Mchola Member

  #8
  Feb 12, 2009
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu, hii nchi inaliwa na wenye meno!!! Kila opportunity inapotokea basi wanakula tu. Waliojiuzia nyumba kinyemela wangechukuliwa hatua kwanza si tu kurudisha then basi kimya!! Ufisadi hauwezi kumalizwa na mafisadi!! period.
  Watawala watambue kwamba hili suala la kujiuzia nyumba za serikali will haunt them for generations and generations!!!It was a wrong decision and they all know it. Hata mtoto mdogo anajua hili!!! Hii kuzirudisha baadhi ni kujikosha tu hamna lolote hapo!!!
   
 9. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  I'm still missing something. What makes an area prime? Typically it would be the accessibility of that area to other major services. For instance, areas close to towns, malls, beaches and so forth. Sasa, what I believe ni kwamba serikali kwa kutumia hizo hela za fidia, wanaweza kabisa kufanya eneo lolote lile kuwa prime. Hizi fedha ndio zitumike kule kwenye satelite cities. These areas will also be prime. Kwasasa hatuwezi kujustify kuwalipa watu fidia huku tukisisitiza kwamba serikali ina nia ya kumfanya kila mwananchi kuwa na makazi bora. Juzi tu kwenye speech ya mwisho wa mwezi, JK ameligusia hili na kuelezea mikakati ya serikali yake kuona hili linatimia. Sasa, sijui hapa tunaelekea wapi. Nyuma au mbele?
   
 10. J

  Jitume Senior Member

  #10
  Feb 12, 2009
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  -Serikali haina nia hata kidogo kutekeleza maagizo ya Bunge (Matakwa ya Wananchi)

  -Idadi ya nyumba zilizoainishwa hapo juu ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya nyumba zote zilizouzwa mikoa yote.

  - Idadi hiyo hapo juu ni ndogo sana hata kwa nyuma zilizoko DSM tu!

  - Iundwe upya kamati maalum kuorodhesha nyumba na kuzirejesha serikalini. wajumbe wa kamati wasiwe na maslahi kwenye jambo hili (Wasiwe wamojawapo wa waliouziwa)

  - Aliyeuziwa nyumba eneo (prime) km Msasani, Maeneo yajulikanayo kama Uzunguni km Arusha, Iringa, Morogoro kilimani, BKB Airport nk ni kwa vipi anaweza kupendekeza yeye mwenyewe nyumba yake irudishwe serikalini?

  -Yale yale ya uchunguzi wa kuwawajibisha Mwanyika na Hosea wakati bado wapo madarakani na ndio waratibu wa shughuri hiyo!!!!

  -Hizo nyumba zilizohamuliwa kurejeshwa zitajwe ili tuhoji kuhusu zilizoachwa

  Kwa mara nyingine, hapa serikali inafanya mchezo wa kuigiza.


   
 11. w

  wajinga Senior Member

  #11
  Feb 12, 2009
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa mbona nyingine tumeshauzia wahindi na maapatiment yameshajengwa bwana nyie mnatuharibia maslahi yetu. Kwa hiyo inabidi tuhonge tena tuanze upya tutalipa mpaka lini bana. Hii inakuwa kama madini nase kilakitu kitaanza upya mikataba upya maana hongo upya mambo hayabadiliki bali tumbo.
   
 12. Z

  Zungu Pule JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 2,139
  Likes Received: 682
  Trophy Points: 280
  Nope. TZS 223 Million haijafikia hata thamani ya kiwanja kilichoko O-Bay. And "accessibility" of an area has a little effect on the house price. Actually being close to towns lower the price of a house because normally that's a polluted area with a lot of noise. The environmental factors and the size of a house contribute significantly to the price of a house. Na mawazo kwamba, Serikali inaweza kutumia hizo pesa "to turn a new area into O-bay" ni ndoto kwa sababu hatuna watu serious wa kusimamia miradi ya namna hiyo. Angalia nyumba walizojenga Mbweni, angalia mafisadi walivyojenga Mbezi. No plan at all. Nyumba za Mbweni ni sub-standard kabisa. And that's enough for a government work! Bila wakoloni ninauhakika tusingekuwa na maeneo kama O.Bay. Prove me wrong!
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  Serikali yafuta mikataba ya nyumba zilizouzwa kinyume
  Stella Nyemenohi, Dodoma
  Daily News; Thursday,February 12, 2009 @20:05​

  Serikali imefuta mikataba ya nyumba zote za serikali zilizouzwa kinyume cha utaratibu. Kutokana na hatua hiyo, Sh trilioni 1.2 zinahitajika kwa ajili ya kuwafidia watumishi wa umma waliofutiwa mikataba yao kutokana na uendelezaji waliokuwa wameufanya katika nyumba hizo.

  Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa aliliambia Bunge juzi wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa azimio la Bunge kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali na kusema fedha hizo zitatengwa katika bajeti yake ya mwaka ujao.

  Katika taarifa hiyo yenye majina ya wahusika wote wa nyumba hizo, Dk. Kawambwa aliainisha makundi matano ya nyumba hizo zilizouzwa kinyume miongoni mwake, zikiwamo zilizouzwa kwa watu binafsi wasio watumishi wa umma baada ya wahusika kutoa taarifa zisizo sahihi.

  Kielelezo kilichoambatanishwa na taarifa hiyo, kimewataja wahusika kuwa ni pamoja na Esther Chilambo ambaye wakati wa ukaguzi, alikuwa mtumishi wa Mipango ingawa alipopewa mkataba alikuwa akifanya kazi Redio Tumaini.

  Hata hivyo, taarifa inaonyesha kwamba aliuziwa kama mstaafu kwa maagizo ya Serikali kumbukumbu Na. GC:210/228/012 dokezo namba 25. Wengine ni Mussa Joseph, Stanley Manongi (wote wamefungua kesi mahakamani kupinga kusitishiwa mikataba) na Monica Senga.

  Taarifa hiyo ambayo iliridhiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa asilimia 80, ilitaja makundi mengine ya mikataba iliyofutwa kuwa ni nyumba za familia sita na watumishi wanne waliouziwa nyumba zaidi ya moja. Kati ya hao, ulijitokeza utata kwa familia zilizokuwa zinamiliki nyumba Namba 36 Mtaa wa Ismailia, Dar es Salaam na nyumba Namba 516/18 ya Mtaa wa Mkadini, iliyoleta taarifa ya kuwa wametalikiana.

  Wahusika ni Ngore Kondo na Zainabu Kondo. Ufumbuzi wa suala hilo utapatikana baada ya kujiridhisha na vielelezo vilivyopo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kuhusu nyumba 27 za taasisi mbalimbali zilizouzwa kwa watumishi wa serikali kuu, miongoni mwa waliouziwa katika Mkoa wa Dar es Salaam ni pamoja na Jaji Stephen Ihema, Bakari Mwapachu, Balozi Adam Marwa na Kuboja NgÂ’ungu.

  Kundi jingine ni nyumba 35 zilizouzwa wakati ziko katika maeneo nyeti ya serikali. Akiwasilisha maoni ya kamati, Mbunge wa Kalambo, Ludovick Mwananzila (CCM), alishauri fedha zitakazotumika kulipa fidia zitokane na bajeti ya wizara kwa kuombwa kutoka serikalini.

  Vile vile kamati ilibaini kwamba zipo nyumba za serikali ambazo hazijakaratibiwa hususani mkoani na kuingizwa kwenye mchakato huo. Ilishauri Wizara na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) waendeleze utambuzi huo ili kupata uhakika wa umiliki wa nyumba zote zilizo chini ya serikali.

  Wakati huo huo, TBA imekusanya Sh 40,929,145,047.13 sawa na asilimia 71.7 57,057,965,241 ya fedha zinazotarajiwa kukusanywa kutokana na mauzo yote ya nyumba katika kipindi cha miaka 10.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  Kutokana na hiyo article hapo juu thamani ya nyumba zote zilizouwa ni shilingi 57,057,965,241. Na pesa zinazotakiwa kurudishwa kwa wale ambao hawakustahili kuuziwa nyumba kwa sababu moja au nyingine ni Sh trilioni 1.2. Nyumba hizo kama kumbukumbu yangu ni nzuri ziliuzwa mwaka 2004 au 2005 kabla Mkapa hajamaliza awamu yake.

  Hivi kweli waliozifanyia ukarabati hizo nyumba walitumia shilingi 1.2 Trilioni kuzifanyia matengenezo!!!? Ni watu wangapi ambao walizifanyia nyuma zao matengenezo? Je, serikali inaweza kuweka majina ya hao wote waliozifanyia nyumba walizouziwa matengezo na kiasi ambacho walichotumia ili tupate jumla ya shilingi 1.2 trilioni? Mimi naona hapa kuna wizi na ufisadi wa hali ya juu. Bila kutoa risiti za kuthibitisha kiasi walichotumia kufanya matengezo hayo basi wasirudishiwe hata senti tano. Kweli hawa watu wana pesa za kufanyia matengenezo nyumba zao kwa shilingi trilioni 1.2? Wamezitoa wapi pesa zote hizi? Wameajiriwa, wamejiajiri au ni mafisadi?

  Pia inasemekana kwamba mkataba ulisema kwamba wanunuzi wote wa nyumba wasizifanyie matengenezo yoyote nyumba zile, kama ni kweli basi hawastahili kurudishiwa hata senti tano maana wamekiuka mkataba.

  Kuna haya kubwa ya kuuweka mkataba wa uuzaji wa nyumba za serikali hapa jamvini ili tuuchambue kwa kina maana hapa naona kuna ufisadi mwingine ambao ni mkubwa zaidi ya EPA, Meremeta, Richmond, Rada unatengezwa ili kuchota shilingi Trilioni 1.2
   
  Last edited: Feb 13, 2009
 15. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145

  Greedy BAs^%*&s!!!
   
 16. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kampeni za 2010 wanaanza kuziona zinakuwa ngumu, maana utegemezi wa kuhonga ni mkubwa kuliko utegemezi wa sera na mafanikio waliyonayo... wameisoma jamii na kuona kuwa mianya mingi waliyotumia 2005 imeshitukiwa tayari au kuwa ni ya hatari mno, hivyo wameanza mikakati mingine ya kufanikisha ununuaji wa kura ifikapo 2010!
   
 17. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwanza tunaomba sana sana mkataba huo uwekwe hapa jamvini

  Maoni yangu ni kwamba lazima mkosaji aadhibike. vinginevyo maana halisi ya shria haitaheshimika.

  1. Walijiuzia nyumba zetu kihuni na kwa bei ya bwerere wanastahili adhabu ya mwizi. Pale Manzese tungewapiga mawe na kuwavisha tairi. Lakini hapa napendekeza adhabu ya kishkaji - WANYANG'ANYWE NYUMBA TU BASI.
   Wamekiuka mkataba kwa kuendeleza nyumba nje ya makubaliano. Hii ni dharau kwa sheria za nchi. WANYANG'ANYWE NYUMBA TU BASI.
   Wametumia vibaya madaraka yao. Hii ingewastahili kupelekwa mahakana na kukutwa nayaliyomkuta Mramba lakini wahukumiwe kishkaji WANYANG'ANYWE NYUMBA TU BAASI
   
 18. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #18
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  .......nyumba zirudishwe zote,,basi!!!.......bado sana!!..hiyo inatakiwa afanye kabla ya mwaka 2010....isije ikawa ajenda!
   
Loading...