Nyumba zilizojengwa chini ya nyaya za umeme Dar kubomolewa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba zilizojengwa chini ya nyaya za umeme Dar kubomolewa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 6, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki
  Mkoa wa Dar es Salaam unatarajia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zote na sehemu za biashara zilizojengwa chini ya nyaya za umeme wa msongo mkubwa, likiwamo soko la wafanyabiashara ndogondogo, maarufu kama 'Wamachinga' lililopo eneo la Tazara Vetenari.


  Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa huo, Saidi Meck Sadiki, wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) na kuwaagiza wakurugenzi wa halmashauri kusimamia zoezi hilo, ambalo alisema anataka lianze mara moja.


  Alisema ni hatari kwa watu kujenga na kuendesha shughuli zao chini ya nyaya za umeme wa msongo mkubwa kwa kuwa kunaweza kuhatarisha maisha yao mali zao.


  “Mkoa wa Dar es Salaam ni vurugu tupu. Na nawaagiza watendaji wote wa halmashauri tatu za mkoa huu kuhakikisha wavamizi hao wanaondolewa haraka ili sehemu hizo zibaki wazi,” alisema.


  Alisema amelijulisha Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), kuhusiana na zoezi hilo na kwamba wote waliovamia, hakuna atakayepona.


  “Ukicheka na nyani utavuna mabua. Hatuwezi kuendelea kuona watu waliovamia maeneo ya chini ya nyaya za umeme wa msongo mkubwa wakiendelea kukaa hapo na kuendesha shughuli zao,” alisema.


  Alisema hata kama watu hao walipewa maeneo hayo kihalali lazima waondoke kwa kuwa hairuhusiwi kujenga kitu chochote chini ya nyaya za umeme.


  Kuhusu wamachinga, Sadiki aliagiza Manispaa ya Ilala kuanza kuwaondoa wale wanaofanya biashara zao jirani na lango la kuingilia ofisini kwake na kama wameshindwa kufanya kazi hiyo waseme ili aifanye yeye mwenyewe.


  “Nataka wamachinga wote wanaofanya biashara sehemu za watembea kwa miguu waondoke na kuacha maeneo hayo yakiwa wazi. Na hili lazima lisimamiwe na manispaa zote tatu za jiji la Dar es Salaam,” alisema.


  Aliwataka watendaji mkoani humo kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuvikimbia vyombo vya habari na kwamba kama kila mmoja atatimiza wajibu wake, atawaona waandishi wa habari marafiki zake.


  “Timizeni wajibu wenu kama mtaona mnafuatwafuatwa na vyombo vya habari. Kinachofanya mfuatwefuatwe ni kutokana na utendaji wenu mbovu na mapungufu mbalimbali mliyonayo,” alisema.


  Kuhusu fidia kwa wakazi wa mabondeni waliokumbwa na mafuriko mwishoni mwaka jana eneo la Jangwani na Msimbazi ambao walipewa viwanja eneo la Mabwepande Wilaya ya Kinondoni, Sadiki alisema serikali haina mpango wowote wa kuwajengea nyumba wananchi hao.
  [​IMG]


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Sirikali ya nyinyiem mawenge kweli jangwani bado naona watu wanaendleza mahsha msimbazi ndio kabisa watu washasahau mafuriko kama yalipita.weng waliopewa viwanja ni wale nyumb zilibomoka.serikali ya kisanii
   
 3. luck

  luck JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 3, 2009
  Messages: 771
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 80
  Nimeona hiyo kitu mtaani kwangu. Wafanyabiashara ndogondogo walio chini ya hizo nyaya wameshaanza kuondoka.

  Ni nzuri kwa usalama wao kwa sababu umeme ukileta balaa hauchagui mtu!
   
 4. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Nashindwa kuelewa serikali yetu ina nini kila idara ni rabsha tupu, hivi kama kweli serikali iko imara wavamizi wa maeneo wataanzia wapi?
  Ilitakiwa wanapoamua kugawa maeneo/viwanja idara husika ihakikishe kuwa kuna kila huduma muhimu ya kijamii kama barabara, nyaya za umeme, maji safi, na taka, nk.nk. eneo unakuta ni pori watu wanfyeka na kuishi humo baada ya miaka kadhaa ni wavamizi! mlikuwa wapi kama si ufujaji wa pesa za walipa kodi????
   
 5. SILENT WHISPER

  SILENT WHISPER JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 2,231
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  mlikuwa wapi wakati wanachimba misingi ya hizo nyumba..??? shame on u..! u r the reason why this city stinks ...! too much bhlaa bhlaaa!
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Moto wa mabua huu. Ni upepo tu, kama zilivyo pepo zingine zilizotangualia
   
Loading...