Nyumba zaidi ya 100 Mbezi Beach kubomolewa kwa nguvu!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,977
20,243
Nyumba zaidi ya 100.Mbezi Beach Zilizo jirani na baharini kubombolewa kufuatia kukiuka sheria za majenzi!

Chanzo ITV
 
Itawezekana kama wenye nchi siyo au hawatakuwa waathirika wa huo mchakato.
 
Walipokuwa wanajenga wenye mamlaka hawakuwaona?

Wengi wameingia hasara kwa mtindo huu, wakati wa ujenzi wakafanikiwa kupata vibali manispaa kwa njia za panya lakini maofisa serikalini hubadilika, anapokuja mwingine hamjuani na kinachofuata ni maumivu.

Poleni sana wajanja wa Mbezi BEach!
 
Hivi mtindo huu utaisha lini ? nyumba zinajengwa na miaka kupita halafu wahusika wanazinduka usingizini,eti nyumba ya ghorofa 16 inajengwa karibu na Ikulu hawaoni imeisha wanadai imekiuka sheria,hapo ni kufukuza kazi wote vijana kibao wanatembea na digrii zao wanahitaji kazi.
 
Nyumba zaidi ya 100.Mbezi Beach Zilizo jirani na baharini kubombolewa kufuatia kukiuka sheria za majenzi!

Chanzo ITV
Hizi kelele tushazisikia sana hadi sasa masikio yamekuwa sugu. Hazina jipya. wakibomoa sawa wakiacha sawa kwa maana hazitukwamui na kututoa hapa tulipo.
 
Wanawatafutia ulaji wa zaidi ya kodi watazopata kama ilivyokuwa kwa wenye majengo pale Oyterbay. Kesi ni lazima washinde.

Nakumbuka jengo moja Kariakoo, lilipokuwa likianza kujengwa, engineer wa City akaja kusema "niwape ujanja wa kupata fedha za haraka? Mkikubali tugawane, kazi yote ntaifanya mimi".

Hiyo ya Mbezi ni ulaji tu huo unasukwa.

Bomoa, kesi, ushindi, serikali inalipa mara mia zaidi ya kodi itayokusanywa na mwenye nyumba kwa miaka 50 ijayo.
 
Nyumba zaidi ya 100.Mbezi Beach Zilizo jirani na baharini kubombolewa kufuatia kukiuka sheria za majenzi!

Chanzo ITV
Hizi ni ndoto za mchana hii ni hadithi kama hadithi thingine tu mfano mawaziri kuhamia dodoma ili kuenzi mji mkuu wetu wz dodoma
 
Wanawatafutia ulaji wa zaidi ya kodi watazopata kama ilivyokuwa kwa wenye majengo pale Oyterbay. Kesi ni lazima washinde.

Nakumbuka jengo moja Kariakoo, lilipokuwa likianza kujengwa, engineer wa City akaja kusema "niwape ujanja wa kupata fedha za haraka? Mkikubali tugawane, kazi yote ntaifanya mimi".

Hiyo ya Mbezi ni ulaji tu huo unasukwa.

Bomoa, kesi, ushindi, serikali inalipa mara mia zaidi ya kodi itayokusanywa na mwenye nyumba kwa miaka 50 ijayo.
Sawa kabisa!
Kwa mara ya kwanza leo umeongea kwa hulka ya kitazania halisi!!
 
Wanawatafutia ulaji wa zaidi ya kodi watazopata kama ilivyokuwa kwa wenye majengo pale Oyterbay. Kesi ni lazima washinde.

Nakumbuka jengo moja Kariakoo, lilipokuwa likianza kujengwa, engineer wa City akaja kusema "niwape ujanja wa kupata fedha za haraka? Mkikubali tugawane, kazi yote ntaifanya mimi".

Hiyo ya Mbezi ni ulaji tu huo unasukwa.

Bomoa, kesi, ushindi, serikali inalipa mara mia zaidi ya kodi itayokusanywa na mwenye nyumba kwa miaka 50 ijayo.

Dada FF, Hapa ndo huwa nashindwa kukuelewa kabisa. Kumbe unatambua madhambi ya Serikali yako lakini kila uchwao unawapigia debe? Au wamekuzima mgao wa Igunga?
 
hahaha! kumbe hujui,huyu mama swala lolote linaloweza kugusa kwao Kariakoo mtaonana wabaya,bomoa ikianza Mbezi si inaweza hamia Kariakoo ? pale kuna nyumba zina vibali vya ghorofa 4 lakini wamejenga hadi 8.
 
Dada FF, Hapa ndo huwa nashindwa kukuelewa kabisa. Kumbe unatambua madhambi ya Serikali yako lakini kila uchwao unawapigia debe? Au wamekuzima mgao wa Igunga?

Serikali ni nani? hata mimi na wewe ni Serikali. Ni wapi uliwahi kusikia FF akisema Tanzania hakuna wezi?

Tatizo mlilo nalo ni kuwa kila mtu ni mwizi, la hasha, bado kuna watu wema wengi sana Tanzania.

Kuna wizi zaidi ya kukwapua akiba za watu za uzeeni na kukataa kuzirudisha? kuna wizi zaidi ya kuuza vi Fuso used vya million 30 million 500?

Hebu funguweni macho japo kidogo.
 
Wanawatafutia ulaji wa zaidi ya kodi watazopata kama ilivyokuwa kwa wenye majengo pale Oyterbay. Kesi ni lazima washinde.

Nakumbuka jengo moja Kariakoo, lilipokuwa likianza kujengwa, engineer wa City akaja kusema "niwape ujanja wa kupata fedha za haraka? Mkikubali tugawane, kazi yote ntaifanya mimi".

Hiyo ya Mbezi ni ulaji tu huo unasukwa.

Bomoa, kesi, ushindi, serikali inalipa mara mia zaidi ya kodi itayokusanywa na mwenye nyumba kwa miaka 50 ijayo.

Sikilizeni haya ndio magamba yenyewe yanazungumza kwani mbinu zao wanajuana!!
 
Serikali ni nani? hata mimi na wewe ni Serikali. Ni wapi uliwahi kusikia FF akisema Tanzania hakuna wezi?

Tatizo mlilo nalo ni kuwa kila mtu ni mwizi, la hasha, bado kuna watu wema wengi sana Tanzania.

Kuna wizi zaidi ya kukwapua akiba za watu za uzeeni na kukataa kuzirudisha? kuna wizi zaidi ya kuuza vi Fuso used vya million 30 million 500?

Hebu funguweni macho japo kidogo.
Uimara wa hoja yako hapo juu umeupoteza kwa komenti hii dada!
 
mama ITIBAIJUKA muulize mzee Isac Cheyo,alikuja na sera kama hizo yuko wapi

Hiki kibibi kizee mzigo tu kwa JK. Hakuna alichofanya cha kuonyesha tangu apewe wizara. Yeye anachokomalia kila kukicha utasikia nitabomoa hapa, kesho kule. Watu mlioko serikalini tambueni kwamba kazi kuu ya serikali yoyote duniani ni kulinda raia na mali zao. TZ ni vingine
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom