Nyumba za wageni kichochea cha ngono Kinondoni, Dar es Salaam

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
NYUMBA nyingi za wageni zisizosajiliwa katika Manispaa ya Kinondoni zimesababisha kiwango cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi kuwa juu kwa asilimia 7.8 ikilinganishwa na kiwango cha kitaifa cha asilimia 5.7.

Akizungumza na gazeti hili Ofisa Uhusiano wa Manispaa hiyo, Sebastian Mhowera alisema nyumba hizo za wageni na sehemu nyingi za burudani kama baa na kumbi za muziki, zinachangia kuwepo kwa vichocheo vya maambukizi licha ya jitihada zinazofanyika kudhibiti tatizo hilo.

“Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa biashara ya ngono ambapo wanawake wanauza miili yao kwa ajili ya kupata fedha na wanaume wanafanya mapenzi na wanaume wenzao,” alisema Mhowera.

Alisema pia kuna matumizi makubwa ya dawa za kulevya na ongezeko la wahamiaji kutoka mikoani kwa ajili ya kutafuta maisha, limesababisha mwingiliano mkubwa wa watu ambapo
kufikia mwaka jana, manispaa hiyo inakadiriwa kuwa na ongezeko watu la asilimia 4.1.

Hata hivyo manispaa hiyo imekuwa ikitoa elimu ya kujikinga na Ukimwi kwa makundi mbalimbali wakiwemo watumishi wake, wahudumu wa baa na nyumba za wageni, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, vijana nje ya shule na waendesha magari ya masafa ya mbali.

Mhowera alisema pamoja na elimu hiyo, bado wanakabiliwa na changamoto ya jamii kutobadili tabia na kusababisha maambukizi mapya kutokana na ongezeko la makundi ya
wanaotumia dawa za kulevya na wanaojiuza na maeneo hatarishi.
 
Tatizo ni matumizi ya madawa ya kulevya...biashara inayoshikiliwa na 'wakubwa'.....ni vigumu kuizuia!
 
Back
Top Bottom