Nyumba za Uswahilini nyingi hazifanyiwi finishing

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Kinachofurahisha mijini ni kuwa nyumba za nyasi na matope zinapotea au kumalizika kabisa. Kila mjengaji hujitahidi kutumia matofali ya saruji, madirisha yanayoingiza hewa.

Tatizo ni kuwa nyumba zetu nyingi huku Uswaz hazifanyiwi finishing na wakazi wanaishi bila matatizo.

Mitaa ya Kwamtogole au Bhuza utakuta nyumba zenye finishing mtaa mzima zinahesabika.

Wengine wakuambia chumba self utalipa 80,000. Ukifika chumba self hakuna mlango kati ya chumba na choo, choo hakina seat ya kukalia na mwenye nyumba haoni kasoro.
 
Sina uhakika kama Tanzania kuna sheria ya ujenzi inayolazimisha nyumba za eneo fulani ziwe na muonekano fulani...

Kama sheria hiyo ipo basi haisimamiwi kabisa...
 
Sina uhakika kama Tanzania kuna sheria ya ujenzi inayolazimisha nyumba za eneo fulani ziwe na muonekano fulani...

Kama sheria hiyo ipo basi haisimamiwi kabisa...
Kama tu nyumba ikiwa haijaisha tayari mamlaka za serikali zinaanza kuleta invoice za kodi ya jengo unategemea nini, maana ukipiga bati tu na kuweka grill na ukaweka mtu aishi kwa usalama wa nyumba serikali inakuja kudai kodi ya jengo badala ya kujiridhisha kwamba jengo limeisha ndio udai kodi ya jengo.

Kilichopo ni kuchukua kibali cha ujenzi baada ya kulipia na hakuna anaefuatilia kama hiyo ramani iliyopitishwa kama imefuatwa maana unaweza ukachukua kibali cha ujenzi kwa ramani nyingine na ukaja ukajenga nyumba ina mfanano tofauti na ramani na bado ikawa sawa tu...watapita kwa jirani yako ambae hana kibali cha ujenzi na kuandika ukutani "simamisha ujenzi au wasilisha kibali cha ujenzi ofisini" lakini wewe mwenye kibali uliejenga tofauti na ramani uliyowasilisha Manispaa / Jiji wanakupita maana wanahesabu una kibali.

Ila Dodoma walikuwa wanafuatilia enzi zile za CDA ila mwisho wa siku kwenye finishing sasa inatokana na mfuko wa mtu yaani wakishakagua mpaka hatua ya renta hapo inakuwa mwisho kunako endelea kwingine hawahusiki
 
Kinachofurahisha mijini ni kuwa nyumba za nyasi na matope zinapotea au kumalizika kabisa. Kila mjengaji hujitahidi kutumia matofali ya saruji, madirisha yanayoingiza hewa.

Tatizo ni kuwa nyumba zetu nyingi huku Uswaz hazifanyiwi finishing na wakazi wanaishi bila matatizo.

Mitaa ya Kwamtogole au Bhuza utakuta nyumba zenye finishing mtaa mzima zinahesabika.

Wengine wakuambia chumba self utalipa 80,000. Ukifika chumba self hakuna mlango kati ya chumba na choo, choo hakina seat ya kukalia na mwenye nyumba haoni kasoro.
🤣🤣🤣🤣kama hutaki za 80k nenda kalipe za 300k makumbusho zina finishing.

Uswazi tuachie sisi na maisha yanasonga vizuri tu
 
Back
Top Bottom