Kikwete: Tutazirudisha baadhi ya nyumba za serikali zilizonunuliwa

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,006
2,166
Kikwete: Tutazirudisha baadhi ya nyumba za serikali zilizonunuliwa
By Habari Tanzania | Published 10/3/2006.

RAIS Jakaya Kikwete, amesema serikali yake imefikia uamuzi wa kuzirejesha baadhi ya nyumba za serikali zilizouzwa kwa watumishi wa umma baada ya kubaini kwamba zilijengwa katika mazingira nyeti.

Kikwete aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akijibu maswali ya wahariri wakuu wa vyombo mbalimbali vya habari aliokutana nao chini ya kivuli cha utaratibu aliojipangia wa kuzungumza na wananchi kila mwishoni mwa mwezi.

Hatukusudii kuzichukua nyumba zotekwa mfano kuna OCD kauziwa nyumba ya OCD iliyo katika eneo la polisi, na yule OCD aliyeuziwa kahamishwa kutoka Mtwara kwenda Mafiaau kastaafu na nyumba kapangishaKwa kweli kuna maeneo ambayo lazima tufanye marekebisho, alisema Kikwete.

Ingawa hakufafanua iwapo uhakiki wa nyumba zitakazorejeshwa umeshafanyika au la, na wakati hasa utakapoanza utekelezwaji wa kazi hiyo, kauli yake hiyo imehitimisha minongono na malumbano ambayo yamekuwapo kwa muda sasa, kuhusu suala hilo.
................................. etc.
-----------------------------------------------------------
Ajira milioni moja hatujui kama zimefikiwa na ni vigumu kuzitetea. Hili la nyumba liko wazi. Halijatekelezwa. Mwaka huu tena tupewe ahadi zisizotekelezwa kwa jina la siasa?
 
Kikwete: Tutazirudisha baadhi ya nyumba za serikali zilizonunuliwaBy Habari Tanzania | Published 10/3/2006.
RAIS Jakaya Kikwete, amesema serikali yake imefikia uamuzi wa kuzirejesha baadhi ya nyumba za serikali zilizouzwa kwa watumishi wa umma baada ya kubaini kwamba zilijengwa katika mazingira nyeti.

Kikwete aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akijibu maswali ya wahariri wakuu wa vyombo mbalimbali vya habari aliokutana nao chini ya kivuli cha utaratibu aliojipangia wa kuzungumza na wananchi kila mwishoni mwa mwezi.

"Hatukusudii kuzichukua nyumba zote…kwa mfano kuna OCD kauziwa nyumba ya OCD iliyo katika eneo la polisi, na yule OCD aliyeuziwa kahamishwa kutoka Mtwara kwenda Mafia…au kastaafu na nyumba kapangisha…Kwa kweli kuna maeneo ambayo lazima tufanye marekebisho," alisema Kikwete.

Ingawa hakufafanua iwapo uhakiki wa nyumba zitakazorejeshwa umeshafanyika au la, na wakati hasa utakapoanza utekelezwaji wa kazi hiyo, kauli yake hiyo imehitimisha minong'ono na malumbano ambayo yamekuwapo kwa muda sasa, kuhusu suala hilo.
................................. etc.
-----------------------------------------------------------
Ajira milioni moja hatujui kama zimefikiwa na ni vigumu kuzitetea. Hili la nyumba liko wazi. Halijatekelezwa. Mwaka huu tena tupewe ahadi zisizotekelezwa kwa jina la siasa?

Siku zikiwa zinasogea hivi kuelekea uchaguzi tutasikia mengi sana...Waache bana wajikanganye , huenda Mungu akatuona, tukasaidika japo mida hii!
 
Katika upuuzi ambao uliwahi kufanywa na serikali zoote madarakani huu wa nyumba ni komesha. Gharama yake inazidi Epa ndiyo maana leo hii wanajenga nyumba kwa billions.
 
Kikwete: Tutazirudisha baadhi ya nyumba za serikali zilizonunuliwaBy Habari Tanzania | Published 10/3/2006.
RAIS Jakaya Kikwete, amesema serikali yake imefikia uamuzi wa kuzirejesha baadhi ya nyumba za serikali zilizouzwa kwa watumishi wa umma baada ya kubaini kwamba zilijengwa katika mazingira nyeti.

Kikwete aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akijibu maswali ya wahariri wakuu wa vyombo mbalimbali vya habari aliokutana nao chini ya kivuli cha utaratibu aliojipangia wa kuzungumza na wananchi kila mwishoni mwa mwezi.

“Hatukusudii kuzichukua nyumba zote…kwa mfano kuna OCD kauziwa nyumba ya OCD iliyo katika eneo la polisi, na yule OCD aliyeuziwa kahamishwa kutoka Mtwara kwenda Mafia…au kastaafu na nyumba kapangisha…Kwa kweli kuna maeneo ambayo lazima tufanye marekebisho,” alisema Kikwete.

Ingawa hakufafanua iwapo uhakiki wa nyumba zitakazorejeshwa umeshafanyika au la, na wakati hasa utakapoanza utekelezwaji wa kazi hiyo, kauli yake hiyo imehitimisha minong’ono na malumbano ambayo yamekuwapo kwa muda sasa, kuhusu suala hilo.
................................. etc.
-----------------------------------------------------------
Ajira milioni moja hatujui kama zimefikiwa na ni vigumu kuzitetea. Hili la nyumba liko wazi. Halijatekelezwa. Mwaka huu tena tupewe ahadi zisizotekelezwa kwa jina la siasa?

Hadithi njoo utamu kolea!
 
Hizi nyumba zilisharudishwa. Nakumbuka waziri wa miundo mbinu aliripoti mbungeni.
 
Kikwete: Tutazirudisha baadhi ya nyumba za serikali zilizonunuliwaBy Habari Tanzania | Published 10/3/2006.

"Hatukusudii kuzichukua nyumba zote…kwa mfano kuna OCD kauziwa nyumba ya OCD iliyo katika eneo la polisi, na yule OCD aliyeuziwa kahamishwa kutoka Mtwara kwenda Mafia…au kastaafu na nyumba kapangisha…Kwa kweli kuna maeneo ambayo lazima tufanye marekebisho," alisema Kikwete.

Majibu mazuri na ya ulaghai yatakuwepo..wanasiasa wapo makini ktk kuchagua setensi za utata........
 
wakati mkapa anauza alifikiri ni jambo jema sasa wamejenga moja tu bilioni 1.2 na wakati huo huo waliuza nyumba 6000.

Nyumba zote za TRC dar na kwingineko ziliuzwa zote na zilinunuliwa na wakubwa wa TRC na hata pinda sijui kama hana moja ya hizo nyumba.
 
Huwezi kumpa mtu kitu ambacho huna! JK hawezi kurudisha hizo nyumba. Ila alijua tunataka kusikia nini, na kama mwanasiasa ndicho alichokuwa anakisema. Mbona siku zinakwenda hamna lolote alilolifanya kwenye ahadi zake? Au anafikiri tumesahau?
 
Wewe ulimpa kura yako ukitegemea nyumba zirudi? Oh pole sana, mwaka huu atasema mkakati wa kurudisha umeanza ili udanganyike tena!!
 
kwa sababu hiyo kila mtu aende nyumbani utaratibu wa uongozi wa mpito tutaitoa. hakuna kazi wiki nzima ni mapumziko
 
Hizi nyumba zilisharudishwa. Nakumbuka waziri wa miundo mbinu aliripoti mbungeni.

Kawambwa alisoma bungeni orodha ya nyumba ambazo walitegemea kuzirudisha lakini nyingi hazikurudishwa kwa kisingizio cha kwamba waliozinunua wamezikarabati kwa fedha nyingi kwahiyo kama serikali ingezirudisha ingepaswa kulipa fedha nyingi zaidi kuliko walizotoa wahusika walipozinunua!! Kuna waziri mmoja mstaafu wa awamu ya nne aliuziwa nyumba ya taasisi ambayo alitakiwa kuirudisha kufuatana na taarifa ya Kawambwa lakini nyumba ile iliyoko Oysterbay mpaka sasa haijarudishwa na muhusika anaipamgisha. All in all serikali haijarudisha zile nyumba wananchi walizotegemea zitarudishwa kama zile za wakina Marten Lumbanga et al ambazo walizikarabati kwa mamiloni ya shilingi halafu wakajazinunua kwa bei ya kutupa!! Kikwete kama kawaida katuhadaa wadanganyika!!
 
Alisha sema hana mpango kuzirudisha kwa vile yeye alipewa. Maanake kama asingepewa angechukua hatua. Kwake hiyo ni hongo
 
Hizi nyumba zilisharudishwa. Nakumbuka waziri wa miundo mbinu aliripoti mbungeni.

Twataka nyumba zote za Serikali zirudishwe ili watumishi wa serikali waendelee kuishi kwenye nyumba hizo kama ilivyokusudiwa. Kulikuwa hakuna sababu yoyote ya kuziuza nyumba hizo zaidi ya sababu za ubinafsi na kutojali maslahi ya Taifa.
 
Back
Top Bottom