Nyumba za Serikali ktk ahadi za Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba za Serikali ktk ahadi za Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MchunguZI, Jan 17, 2010.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Kikwete: Tutazirudisha baadhi ya nyumba za serikali zilizonunuliwaBy Habari Tanzania | Published 10/3/2006.
  RAIS Jakaya Kikwete, amesema serikali yake imefikia uamuzi wa kuzirejesha baadhi ya nyumba za serikali zilizouzwa kwa watumishi wa umma baada ya kubaini kwamba zilijengwa katika mazingira nyeti.
  Kikwete aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akijibu maswali ya wahariri wakuu wa vyombo mbalimbali vya habari aliokutana nao chini ya kivuli cha utaratibu aliojipangia wa kuzungumza na wananchi kila mwishoni mwa mwezi.

  “Hatukusudii kuzichukua nyumba zote…kwa mfano kuna OCD kauziwa nyumba ya OCD iliyo katika eneo la polisi, na yule OCD aliyeuziwa kahamishwa kutoka Mtwara kwenda Mafia…au kastaafu na nyumba kapangisha…Kwa kweli kuna maeneo ambayo lazima tufanye marekebisho,” alisema Kikwete.


  Ingawa hakufafanua iwapo uhakiki wa nyumba zitakazorejeshwa umeshafanyika au la, na wakati hasa utakapoanza utekelezwaji wa kazi hiyo, kauli yake hiyo imehitimisha minong’ono na malumbano ambayo yamekuwapo kwa muda sasa, kuhusu suala hilo.
  ................................. etc.
  -----------------------------------------------------------
  Ajira milioni moja hatujui kama zimefikiwa na ni vigumu kuzitetea. Hili la nyumba liko wazi. Halijatekelezwa. Mwaka huu tena tupewe ahadi zisizotekelezwa kwa jina la siasa?
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Siku zikiwa zinasogea hivi kuelekea uchaguzi tutasikia mengi sana...Waache bana wajikanganye , huenda Mungu akatuona, tukasaidika japo mida hii!
   
 3. b

  bnhai JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Katika upuuzi ambao uliwahi kufanywa na serikali zoote madarakani huu wa nyumba ni komesha. Gharama yake inazidi Epa ndiyo maana leo hii wanajenga nyumba kwa billions.
   
 4. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hadithi njoo utamu kolea!
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hizi nyumba zilisharudishwa. Nakumbuka waziri wa miundo mbinu aliripoti mbungeni.
   
 6. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  Majibu mazuri na ya ulaghai yatakuwepo..wanasiasa wapo makini ktk kuchagua setensi za utata........
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wakati mkapa anauza alifikiri ni jambo jema sasa wamejenga moja tu bilioni 1.2 na wakati huo huo waliuza nyumba 6000.

  Nyumba zote za TRC dar na kwingineko ziliuzwa zote na zilinunuliwa na wakubwa wa TRC na hata pinda sijui kama hana moja ya hizo nyumba.
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,335
  Likes Received: 1,798
  Trophy Points: 280
  Huwezi kumpa mtu kitu ambacho huna! JK hawezi kurudisha hizo nyumba. Ila alijua tunataka kusikia nini, na kama mwanasiasa ndicho alichokuwa anakisema. Mbona siku zinakwenda hamna lolote alilolifanya kwenye ahadi zake? Au anafikiri tumesahau?
   
 9. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wewe ulimpa kura yako ukitegemea nyumba zirudi? Oh pole sana, mwaka huu atasema mkakati wa kurudisha umeanza ili udanganyike tena!!
   
 10. tgeofrey

  tgeofrey JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 526
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa sababu hiyo kila mtu aende nyumbani utaratibu wa uongozi wa mpito tutaitoa. hakuna kazi wiki nzima ni mapumziko
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kawambwa alisoma bungeni orodha ya nyumba ambazo walitegemea kuzirudisha lakini nyingi hazikurudishwa kwa kisingizio cha kwamba waliozinunua wamezikarabati kwa fedha nyingi kwahiyo kama serikali ingezirudisha ingepaswa kulipa fedha nyingi zaidi kuliko walizotoa wahusika walipozinunua!! Kuna waziri mmoja mstaafu wa awamu ya nne aliuziwa nyumba ya taasisi ambayo alitakiwa kuirudisha kufuatana na taarifa ya Kawambwa lakini nyumba ile iliyoko Oysterbay mpaka sasa haijarudishwa na muhusika anaipamgisha. All in all serikali haijarudisha zile nyumba wananchi walizotegemea zitarudishwa kama zile za wakina Marten Lumbanga et al ambazo walizikarabati kwa mamiloni ya shilingi halafu wakajazinunua kwa bei ya kutupa!! Kikwete kama kawaida katuhadaa wadanganyika!!
   
 12. D

  Deo JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Alisha sema hana mpango kuzirudisha kwa vile yeye alipewa. Maanake kama asingepewa angechukua hatua. Kwake hiyo ni hongo
   
 13. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Twataka nyumba zote za Serikali zirudishwe ili watumishi wa serikali waendelee kuishi kwenye nyumba hizo kama ilivyokusudiwa. Kulikuwa hakuna sababu yoyote ya kuziuza nyumba hizo zaidi ya sababu za ubinafsi na kutojali maslahi ya Taifa.
   
Loading...