Money Stunna
JF-Expert Member
- Aug 9, 2011
- 13,054
- 6,281
NYUMBA 215 zilizojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kuwauzia wanachama wake kwa bei nafuu eneo la Kijichi Dar es Salaam hazikamatiki baada ya gharama halisi anayotakiwa kulipa mwanachama kuwa kati ya Sh200 milioni na Sh260 milioni.
Benki ya Commercial Bank Of Afrika (CBA) ilidokeza hayo jana ilipokuwa ikitoa utaratibu wa kupata mkopo wa kununua nyumba hizo kupitia benki hiyo baada ya kuteuliwa na NSSF kuwasaidia mikopo wanachama waliotimiza masharti ya wali kununua nyumba hizo.
Ofisa wa CBA (jina lake linahifadhiwa) alimweleza mwanachama wa NSSF aliyefika kujua utaratibu wa kupata mkopo wa kununua nyumba hizo kwamba pamoja na NSSF kuwaeleza wanachama wake kwamba nyumba zitauzwa kati ya Sh90 milioni na Sh118 milioni, ukweli ni kwamba gharama halisi ni kati ya Sh200 milioni na Sh260,000 kulingana na hadhi ya nyumba.
Kwa mfano nyumba za 3A-3 zenye vyumba vitatu ambazo NSSF ilisema inahitaji Sh90 milioni, gharama halisi ni Sh214,500,000 zinazojumuisha gharama mbalimbali za mkopo utakaolipwa kwa miaka 20, alisema ofisa huyo.
Alisema utaratibu wa kupata mkopo ni kwamba CBA inatoa asilimia 90 ya bei halisi na kwamba riba ni asilimia 19.5 huku mkopaji akitakiwa kukatwa asilimia 45 ya mapato ya mkopaji kila mwezi.
Ukitaka nyumba ambayo NSSF inataka irudishiwe Sh90 milioni, basi utakuwa ukikatwa Sh1.45 milioni kila mwezi ili kurudisha mkopo kwa muda wa miaka 20, alisema.
Mbali ya gharama ya riba kufikia Sh214.5 milioni katika kununua nyumba hiyo, lakini mteja pia atatakiwa kugharimia masuala ya kisheria, uthamini wa nyumba, uwezeshaji, na kuingia kwenye bima.