Nyumba za NHC kwa nini wasipewe Walimu na Madaktari?

mooduke

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
628
111
Jamani mimi nafikiri kwa kuwa nyumba za shirika la nyumba ni mali ya umma kwa nini Bunge lisitunge sheria kwamba watumishi wa umma kama walimu na madaktari kisheria wakapewa kipaumbele kupangishwa nyumba hizo kulinga na mahali anapofanyia kazi mtumishi huyo?
 
Jamani mimi nafikiri kwa kuwa nyumba za shirika la nyumba ni mali ya umma kwa nini Bunge lisitunge sheria kwamba watumishi wa umma kama walimu na madaktari kisheria wakapewa kipaumbele kupangishwa nyumba hizo kulinga na mahali anapofanyia kazi mtumishi huyo?

Wahindi unataka wakakae wapi wewe
 
MAT walikaa na wahusika wa NHC kuhusu kuuziwa nyumba zinazouzwa na NHC.Katika majadiliano hawakufikia muafaka kwa sababu kiwango ambacho inabidi uchangie kwa mwezi unabaki bila kitu mfukoni.juhudi za kuwashawishi wapunguze kiwango cha makato kwa mwezi ziligonga mwamba.KIWANGO CHA MSHAHARA WANACHOPATA MADAKTARI NI KIDOGO KIASI KWAMBA HAWAKOPESHEKI NA NHC
 
Ndugu yangu Mooduke, mawazo yako nayaunga MKONO, Lakini tofauti yangu na wewe ni kwamba Hao Waalimu na Madaktrari kupewa hizo nyumba itakuwa sio sawa kwa maana hivi NHC ni shirika la kibiashara likiwa linajenga nyumba na kugawa wao pesa watapata wapi? Jambo la kuangalia ni kwamba serikali ikae na NHC kuingia mkataba utakao simamiwa kisheria (Contract) ili kufanya mpango wa kutoa kipa umbele kuwa NAFASI kwanza iwe ni waalimu, madaktrari, manesi wanajeshi police na watu wote muhimu wanao hudumia wananchi, ama kwa kununu au kupanga kwa bei nafuu ambayo wahusika wataweza kuimudu, wanunuzi wapewe muda mrefu wa wao kulipia hizo nyumba endapo watazinunua, kwa mfano nyumba ina gharimu milioni 60 au vyovyote vile basi apewe muda sio kuambiwa baada ya miaka miwili deni liwe limekwisha, kwani hata akiamua kukabidhi mshahara wake wote kwa NHC haitowezekana kumaliza deni, wafanye mpango wa muda mrefu kama lease za viwanja, na kama mtu hana uwezo wa kununua basi apewe kipaumbele cha kuwa mpangaji na pango liwe bei nafuu kutokana na mshahara wake, mimi nimesikia mara nyingi watu wanasema kuwa kunabaadhi ya mashirika kama vile NSSF, NHC na mengineyo wanajenga nyumba ili kuwauzia wananchi wenye vipato vya chini, lakini uliza basi bei ya hiiyo nyumba ya mwenye kipato cha chini utashangaa maana mimi kwa kweli hata sijui kipato cha chini ni shs ngapi kwa mwezi. Kwa hiyo serikali ikae ilifikirie hilo, maana nchi zilizoendelea hutoa mikopo na mapango kwa kuwapa kipaumbele wafanyikazi serikalini ambao huitwa KEY WORKERS, mfano Madaktari, manesi, waalimu, wanajeshi, polisi n.k kwa maana ya wale watu wanaotoa huduma muhimu kwa UMMA." MCHEZA KWAO HUTUNZWA"
Basi serikali iwatunze watu wao kwa kuwarahisishia makali ya maisha.:eyebrows: (TIZAMENI):eyebrows:
 
Suala hapa ni kwamba serikali ijenge nyumba karibu na maeneo wanayofanyia kazi. Kama mwalimu wa Bunge Primary School atauziwa nyumba karibu na bunge itakuwaje akihama?
 
Ndio waliokuwa na hizo nyumba, wakawauzia wahindi tenancy za jamuhuri, makunganya street n.k na wao kuhamia tabata, mbagala n.k
 
Back
Top Bottom