kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,222
- 1,670
Zile nyumba zilizojengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kuwauzia wanachama wake kwa bei nafuu ziko tayari, gharama halisi ni kati ya sh200 milioni na sh260 milioni. Benki ya CBA imeteuliwa na NSSF kuwakopesha wanachama waliotimiza marsharti, na mkopo utalipwa kwa miaka 20! CBA itatoa asilimia 90 ya bei kwa riba ya 19.5% na mkopaji akitakiwa kukatwa 45% ya mapato kila mwezi. CBA wameeleza kuwa kwa mfano ukitaka nyumba ambayo NSSF inataka irudishiwe sh90 milioni, utakuwa ukikatwa 1.45 milioni kila mwezi ili kurudisha mkopo kwa muda wa miaka 20. Mbali ya riba, mteja atatakiwa kugharamia masuala ya kisheria, uthamini wa nyumba, uwezeshaji na kuingia mkataba wa bima. Source by Mwananchi: Naam wanafao la kujitoa changamkeni, Ndugu Ramadhan Dau' kaisha wawezesha, nyumba hizo za bei nafuu!