Nyumba za kupanga, watoto wa wenye nyumba ni mwiba

Google Diggers

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
940
1,123
Title inajielezea, niende kwenye mada hii. Wakati naishi nyumba ya Mama mmoja mumewe aliishatangulia mbele ya haki. Allah amlipe mema.

Watoto wa nyumba hiyo hawakunipendeza hata kidogo. Wana jeuri, dharau, majivuno, kibri na kujiona werevu na hawajui wenye shida hawafikirii hata aliyejenga nyumba yao ametangulia, na sote tutarejea.

Kila utakalofanya halikubaliki, utakapopita haparuhusiwi, utakaposhika utachafua, wana kutreat kama mtu wa chini sana wakati hawakujui, hawajui unafanyashughuli gani, una kausafiri kako parking hairuhusiwi watoto wana nongwa hao sijapata kuona. Yaani hawa siku atapangisha ntu na silaha anawafyekelea mbali

Niliishi nyumba za kupanga yapata miaka 15. Nyumba hiyo ya #9 katika makazi niliyopata kukaa ile ilikuwa moto wa kuotea mbali. .

Kazi yao kuchungulia madirishani kuwatazama wapangaji, kutunga sheria mpya kila uchao.

Ukizaliwa kwenye familia yenye uwezo wazazi wakashindwa kukulea na maadili ya kibinadamu utachekesha sana. Sina hakika kama wale vijana watamudu maisha yao. Kwa namna walivyokuwa mwiba, unajiuliza kama wanajua watatakiwa waje kuishi na familia zao, wazitunze, wapate kazi, wajenge, nk.

Usiombee kuwa na watoto kwenye nyumba za kupanga, katika mazingira yale ukaondoka kwenda kibaruani, familia yako huko nyuma unaona kabisa itakerwa, ukirudi kazini watoto wanaanza kukushitakia, Mama tumenyimwa maji, Mama tumezimiwa umeme, baba hivi mara vile.

Hivi nchi hii haina sheria kweli kuwalinda wapangaji?
 
Nyumba ambazo wenye nyumba wanaishi hapohapo sio za kupanga, pia nyumba za urithi ambazo walioachiwa hawana kazi mjini wanategemea kula kwa kodi utakayolipa tabu sana kukaa.
 
Wewe nae kubwa jinga unajiandikiaga tu bila kushirikishaka bongo sijui huwaga una hang over ya gongo.
Point hapa kubwa ni hata kama mzazi unajiweza jitahidi watoto wako wawe na tabia njema wasiwe wanyanyasi kwa wengine.
Hukawii kusema mimi ni mpangaji, mimi ni mtoto wa mwenye nyumba na mpangaji kwingine.
Rudi kapange tena naona umemiss mashushu na kushushuliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hujawahi kukaa nyumba ya kupanga, niseme una bahati mbaya, ni experience nzr sana. Unajiimarisha, kiutu, imani, interaction, na mengine mengi.

Hizi nyumba zina vilanga vingi sana. Vituko
 
mbona simple tu,wengine huwa tunaita faza/maza house na kumwambia kabisa ainishe ni nani msemaji kwenye nyumba yake.au lah kuna mtu/watu atakula makofi na mitama.

uzuri wengine mapozi yetu tu usoni yanakuwa yana display sheria zote,kuna nyumba jamaa yangu alifanyiwa visa,halafu mimi napitwa tu,mpaka nikahisi labda wameniroga na kuniweka kiganjani.

usafi demu wa jamaa anasemeshwa,wangu anaachwa.
makelele ya redio hivyo.
umeme jamaa asichelewe,nongwa.
 
Back
Top Bottom