Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Huku kwetu Kwamtogole nyumba za kupanga ni kiinua mgongo endelevu. Haya yalianza enzi za mkoloni, makuli wengi wa bandarini ndiyo walikuwa Baba wenye nyumba.
Siku hizi wengi hupenda kuchukua chumba na sebule. Katika chumba na sebule Hii ni nyumba inayostir familia ya takriban watu watano-sita. Baba, mama na watoto watatu. Hii ni kaya ndani ya nyumba na unaweza kukuta nyumba ina kaya sita. Nyumba moja ina watu 30-40 wanaotumia maji, choo, na umeme kila siku.
Baba wenyenyumba wangepaswa kuwa sehemu ya uongozi wa serikali ya mtaa. Hawa wana uwezo wa kutambua wapangaji na wageni wa wapabgaji wao. Ni watu muhimu katika kuzuia vitendo vya uhalifu.
Wakati wa kupiga kura, mwenyenyumba ana nafasi kubwa ya kushawishi hasa wake wa wapangaji wake wakipigie chama gani. Anajua hali zao kiuchumi, akiweka siasa kidogo amepata wapiga kura kumi ndani ya nyumba moja.
Katika mipango ya maendeleo serikali izingatie idadi ya watu huku kwetu Uswahilini ni mara kumi ya ushuani.