Nyumba za kupanga ni degree tosha

Ndefu ila soma
Hii ni summary fupi ya nyumba nilizokaa.
Nyumba namba 1

Hii nyumba nilianza maisha nikiwa chuo. Nyumba ilikua na vyumba vine. Tulianza kulala kwenye mkeka baadaye nikanunua godoro. Nyumba haikua na maji wala umeme, maisha yalikua ni ya shida sana. Hatukua na choo tulikua tunajisaida choo cha nyumba ya jirani (nyumba za mtu mmoja). Nilihama baada ya kupata boom. Sikuwahi kufanya uvuvi ingawa jamaa niliyekua naye alikua anafanya uvuvi haramu.

Niliona kushea chumba ni utumwa maana inabidi ufuate ratiba za geto, hakuna excuse. Kupika na kuosha vyombo ni majukumu ya kila siku ukiwa ghetto.

Namba 2

Hii nyumba nilikaa baada yakuondoka nyumba namba moja. Nyumba ilikua siyo mbaya ila ilikua na makelele siku za jumapili maana ilikua jirani na kanisa kubwa la mtume mmoja. Nyumba haikua na maji kwa hiyo usafi ilikua kipengele.

Namba 3

Hiii nyumba kodi yake ilikua kubwa kuliko ya 1 na 2. Tulishea korido. Mimi ndio nilikua na feni jamaa walinilalia sana umeme. Walinituhumu kua nakesha na feni kwa hiyo namaliza umeme. Wapangaji wote walikua wanafunzi, maji yallikua yanasumbua na umeme pia. Maisha yalinipiga sana huku.

Namba 4

Hii nyumba ilikua ya mwanajeshi mmoja (RIP), maji tulikua tunachota kwake ila niliondoka baada ya miezi miwili ili nikae karibu na kituo cha kazi. Umeme haukuwahi kusumbua na majirani walikua wakarimu sana. Sababu ya kuondoka ni umbali mkubwa kutoka kazini kwangu.

Namba 5

Hii nyumba ilikua pembeni kidogo ya mji. Ilikua chumba na sebule. Changamoto yake ilikua umeme na maji. Bili zilikua zinatisha sana, halafu wanaokausha umeme walikua wagumu kulipa nakumbuka kuna mmama alitumia unit 90 za umeme halafu anakataa bili.Tulilazimika kukubali bili kwa kua walihusika na usafi wa chooni na bafuni. Hii nyumba choo chake kilikukua kisafi sana.

Namba 6.

Hii nyumba ilikua ya kishua. Ilikua imejitenga na haikua na usumbufu wa maji na umeme. Nilikua nakaa na mfanyakazi mwenzangu, tumefichiana siri za uvuvi sana. Maisha yalikua matamu sana. Uvuvi ulifanyika bila shida, japo kuna siku watu walimsanua demu wake ikatokea fumanizi dogo.

Namba 7

Hii nyumba ilikua chumba, sebule, kibaraza na choo. Maji yalikuepo ila yalikua na spidi sana kiasi cha kupasua mabomba ya maji. Changamoto kubwa ilikua kuvuja kwa maji kutokana na ukubwa wa presha ya maji. Bili zililipwa vizuri hadi alipohamia dada mmoja aliyekua anafanya kazi bar. Bili ziliongezeka balaa na maana kila asubuhi lazima akaushe nywele.

Namba 8

Hii nyumba nilihama baada ya mambo ya kiuchumi kuyumba kidogo msimu wa Corona. Hii nyumba ilikua njiani kabisa. Ilikua jirani na bar na wapita njia walipita mbele ya nyumba kwa hiyo usalama ulikua mdogo sana. Kuna siku nimeingia msalani nikaacha funguo mlangoni wezi wakapita na funguo na kufuli. Choo kilijaa tukaambiwa tuchange wavute maji, nilikaaa kidogo nikahama.

Namba 9.

Hii nyumba nilihamia baada ya Corona kuanza kuishiwa nguvu. Mishe mishe zikaanza kama kawaida nikarejea kwenye mishe zangu za kusaka ugali. Mwenye nyumba alikua na roho mbaya sana maana alifirisika (zamani alikua tajiri). Ana kijiji cha watoto. Maza house Mchana anaingia kwa mpangaji anaangalia TV. Faza house alikua anatongoza wake za wapangaji na alikua anawashika makalio, kuna ambao walikua wanachekelea nadhani alikua anawala bila waume zao kujua.

Namba 10.

Sasa bana kwenye hii nyumba maza house alikua ni mbibi mtu mzima na jirani yangu pia alikua mtu mzima (50+) huyu mama alikua na kamsela kama miaka 27 hivi kalikua kanampelekea moto. Wakigombana sauti yote unaskia. Halafu alikua anawasha jikola mafuta ya taa, akizima ,moshi wote unabaki ndani. Nyumba haikua na ventilation kabisa. Kuna kipindi maza house alianza ukarimu uliopitiliza, akawa analeta ndizi, kitimoto na vinono. Nikaona mama anakoelekea siko.

Hii nyumba nilikua naoekana wa kishua maana nilikua na kausafiri ka kuazima kwa hiyo nilikua navimba. Nikiwa kwenye hii nyumba majanga yalianza kunikuta usafiri wa watu ukawa na masuala ya kiufundi mengi yasiyoisha ilinikausha kama milioni hivi. Niliondoka baada ya kupata mrembo aliyeniambia hapo siyo hadhi yangu (huyu mrembo alinikacha kikatili japo nilihamia nyumba nzuri).

Hii nyumba ilikua na changamoto ya wizi pia, haipiti wiki hujaskia stori ya wezi kupitisha mikono madirishani, kwa hiyo ukilala unalala na nyundo au panga.

11. Itoshe kusema hii nyumba ilikua ya kishua (studio room ya kizungu siyo hizi za uswazi. Garden nzuri nje, feni, TV kitanda cha kishua. Choo kilikua kikubwa chenye heater kwenye shower. Ilikua ni furnished room yaani unaingia na begi lako tu. Haina makelele, haina usumbufu kodi yake ilikua ya kishua. Kale kausafiri ka kuazima niliona aibu kukapaki. Mimi peke yangu ndio nilikua na kausafiri kaajabu. Inshort mi ndio nilikua maskini kuliko wote.
KIla nikienda huu mkoa hua nabook chumba kwenye hii nyumba. Hua inanifanya napunguza stress zangu za maisha.

Hapa nataka nitoe ushauri kwa ndugu zangu usikae na jamii ambayo hamuendani kipato. Kama we ni maskini ukae na matajiri kama we ni tajiri usikae mtaa wa maskini watakunyonya damu.

Uvuvi ulifanyika kama kawaida, mrembo aliyesababisha nihamie hii nyumba aliolewa na maisha yakaendelea.

Ujumbe usifanye maamuzi makubwa kwa kumfurahisha mwanamke lolote linaweza kutokea.

Namba 12.

Nyumba hii ilikua ndani ndani na bei yake ilikua nafuu sana. Hii nyumba mazingira yake hayakua mazuri na maji walikua wanayafata mbali. Nilimpangishia mzazi mwenzangu. Alikaa kwenye hiyo nyumba hadi binti mmoja kwenye nyumba ya wapangaji kupatwa na mapepo hali iliyofanya mama la mama akimbie nyumba kwa hofu ya mtoto kuchukuliwa.

Namba 13.

Hii ilikua na vyumba 8 choo kimoja ambacho pia kilikua bafu baada ya bafu kuziba. Chooni nilikua naamka saa 11 ili niwahi kuoga.

Namba 14.

Hapa palikua pazuri ila kuna changamoto ya maji na umeme. Nyumba haina maji ingawa mabomba yapo kama kawaida. Umeme upo ila kuna hitilafu kwenye wiring. Wapangaji walikua wagumu kulipa bili, maji tulikatiwa maana walikua hawalipi bili ya maji. Niliongea na mwenye nyumba kuhusu maji akanionesha kisima cha maji ya chumvi kama maziwa alichochimba ili tuwe tunatumia. Nikasubiri kodi iishe nikasepa.

Namba 15.

Hapa mwenye nyumba yuko poa sana. Kama kuna changamoto anarekebisha haraka sana, kama hana pesa anakwambia rekebisha nitakulipa na analipa kwa wakati. Sijawaza kuondoka kabisa.

Ni muda muafaka nipambanie kwangu.
 
Umeishi nyumba nyingi mno. Hata hapo utahama.
 
Back
Top Bottom