Nyumba yetu kila siku inafagiliwa tu lakini haipigwi deki

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,691
149,912
Hii nyumba jamani ni chafu ila tuliemuajiri kufanya usafi sidhani kama kweli anapenda usafi na kuchukia uchafu ndio maana kila siku kazi yake imekuwa ni kufagia tu lakini kupiga deki nyumba ing'ae hataki na sijui kwanini.Yaani hata fagio lenyewe anaangalia ni wapi alipitishe kwingine anapotezea!

Ukikagua hii nyumba utakuta chini ya makochi,kwenye uvungu wa vitanda, nyuma ya milongo,n.k kumejaa,vumbi na mende walionenepeana utazani wanaishi peponi kitu ambacho hakikubaliki hata kidogo.

Anapitisha fagio juu juu tu anaacha uchafu mwingi na kudeki ndio kabisa amegoma.Hii sio fair kabisa jamani na sisi wenye nyumba ndio tuko hatarini kupata maradhi kisa tu mtumishi wetu ameamua kulipua kazi yake ya kufanya usafi kwa kuifanya nusunusu.

Mimi nafikiri mkataba wake ukiishi tuajiri muhudumu mwingine atakaeweza kuihudumia nyumba yetu vizuri zaidi kwa viwango vya kuridhisha ili hata majirani zetu waitamani badala ya kila siku kutucheka.
 
Back
Top Bottom