Nyumba yangu inapigwa mnada na NMB

Degelingi_One

Member
Nov 17, 2018
72
121
Habari wakuu humu ndani.

Mimi ni mfanyakazi wa serikali nipo Dodoma kikazi. Nina nyumba yangu mkoani Iringa.

Baba alishawahi kuchukulia mkopo katika bank ya NMB. Leo wakati natoka kazini nimepigiwa simu na mpangaji wangu kuwa nmb wamefika nyumbani na kuchora tangazo "Nyumba inauzwa".

Jamaani wataalamu wa mambo haya naomba ushauri nifanyaje?

Natanguliza shukrani
 
Mwambie baba alipe deni la mkopo, lakini wewe kwanini umruhusu achukulie mkopo nyumba yako?
 
NyitalaNB,
Dawa ya deni ni kulipa kwa nn hukukopa kutumia mshahara wako ukampa baba ako fedha mkadaiana wenyewe?kumbuka fedha haina undugu dingi kashindwa rejesho maumivu unayapata wewe
 
Dawa ya deni ni kulipa kwa nn hukukopa kutumia mshahara wako ukampa baba ako fedha mkadaiana wenyewe?kumbuka fedha haina undugu dingi kashindwa rejesho maumivu unayapata wewe
Hivi mkuu nikikopa kwa kutumia mshahara wangu kisha nikaacha kazi ghafla huwa inakuaje?
 
Nenda mahakamani chukua zuio la mahakamani. Wakati kesi inaunguruma na nyie mnapambana kulipa deni. Yaani zuio la mahakama ni kwa ajili ya ku buy time tuu wakati mnajipanga kulipa
It's almost about 7M. Kwa haraka haraka niliwaza kuwauzia CRDB hili Deni ili nianze kukatwa kwenye mshara wangu. Nawaza kufanya hivi coz mshua Mambo Ni mabaya mno kwake
 
hilo
Mie nmb walitangaza nyumba access bank wakatangaza magari ila nikasolve kwa zuio la mahakama na leo nipo huru nimelipa kote na nimepumzika mikopo kwa miaka mitatu sasa. Na sina mpango wa kukopa mpaka mambo yakae vzr
ulitoa zuio kwa kutumia sababu zipi?
 
It's almost about 7M. Kwa haraka haraka niliwaza kuwauzia CRDB hili Deni ili nianze kukatwa kwenye mshara wangu. Nawaza kufanya hivi coz mshua Mambo Ni mabaya mno kwake
Kumbe una solution tayari, fanya huu uamuzi umalizie deni la watu. Au nenda NMB Uhamishe deni kwako.

Mahakamani utaenda kwa grounds zipi kama mkopo ni halali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom