Nyumba yangu iliyo Mbezi Lous ina changamoto ya nyufa

Rwebo

JF-Expert Member
Oct 17, 2015
973
1,135
Wakuu nyumba yangu ina changamoto ya cracks za mara kwa mara nyingine zinakuwa perpendicular nyingi diagonal. Udongo wa hapa ni clay (mfinyanzi).

Nataka kushusha ukuta wote naomba ushauri wenu wataalamu jinsi ya kutibu tatizo hili.
 
Wakuu njumba yangu ina changa moto ya cracks za mara kwa mara nyingine zina kuwa perpendicular nyingi diagonal. Udongo wa hapa ni clay (mfinyanzi). Nataka kushusha ukuta wote naomba ushauri wenu wataalamu jinsi ya kutibu tatizo hili.
Kuna kosa ulifanya wakati wa kujenga msingi. Ambacho ulitakiwa kufanya baada ya kuchimba msingi ungeweka mchanga kama 4" kisha ndipo umwage zege la 3" na nondo. Baada ya hapo ungejenga msingi wako na baada ya kumaliza msingi usirudishe ule udongo uliotoa bali rudishia mchanga pande zote ndani na nje.

Pia hata kwenye vyumba toa udongo wote weka mchanga. toa usawa wa futi moja na nusu kwenda chini

problem solved
 
Kuna kosa ulifanya wakati wa kujenga msingi. Ambacho ulitakiwa kufanya baada ya kuchimba msingi ungeweka mchanga kama 4" kisha ndipo umwage zege la 3" na nondo. Baada ya hapo ungejenga msingi wako na baada ya kumaliza msingi usirudishe ule udongo uliotoa bali rudishia mchanga pande zote ndani na nje...
Kama ulijengs msingi kwa mawe lazima ipasuke, ila unapomaliza kujenga msingi funga renta, bila kusahau ukianza kujenga tofali chini mwaga zege nchi 3, na baada ya msingi km pesa inaruhusu weka pvc, baada ya madirisha weka renta na renta ya juu so nyumba itakuwa na renta 3 nakuahidi nyumba haitachanika hata crack moja
 
Kama udongo ni 'black cotton soil' si ni kwamba mlipaswa au Fundi alipaswa kujua cha kufanya?.

Maana hiyo type ya udongo ina namna yake ya kipekee ya ku deal nayo tofauti na aina nyingine za udongo.

Sasa je mlifanya yote yanayohitajika na bado nyufa zinatokea au mlijenga kama tu wanapojenga kwingine?.
 
Kama udongo ni 'black cotton soil' si ni kwamba mlipaswa au Fundi alipaswa kujua cha kufanya?.

Maana hiyo type ya udongo in namna yake ya kipekee ya ku deal nayo tofauti na aina nyingine za udongo.

Sasa je mlifanya yote yanayohitajika na bado nyufa zuinatokea au mlijenga kama tu wanapojenga kwingine?.
Ni muhimu kumshauri namna ya kulikabiri tatizo kwa sasa
 
Wakuu njumba yangu ina changa moto ya cracks za mara kwa mara nyingine zina kuwa perpendicular nyingi diagonal. Udongo wa hapa ni clay (mfinyanzi).

Nataka kushusha ukuta wote naomba ushauri wenu wataalamu jinsi ya kutibu tatizo hili.
Vema ukaweka na picha
 
Ni muhimu kumshauri namna ya kulikabiri tatizo kwa sasa
Mimi si Mtaalamu wa Ujenzi ila nafahamu tabia za udongo huo.

Nilichotaka ni aeleze kama walifanya taratibu zote kama inavyotakikana na bado nyumba inapasuka ili Mafundi waone namna nyingine ya kuangalia uwezekano wa tatizo....kwani kama walijenga tu kwa taratibu za kawaida basi ushauri waweza kuwa ni kuzingatia tu kanuni za kujenga kwenye udongo wa aina hiyo.

Au la huenda hapo kuna tatizo la ziada linayohitaji mbinu na Utaalamu wa ziada.
 
Ukweli walijenga kwa taratibu za kawaida tu
 
Kuna kosa ulifanya wakati wa kujenga msingi. Ambacho ulitakiwa kufanya baada ya kuchimba msingi ungeweka mchanga kama 4" kisha ndipo umwage zege la 3" na nondo. Baada ya hapo ungejenga msingi wako na baada ya kumaliza msingi usirudishe ule udongo uliotoa bali rudishia mchanga pande zote ndani na nje.

Pia hata kwenye vyumba toa udongo wote weka mchanga. toa usawa wa futi moja na nusu kwenda chini

problem solved
Kwahiyo msingi uchimbwe futi ngapi?
 
Umemaliza kila kitu hapa👏👏 fundi wake alikosea kutokea kwenye msingi alipoona udongo ni mfinyanzi alitakiwa kwanza kufanya stabilazation ya soil .Nyufa anazoziona ni matokeo ya soil kushindwa kuimili uzito wa jengo husika kwa maana udongo mfinyanzi unaleast load bearing capacity .Ushauli ni kuangusha ukuta mzima na kuanza upya jwa kufuata njia aliyotoa boss apa .Nyumba iko kwenye msingi
 
Kuna kosa ulifanya wakati wa kujenga msingi. Ambacho ulitakiwa kufanya baada ya kuchimba msingi ungeweka mchanga kama 4" kisha ndipo umwage zege la 3" na nondo. Baada ya hapo ungejenga msingi wako na baada ya kumaliza msingi usirudishe ule udongo uliotoa bali rudishia mchanga pande zote ndani na nje.

Pia hata kwenye vyumba toa udongo wote weka mchanga. toa usawa wa futi moja na nusu kwenda chini

problem solved
Mleta mada kama una uwezo vunja nyumba nzima ufuate ushauri huu.
 
Na lile jengo la stand pale mbez ndo lipo juu ya mfinyanz kabisa asee
 
Kuna kosa ulifanya wakati wa kujenga msingi. Ambacho ulitakiwa kufanya baada ya kuchimba msingi ungeweka mchanga kama 4" kisha ndipo umwage zege la 3" na nondo. Baada ya hapo ungejenga msingi wako na baada ya kumaliza msingi usirudishe ule udongo uliotoa bali rudishia mchanga pande zote ndani na nje.

Pia hata kwenye vyumba toa udongo wote weka mchanga. toa usawa wa futi moja na nusu kwenda chini

problem solved
Yote hayo hutegemeana na aina ya udongo wa sehemu husika, mafundi wengi wanapopewa site huanza kujenga tu bila kujua wanajenga juu ya udongo wa ana gani.

NB : PVC husaidia sana kupunguza suala ya nyufa kwenye nyumba.
 
Na lile jengo la stand pale mbez ndo lipo juu ya mfinyanz kabisa asee
Na siku zote mfinyanzi hauna uwezo wa kubeba uzito wa nyumba kwa muda mrefu bila kunifanyia stabilization, hasa wakati wa mvua unapopatwa na kiwango kikubwa cha maji.

Nyufa ni lazima hapo.
 
Wakuu nyumba yangu ina changamoto ya cracks za mara kwa mara nyingine zinakuwa perpendicular nyingi diagonal.
Watanzania tulikubaliana ili kumuenzi Rais wetu JPM, tusiwe tunaita nyufa bali expansion joints. Anzia hapo
 
Back
Top Bottom