Linapokuja suala la uwajibikaji kwenye utekelezaji wa maamuzi yoyote ya baraza la mawaziri, then uamuzi huo unatumia kanuni ya a collective responsibility, hapa Magufuli alikuwa ni mtekelezaji tuu na alitimiza wajibu wake kikamilifu.
P
..naomba kutofautiana na wewe.
..Collective responsibility maana yake ni kuwa waziri hawezi kupingana na uamuzi wa baraza huku akiendelea kushika nafasi yake.
..haimaanishi kwamba akitekeleza uamuzi fulani na ukaliletea taifa hasara hatastahili lawama au hatawajibika.
..Na maamuzi ya baraza la mawaziri hutokana na mapendekezo ya waziri husika ktk kikao cha baraza na mawaziri.
..Na cabinet ikiamua, na waziri mhusika akakubali kutekeleza, mambo yakienda mrama.waziri hawezi kukwepa lawama kwa kudai ulikuwa ni uamuzi wa baraza.
..Pia baraza la mawaziri likiamua, na waziri husika akatekeleza, na matokeo yakawa mazuri, waziri mhusika hupewa kongole. Hatuwezi kumnyima sifa na badala yake tukalipongeza baraza la mawaziri.
..Mwisho, suala hili ni sawa na Polisi aliyefyatua risasi na ikaua raia asiye na hatia. Utetezi kwamba aliamriwa na kamanda wake hautoshi kumuepusha na hatia.