Nyumba ya Sanaa inabomolewa!

Shomari

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,112
241
Kua habari zinazoendelea huko facebook kubomolewa kwa Nyumba ya Sanaa, Je kuna mtu anayefahamu suala hili kiundani atujuze, kama kama inabomolewa kweli ni hatua gani zinazochukuliwa na wanaharakati kuzuia ubomoaji?, huu ni muda wa Wasanii kuungana pamoja na kuonyesha mshikamano katika hili.
 
Niliwahi kuona barua iliyotumwa kwa rais kwa dispach ambayo wasanii walisign kumwomba aingilie kati kuzuia uvunjwaji wake. lakini kama kawaida Kikwete msikivu hakuwa na muda wa kilio cha wasanii.
ndo maana hajawapangia wizara itakayoshughulikia ishu zao.

Barua ilipelekwa last month naambiwa ikapokelewa. na wasanii walituma nakala kwenye balozi za nchi zilizojenga nyumba ya sanaa.

Inaonesha kuna watu Ikulu wanafaidika na kuuzwa kwa nyumba ya Sanaa
 
pale itajendwa benk, si mwajua huu ni bank street
unajua unachokiongea wewe au unashabikia usilolijua???
Unajua nyumba ya sanaa imeanzaje mpaka kufika pale?? unajua kadhia iliyopelekea mvurugano wa sasa??
au unadhani bank ni bora kuliko heritage??? ile ni icon ya taifa.

au tuseme kwamba na movenpick itavunjwa kupisha ujenzi wa bank??? kama nchi nzima ikijaa banks unadhani wananchi watapata wapi pesa za kuweka kwenye bank? siyo kila mtu ni mkulima wala m-beba mabox. ajira zinatofautiana ila twatumia currency moja kwa malipo na makusanyo halali.

FYI
pale wanapavunja kujenga hotel appartments and bussiness centre. hiyo bank haipo kwenye plan.

Waza fikra sahihi wewe

Kua habari zinazoendelea huko facebook kubomolewa kwa Nyumba ya Sanaa, Je kuna mtu anayefahamu suala hili kiundani atujuze, kama kama inabomolewa kweli ni hatua gani zinazochukuliwa na wanaharakati kuzuia ubomoaji?, huu ni muda wa Wasanii kuungana pamoja na kuonyesha mshikamano katika hili.

Ni kweli pale panavunjwa na panajengwa MAKAO MAKUU YA BENKI YA NMB. Na wamefuata taratibu zote na wala hakuna ufisadi wowote ulio fanyika pale mkuu
 
pale itajendwa benk, si mwajua huu ni bank street

Nyumba ya sanaa inapigwa nyundo na pale panajengwa benki, sitaki kuamini. Jamani hivyo sisi tumelaaniwa such a unique architectural masterpiece going down, with such a noble and just cause for its establishment?????? Hivi Julius akiamka leo mtamwambia nini???? Kainzi kanahitajika hapa, jamani sio bure.

Nyumba ya Sanaa ni duka maalumu kwa ajili ya wasanii wa Tanzania kuonyesha na kuuza kazi zao za sanaa walizobuni wao wenyewe. Mwanzilishi wa Nyumba ya Sanaa ni Sr. Jean Pruitt ambaye ni Sista anayefanya kazi na shirika la Maryknoll sisters chini ya kanisa Katoliki nchini Tanzania.

Historia ya Nyumba ya Sanaa

Nyumba ya Sanaa ilianzia shughuli zake mtaa wa Mansfield uliopo nyuma ya kanisa kuu la Mtakatifu Joseph. Sr. Jean Pruitt alianzisha Nyumba ya sanaa mwaka 1971 pale Mtaa wa Mansfield, baada ya kukusanya vijana na kuanza kufanya kazi za sanaa. Wazo hili la Sr. Jean lilizaa matunda na kazi za sanaa zilizokuwa zinafanywa na vijana kuonekana na jamii pamoja na Taifa. Baada ya kazi zilizokuwa zinafanywa na vijana chini ya Sr. Jean Puitt kuonekana zina manufaaa zaidi kwa Taifa la Tanzania, Nyumba ya Sanaa ilizinduliwa na Mwalimu J.K.Nyerere mwaka 1972 hapo hapo mtaa wa Mansfield. Katika harakati za kuipanua Nyumba ya Sanaa Sr. Jean Pruitt alisaidia kupatikana kwa wafadhili kwa ajili ya kujenga jengo ambalo lingeweza kuchukua wasanii wengi kwani ofisi ya mtaa wa Mansfield ilikuwa ndogo. Mwalimu J.K.Nyerere alitoa kiwanja kilichopo makutano ya barabara za Alli Hassani Mwinyi na Ohio na Nyumba ya Sanaa ikajengwa hapo. Jengo hili jipya la Nyumba ya Sanaa lilianza kujengwa mwaka 1981, na lilizinduliwa rasmi na Mwalimu J.K.Nyerere mwaka 1982. Na mwaka uliofuata Mei 1, 1983 wafanyakazi walihamia jengo hili jipya llilopo Upanga mtaa wa Ohio wakitokea mtaa wa Mansfield. Sr. Jean Pruitt alianzisha Nyumba ya Sanaa kama sehemu ambayo vijana wasanii watabuni na wataonyesha kazi zao za sanaa ili ziweze kutambulika kitaifa na kimataifa na kuziuza ili waweze kuondokana na umasikini. Ndani ya nyumba ya Sanaa maonyesho mbalimbali ya kitamaduni huonyeshwa na ni eneo muhimu ambapo unaweza kuona ngoma mbalimbali za kitamaduni za jamii mbalimbali za Tanzania.
Wasanii Maarufu waliotokana na Nyumba ya Sanaa

Nyumba ya Sanaa imeibua vipaji vya wasanii wengi sana kwa upande wa uchoraji na utengenezaji wa nguo za Batik. Miongoni mwa wasanii maarufu wajulikanao kitaifa na kimataifa walioibuliwa pale Nyumba ya Sanaa ni George Lilanga, Francis Patric Imanjama, Malaba, Ntila n.k

Source: wikipedia
 
Nimemwomba msanii aliyekuwepo nyumba ya sanaa kabla hawajapewa notisi anitumie barua waliyoituma kwa rais. Angalia kwa makini mapendekezo ya wasanii na uzito wa rais kuchukua maamuzi sahihi kwa wakati. Hii serikali yetu ndiyo inayolea wahuni na wahalifu halafu baadae inasema mwananchi do your part wakati yenyewe ni lijibwege mtozeni mkubwa
K.n.y.
WASANII (kada mbalimbali)DAR ES SALAAM
TANZANIA

08/ 08/2010

KWA
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
IKULU
DAR ES SALAAM

YAH: BARUA YA DHARURA KUHUSU HATIMA YA NYUMBA YA SANAA.

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tafadhali rejea kichwa cha habari kwa kumbukumbu ya waraka huu.

sisi ni mjumuiko wa wasanii wa asasi na kada mbalimbali ambazo ni uchoraji, mitindo, ufumaji, paitings, etchings, batik, screen printing, ngoma na sanaa za maonesho. Kwa pamoja tunaleta kilio na maoni yetu kwako, tukiomba busara zako kuingilia kati kuweza kuirejesha Nyumba ya Sanaa katika mikono salama kwa manufaa ya wasanii, vijana, wanawake na wasiojiweza.

Nyumba ya Sanaa ilianzishwa mnamo 1972 kwa madhumuni ya kutoa mafunzo ya sanaa kwa vijana, wanawake na wasiojiweza pamoja na kutafuta masoko ya sanaa na kazi za mikono. Mnamo mwaka 1983 serikali ya Norway kupitia shirika lake la NOVIB waliikamilisha ujenzi wa jengo la sasa la Nyumba ya Sanaa baada ya wasanii kupewa kiwanja kutoka kwa Baba wa Taifa Mwalimu, J. K. Nyerere katika kuunga mkono juhudi na malengo ya taasisi ambapo aliweka jiwe la msingi la Nyumba ya Sanaa. Katika kipindi chote hadi kufikia mwaka 1998 kulikuwa na mshikamano na ushirikiano mzuri kati ya menejimenti na wafaidika wa Nyumba ya Sanaa.

Mheshimiwa Rais, Tangu mwaka 1998 kumekuwepo na kutoelewana baina ya Bodi ya wadhamini baada ya kutiliana shaka wenyewe kwa wenyewe, pia kati ya Bodi ya Wadhamini na Wanachama waanzilishi wa Nyumba ya Sanaa. Matokeo ya ugomvi huo ni pamoja na kuasisiwa kwa shirika la Dogodogo Centre baada ya kumeguliwa kutoka Nyumba ya Sanaa. Hali ya kutoelewana na kutoaminiana ilidumu kwa kipindi kirefu licha ya juhudi za Kabidhi Wasii Mkuu kujaribu kusuluhisha bila mafanikio. Matatizo haya yalipelekea ufunguaji wa kesi mahakamani. Tarehe 24 Februari, 2005 Msajili alifuta rasmi usajili wa Bodi ya Wadhamini ya Nyumba ya Sanaa akiwataka wakabidhi mali na shughuli za NYUMBA YA SANAA kwa asasi mbadala. Baada ya hapo Bodi haijawahi kukasimisha amali na majukumu ya Nyumba ya Sanaa kwa asasi mbadala, lakini Bodi imeendelea kuwepo chini ya Uenyekiti wa ndugu Alipo Atunkolepo (Wakili wa kujitegemea). Hali hiyo imepelekea Nyumba ya Sanaa kuendeshwa kama kampuni binafsi kwa faida ya wajumbe wachache wa Bodi ambao ni ndugu Alipo Atunkolepo ( Mwenyekiti), S. J. Ntomola (Mjumbe), B. P. Lyimo (Mjumbe) na Josephat Rweyemamu (Mjumbe).

Sisi wasanii kwa nyakati tofauti tulifanya juhudi kuwasilisha kilio chetu kwa maofisa mbalimbali serikalini akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo ambaye alimpa jukumu Mkrugenzi wa Utamaduni la kufuatilia suala la Nyumba ya Sanaa lakini tangu mwaka 2007 mpaka sasa hatujaona mwelekeo wa kulipatia ufumbuzi.

Mheshimiwa Rais, Kuanzia kufutwa kwa Nyumba ya Sanaa mwaka 2005 mpaka sasa kumekuwepo na kasi ya kubadili mwelekeo wa malengo, mtazamo, usimamizi na usalama wa mali za iliyokuwa taasisi ya Nyumba ya Sanaa. Sehemu kubwa ya jengo lililojengwa kwa msaada wa serikali ya Norway, imepangishwa kwa wafanyabiashara mbalimbali, pia kumekuwepo majaribio kadhaa ya kupata mkopo benki kwa udhamini wa majengo ya Nyumba ya Sanaa, lakini mnamo hivi karibuni, Mwenyekiti Alipo na baadhi ya wajumbe wake wamefanikiwa kupata mwekezaji ambaye wameshaingia ubia kimkataba, katika utekelezaji wa mkataba huu ni kujenga jengo la ghorofa katika eneo lenye jengo la sasa. Ikichukuliwa kwamba mwekezaji atapaswa kulivunja au kubadilisha mfumo wa jengo liweze kujengwa la ghorofa.

Mheshimiwa Rais, tunaandika waraka huu kwako kwa kuwa mwekezaji ameshaanza hatua za awali katika ujenzi wa ghorofa hiyo kwa kuwapa NOTISI wapangaji wote wakiwemo wasanii wachache waliosalia Nyumba ya Sanaa kuhama na kupisha ujenzi. Notisi hiyo haioneshi hatima ya sanaa na wasanii baada ya ujenzi wa jengo hilo.

Madhumuni yetu

Mheshimiwa Rais, Kwakuwa Nyumba ya Sanaa iliimarishwa kwa juhudi za kujitolea kati ya waanzilishi, serikali ya Norway (kujenga kituo) na serikali ya Tanzania chini ya dhamira ya dhati ya marehemu Baba wa Taifa ili kukuza na kuendeleza sanaa na masoko nchini. Ichukuliwe kwamba Nyumba ya Sanaa ilikuwa inaendeshwa na Bodi Huru lakini kwa manufaa ya wasanii na wazalishaji wa Tanzania. Sisi wasanii tunaamini kwamba:-

  • Nyumba ya Sanaa kuendelea kuwa chini ya Bodi iliyofutwa ni kuwanyima fursa wasanii, vijana, wanawake na wasiojiweza kuendeleza vipaji vyao, kwani kumekuwa hakuna uhusiano wala ushirikishwaji tena wa wasanii katika maamuzi ya hatima ya Nyumba ya Sanaa. Tangu kufutwa kwa Nyumba ya sanaa mwaka 2005 hakujawahi kuitishwa au taarifa kwa wasanii walengwa kuhusu maendeleo au mabadiliko ya asasi.
  • Kutokana na kukosa usimamizi sahihi wa dira ya Nyumba ya Sanaa, imepelekea usitishwaji wa shughuli zote za mafunzo na uzalishaji kutokana na maeneo ya shughuli hizo kupangishwa wafanyabiashara wa kawaida.
  • Kitendo cha Bodi iliyofutwa kuendelea kusimamia mali za asasi ni kumaliza tumaini dogo lililobaki katika kutoa nafasi kwa makundi-lengwa kwa mujibu wa uanzishwaji wake.
  • Kwa kuwa jengo la sasa la Nyumba ya Sanaa lilijengwa kwa umakini mkubwa na baadhi ya kazi za wasanii nguli wa Tanzania ambao ni Ndugu Robino Ntila, Augustino Malaba na Marehemu Lilanga (Mungu amlaze pema), kazi za wasanii hawa katika umaliziaji wa ujenzi umelifanya jengo kuwa ARTFACT ambayo naamini vizazi vijavyo watatumia kama alama ya utalii. Hivyo ujenzi wowote utaondoa taswira nzuri ya kuvutia ya Nyumba ya Sanaa.
  • Nyumba ya Sanaa ilikuwa ni mlango wa masoko ya sanaa na kazi za mikono, hivyo kutokuwepo kwake inakwamisha juhudi za wazalishaji kazi za sanaa wa Tanzania kuweza kushiriki vyema masoko na hasa soko la pamoja la Afrika Mashariki.
  • Hivi sasa Nyumba ya Sanaa inanufaisha wachache ambao si walengwa waliokusudiwa. Tunafahamu kwamba wanufaika hawa hawana rekodi ya uwekezaji katika Nyumba ya Sanaa, hivyo wanavuna matunda yaliyopandwa na wengine hasa kupitia ushirikiano mwema baina ya serikali ya Tanzania (kupitia Ikulu) na Norway (kupitia shirika la NOVIB).

Mheshimiwa rais, tunaleta kwako kilio chetu tukiambatanisha mapendekezo kadhaa:-

·Nyumba ya Sanaa irudishwe serikalini kwa mdhamini mkuu wa serikali ili mchakato wa uanzishwaji wa Bodi huru kuisimamia malengo yake. Uhuishaji wa Nyumba ya Sanaa itachangia sana kuongeza ajira na pato la taifa hivyo kupunguza tatizo la uzururaji na kilio cha masoko ya sanaa.

·Kutokana na maduka binafsi ya kazi za sanaa kufungwa jijini Dar es Salaam, imepelekea wasanii wengi kukosa fursa ya kuonesha na kuuza kazi zao za sanaa, pia watalii wamekosa eneo la kununua sanaa-mseto za Tanzania. Sanaa hizi zimekuwa pia zinakusanywa kutoka mikoa yote ya Tanzania.

·Kwa kuwa tangu kufutwa kwake mnamo mwaka 2005, Nyumba ya Sanaa imeendelea kufanya biashara pamoja na kuingia mikataba ya biashara mpaka sasa 2010, tunaomba serikali yako itathmini na ilipwe kodi kutokana na faida ya biashara zilizoendeshwa mara baada ya kusitishwa uendeshaji wake.

·Tunakuomba usitishe uvunjwaji wa jengo lililopo sasa, kwani ni utalii na alama ya taifa kuonesha serikali za Norway na Tanzania zilivyothamini juhudi za wasanii na wazalishaji kujikwamua kiuchumi na kuchangia pato la Taifa.

·Tumeambatanisha na barua ya notisi iliyotolewa kwa watumiaji wote wa jengo la sasa la Nyumba ya Sanaa.

·Nyumba ya sanaa ifufuliwe upya bila kubadili malengo bali kuyaboresha.

Mheshimiwa rais, kwa moyo mkunjufu, tunaamini kwamba wewe na serikali yako ni sikivu na mnatupenda kwa dhati mkiwa na nia ya kutupatia kila aina ya msaada ili tuweze kuchangia pato la taifa kama kada nyingine za jamii.

Mheshimiwa rais, tunafahamu kwamba waraka huu wa dharura umekufikia huku ukiwa katika kipindi cha uchaguzi mkuu. Tunaamini kwamba utatafakari ombi letu na kuamua kwa hekima.

Kwa heshima na taadhima tunaambatanisha majina na saini zetu kuunga mkono barua hii.

Nakala kwa:-
  1. Balozi wa Norway Tanzania
  2. UNESCO Tanzania
  3. Kabidhi Wasii Mkuu
  4. Bunge
 
Kwa upande wa wamasai ukienda Ngorongoro kuna "Boma" ambako huonyesha tamaduni za kimasau. Ukibahatika kwenda Haydom kuna Four Corners Cultural Centre inajengwa. Ni wakati muafaka wachaga wakajenga cultural centre yao kule uchagani, wahaya kule Bukoba, Wangoni kule Songea, Wanyakysua kule Mbeya nk. Tatizo ni kwamba siyo maeneo yote yanayotembelewa na wageni.

Ushauri
Dodoma kwa sasa ni eneo linalofikiwa sana na wageni ni wakati muafaka wa kuhifadhi na kudumisha tamaduni za makabila yetu. Kwa waliowahi kwenda Africa Kusini watakubaliana na mimi kuwa mila zao wanazitumia kama kivutio cha kuingiza fedha za kigeni, nasi tukafanye hivyo pale Dodoma.
 
Attachments

  • IMGP1636.JPG
    IMGP1636.JPG
    117.3 KB · Views: 120
Nimemwomba msanii aliyekuwepo nyumba ya sanaa kabla hawajapewa notisi anitumie barua waliyoituma kwa rais. Angalia kwa makini mapendekezo ya wasanii na uzito wa rais kuchukua maamuzi sahihi kwa wakati. Hii serikali yetu ndiyo inayolea wahuni na wahalifu halafu baadae inasema mwananchi do your part wakati yenyewe ni lijibwege mtozeni mkubwa
ooh very sorry msanii, na wasanii wote kwa ujumla!
ndivyo tulivyo cc bwana.
 
Wasanii hawana imani tena na serikali ya kikwete.
I dare to say hajui vipaumbele vya taifa zaidi ya kutaka kuongoza tu
 
kuna vitu vinanikeraga sana, eti preserve nyumba ya sanaa for heritage, usiweke mradi wa umeme kihansi, utaua vyura, usipitishe barabara kandokando ya serengeti, utabughudhi wanyama......usipofikiria sana utagundua wazungu wanatuona sisi waafrika kama makumbusho flani hata mahitaji yetu ya kibinadamu yanapimwa katika mtazamo huo.. vunja weka vitu vya maana hao vyura wa kihansi waite wazungu wakaweke huko kwao sisi tunao wakutosha, na hiyo nyumba ya sanaa inafaida gani kwa mtanzania wa kawaida?vitu vyote vinapatikana slipway,makumbusho,bagamoyo hakuna sababu ya kuwa nazo kama uyoga kila sehemu.
 
Nyumba ya sanaa ni mfano mdogo tu wa wasanii wa Tanzania wanavyopunjwa na kunyoywa jasho lao, Tingatinga ni kundi lingine. Serikali haiwajali hata kidogo, ndio maana wanasota wakichora morogoro store, wakichonga mwenge lakini hakuna wanachopata.

Kwa mfano majuzi picha moja ya Tingatinga imeuzwa US $ 54,000 lakini aliyechora na au warithi wake hawakuambulia chochote pamoja na kuwa Tanzania imesaini mkataba wa Berne wa kutunza haki za wasanii, Kipengere cha droit de suite kingeweza kumsaidia, lakini kwa jinsi wasanii walivyopuuzwa serikali wala haioni umuhimu wa kuingiza hii kitu kwenye sheria zetu kama mkataba wa berne unavyotaka, ili kuwafanya wasanii wafaidike na kazi zao kupitia hii droite de suite. Tanzania iliridhia mkataba huu Julai 1994 na mpaka leo mika 16 baadaye hakuna kilichofanyika.

Kwa misingi hiyo sintoshangaa kama hiyo barua ya wasanii kwenda kwa raisi itakaa bila kujibiwa na jengo hilo likaangushwa.
 
Wasanii hawana imani tena na serikali ya kikwete.
I dare to say hajui vipaumbele vya taifa zaidi ya kutaka kuongoza tu

Msanii naomba uqualify statement yako, Isipokuwa wa bongo fleva, hiyo kwa tanzania ndio sanaa kuchonga na kuchora ni ubangaizaji to
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Nasikia ati ilikuwa haina hata hati....Mwalimu alitoa ardhi kama ya kijijini....hata pale AMREF ni barabara lakini Mwalimu aliruhusu wajenge...nao hawana hati lakini kuna wajanja wanahati ya sehemu hizo zote mbili na wanakopea Benki
 
Wasanii hawana imani tena na serikali ya kikwete.
I dare to say hajui vipaumbele vya taifa zaidi ya kutaka kuongoza tu

Duuh..Ndio maana anapenda sana kujiweka karibu na wasanii kumbe pia anawasanii kiaina, hii inanikumbusha alhaji Mwinyi alivyojaribu kuuza ile Rolls Royce ya kwanza pale Ikulu magogoni lakini bahati aliweza kutumia busara na kuahirisha biashara ile (Nafikiri mchonga aliingilia kati)
 
kuna vitu vinanikeraga sana, eti preserve nyumba ya sanaa for heritage, usiweke mradi wa umeme kihansi, utaua vyura, usipitishe barabara kandokando ya serengeti, utabughudhi wanyama......usipofikiria sana utagundua wazungu wanatuona sisi waafrika kama makumbusho flani hata mahitaji yetu ya kibinadamu yanapimwa katika mtazamo huo.. vunja weka vitu vya maana hao vyura wa kihansi waite wazungu wakaweke huko kwao sisi tunao wakutosha, na hiyo nyumba ya sanaa inafaida gani kwa mtanzania wa kawaida?vitu vyote vinapatikana slipway,makumbusho,bagamoyo hakuna sababu ya kuwa nazo kama uyoga kila sehemu.
kweli unauwezo mkubwa wakufikili wewe!? kwa taarifa yako hata hao unaowafagilia wanakumbukumbu zao!
 
Dar City Centre Dar Tower

The Dar Tower is to be constructed on 1-acre plot located next to Movenpick Hotel, a well known five-star hotel. It is a corner plot bordered by two main roads on two sides and an exclusive golf course club, Gym Khana, on the other. A number high rise towers are currently built in the proximity of the site.

For example, another 25-floor building is now constructed on the former Red Cross site across the road while a similar tower to be known as Uhuru tower is being built just 250 meters away. The more established towers in the area include Barlcays House, the head office of Barclays Bank, the PPF tower owned by the Parastatal Pension Fund but used by number of banks and international organizations. A number of other high-profile companies and government agencies are located nearby, which explains why the demand for commercial and residential accommodation in the area is very high.

The proposed Dar Tower is a 25-floor mixed-use development with one level underground parking. The ground floor and mezzanine will be used for retail purposes. This will be followed by 10 floors of office space and 10 floors of residential. There will be gym with a swimming pools and coffees shops as wells. The Dar Tower is designed to serve the business community who would like to take apartments and office in the same place.

The residents of Dar es Salaam can understand the importance of having all these amenities in one place at the city centre. Traffic congestion and heat are major problems in Dar, therefore having all your working and an amenity in one air-conditioned place is a major advantage for the business community. With a five-star hotel and a golf course next door, and all other banking, commercial and government offices within a walking distance, the Dar Tower is designed to provide an idyllic atmosphere to work, live and entertain. This plot is highly sought-after by companies and wealthy individuals who all competed with IPIT to own it.

Promoters
The Dar Tower is promoted by a group of experienced businessmen and international institutions with track record of initiating and successfully completing development projects in Europe, Arabia and Africa. These promoters are listed below:

  • Integrated Property Investments Ltd, UK.
  • Russell Woods / Saudi Binladen Group (SBG), UK, Saudi Arabia
  • Permal Hedge Fund, NY, USA
  • Sheikh Yusuf Al Hajiri and Sons, Kuwait
  • Former IMF Country Director,
  • Others
Need we say more????????????
 
Hicho ndicho nikijuacho na mimi pia.
Ahsante sana mkuu. umeenda maili mbili mbele yangu.
Wahuni hawa we waache tu, wataishia gerezani punde
 
Nimepitia mawazo yote mpaka muda huu sijaona sehemu ambayo inahusisha nyumba ya sanaa na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA)...nimechanganyikiwa naomba msaada kabla ya kuendelea. Naomba kujua uhusiano uliopo katika ya hivyo vitu viwili, BASATA wanasemaje kuhusu issue hii yote. Na hawa wasanii sioni sehemu kuonyesha barua yao ilikuwa na baraka za BASATA....Naomba kuwasilisha.

Cha kuongezea soma hii link ifuatayo kuhusu huo mradi na share za wamiliki wa nyumba ya sanaa katika huo mradi, ni juu yako kuverify integrity ya hiyo website.

City Tower Morabaha Offer | Ipi Ltd | Property Investments Specialists | UK

Back
Top Bottom