Nyumba ya Mwalimu Mkuu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,082
Hii ni nyumba anamoishi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lihumbe iliyopo kata ya Mbagamao, wilayani Mbinga mkoani Ruvuma, Bw. Osmundi Nombo na mwalimu mwenzake. (Picha na Grace Michael).

Pamoja na kuwa tuna utajiri mkubwa wa dhahabu, almasi, gas, Tanzanite miti ya aina mbali mbali lakini tunashindwa kuwathamini Walimu wetu kwa kuwajengea nyumba zenye hadhi na kazi zao. Wakati mafisadi, wala rushwa na viongozi waroho wa utajiri wa haraka haraka wanakuwa mabilionea kwa speed kali sana, lakini hivi ndivyo wanavyoishi Watanzania wengi wakiwemo walimu. Baada ya miaka 47 ya uhuru kuwa na walimu wanaoishi katika nyumba kama hii ni aibu ya hali ya juu.
 
Kwani ndugu yangu bubu hujui kuwa walimu ndiyo wanyonge wa nchi hii?
Haki ya walimu imepuuzwa kwa kile ambacho naweza kusema kinachangiwa na waalimu wenyewe. Ni kwa muda mrefu waalimu wamekuwa wakitumika kama jumuia ya chama tawala. Serikali imekalia mawazo yao kwa kiwango cha wao kutokusimama kidete kupigania mazingira bora ya kazi.
Wakati wafanyakazi wengine wakiombwa kwa hiari kuchangia shughuli za maendeleo kwa waalimu hakuna mjadala unapewa salary slip unakuta pesa ilishakatwa tena kwa kiwango walichopanga wao.
Waalimu ndiyo hasa wanajua siri za uchaguzi. Wamekuwa wakichukuliwa kusimamia upigaji kura. Huko vijijini walimu ndiyo wanadi wakubwa wa sera za chama tawala na siku zote wao ndiyo upelekea chama tawala kukaa madarakani tokana na heshima ambayo jamii hususani ya vijijini uwapatia kiasi cha kuwasikiliza wao. Sheria haimruhusu mtumishi wa umma kushiriki katika shughuli za kisiasa kwa maana ya kuwa nutral lakini waalimu, Mungu wangu, urubuniwa na kupewa viposho kisha kusahau hizo nyumba mbofumbofu na kuishawishi jamii kuwachagua hao hao ambao hawajali maslai yao. Na kama kura uibiwa basi waalimu ujua na kuruhusu hayo yatendeke.
Tumekuwa tukiwaonea huruma lakini wao wenyewe ni wanafiki wa nafsi zao. Kama nchi hii tunarudi nyuma ni kutokana na watu wa namna hii.

Hii ni nyumba anamoishi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lihumbe iliyopo kata ya Mbagamao, wilayani Mbinga mkoani Ruvuma, Bw. Osmundi Nombo na mwalimu mwenzake. (Picha na Grace Michael).

Pamoja na kuwa tuna utajiri mkubwa wa dhahabu, almasi, gas, Tanzanite miti ya aina mbali mbali lakini tunashindwa kuwathamini Walimu wetu kwa kuwajengea nyumba zenye hadhi na kazi zao. Wakati mafisadi, wala rushwa na viongozi waroho wa utajiri wa haraka haraka wanakuwa mabilionea kwa speed kali sana, lakini hivi ndivyo wanavyoishi Watanzania wengi wakiwemo walimu. Baada ya miaka 47 ya uhuru kuwa na walimu wanaoishi katika nyumba kama hii ni aibu ya hali ya juu.
 
Mtanisamehe kama itabidi nirudi nyuma na kutoa maoni tofauti kabisa na ya Kichore. Nafikiri jambo la kujiuliza ni kama jamii zinazoishi maeneo yanya mazingira ya ajabu kama hayo ya mwalimu kuishi kwenye kibanda mbofombofu kuliko cha ng'ombe hakuna WATU. Yaani WATU WOTE, pamoja na waliokwisha kwenda shule (ambao baadhi yao hutoa mawazo humu JF)WANAOTOKA MAENEO HAYO WAMEJIKALIA TU!!! Yaani hawawezi kufanya chochote juu ya hali ya waalimu wa watoto wao, wadogo zao, nk hadi chama tawala kiondoke madarakani!!! She!!(samahani mzimu wa kimasai umenipanda!).
Kama suala la unafiki, tusiwatwishe waalimu peke yao. Sote tunaokubali kupewa vikanga, mchele na visenti kidogo wakati wa uchaguzi tu wanafiki, so y single out teachers?
Nakumbuka nilipokuwa najenga kibanda yangu kijijini, walimu wa shule ya pale kitongojini walinieleza tatizo la shule la vyumba vya madarasa na vyoo kwa wanafunzi. Pale wanafunzi walikuwa wakienda haja kwenye mashamba ya jirani, lakini WANAKIJIJI HAWAKUONESHA KUJALI HILO!! Nilianza kuhamasisha wanakijiji wenzangu kwa kutoa lori la mchanga na mifuko kadhaa ya saruji na tukaanza harambee. Nikaenda Dar es Salaam na kuwakamata baadhi ya wasomi na wafanyibiashara waliotoka kijijini kwetu. Mbona baada ya muda mfupi tu madarasa mawili yalijengwa na baadaye shule yetu ikabadilika kabisa?!?
Kwa hiyo naamini tuangalie namna mbadala za kuweza kutatua matatizo kama haya, kwa mfano kukumbushana wajibu wa wasomi, wafanyibiashara n.k. kwa jamii na vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom