Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,900
- 30,235
NYUMBA YA MWALIMU NYERERE MAGOMENI MADUKA SITA 1955
Rafiki yangu kanipatia picha ya nyumba aliyokaa Mwalimu Nyerere Magomeni Maduka Sita.
Mwalimu Nyerere anaonekana nje ya nyumba yake akiingia ndani.
Picha ya nyumba hii nimeitafuta kwa miaka mingi bila mafanikio.
Mwalimu baada ya kutoka UNO mwaka wa 1955 waajiri wake wamishionari hawakuweza kumstahamilia wakamwambia achague siasa au kazi.
Halmashauri Kuu ya TANU chini ya Mwenyekiti wake Clement Mohamed Mtamila ikakutana nyumbani kwa Mzee Mtamila Mtaa wa Kipata na Sikukuu kujadili barua ya Mwalimu Nyerere aliyoandikiwa na mwajiri wake.
Uamuzi ulikuwa Mwalimu aache kazi.
Mwalimu akaacha kazi na kuhamia nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu si mbali sana na nyumba ya Mzee Mtamila.
Inasemekana Mwalimu aliishi na Abdul Sykes kwa miezi mitatu hadi TANU walipomtafutia nyumba hiyo hapo juu Magomeni Maduka Sita.
Nyumba hii haipo hivi sasa kwani ilivunjwa.
Picha hiyo hapo chini ya nyumba ya Mwalimu ni kiwanja ilipokuwa nyumba hii.
Picha hii iliyopigwa tarehe 15 June 2015 inaonyesha kiwanja kimezungushwa mabati kwa ajili ya ujenzi wa ghorofa.
Picha ya mwisho ni nyumba ya Abdul Sykes mbayo Mwalimu Julius Nyerere aliishi kabla ya kuhamia Magomeni.