Nyumba ya Mungu; Bwawa la kuzalisha umeme na samaki linavyowapa somo la uvuvi watu wanaolitegemea

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Wakuu salaam...
Bwawa tajwa hapo limepakana na mikoa miwili ya Kilimanjaro na Manyara. Limegusa wilaya tatu za mikoa hiyo ambazo ni Simanjiro, Mwanga na Moshi DC.

Bwawa hili lililojengwa miaka ya 1970s kwa lengo la kuzalisha umeme, limekuwa tegemeo kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo na wageni mbalimbali.

Ukiachana na uzalishaji wa umeme, bwawa hili pia hutegemewa kwa uvuvi wa samaki watamu aina ya perege, ufugaji pamoja na shughuli za kilimo Cha bustani.

Kwa upande wa umeme hakuna tatizo kwani hadi saivi bwawa hili linazalisha umeme bila shida yoyote.
Tatizo lipo kwenye uvuvi wa samaki. Miaka ya nyuma kidogo kuanzia 2010 kurudi nyuma, bwawa hili lilikuwa na samaki wakubwa Jambo lililopelekea wavuvi na wafanyabiashara wa samaki kujipatia kipato Cha kutosha.
Ilifikia mahali baadhi ya watumishi wa serikali waliacha kazi Serikalini na kufanya biashara ya samaki. Kwa wakati huo utajiri ulikua nje nje.

Sasa balaa limekuja baada ya wavuvi kugundua njia za uvuvi ambazo zimewamaliza wale samaki kwenye bwawa. Kibao kimegeuka moja kwa moja, hakuna samaki wanaoweza kukidhi mahitaji ya wavuvi na familia zao.

Maisha yamekuwa magumu kiasi kwamba wazazi wamekuwa wakiacha watoto kweny majumba ili wao waende kutafuta samaki kwenye mabwawa mengine huko mikoani.

Ni kilio, watu wanajuta...wanajuta kwani wamegundua kuwa hili kaburi walijichimbia wenyewe.
Wewe mfanyabiashara uliyetegemea kutumiwa samaki kutoka nyumba ya Mungu, kuwa mpole na mvumilivu. Huku hakuna samaki tena!

Mjenga nchi ni mwananchi.
 
Mkuu hebu nisaidie jambo hivi ni kweli hakuna mchaga anaehusika na uvuvi kwenye bwawa hilo maana kuna clip inasambaa mitandaoni kuwa wachaga hawavui kabisa samaki kwasababu wao sio utamaduni wao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom