Nyumba ya mbunge mteule Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi yanusurika kuchomwa moto, Salome Makamba asakwa

Kwani nyumbani kwa mbunge mteule hakuna cctv camera? Chunguzeni hizo camera kisha mtoe tamko kuwa waliokamatwa ni hao waliotaka kuchoma hiyo choo ya nje ya Katambi, kama hakuna camera polisi na huyo Katambi wao waache kutufanya wananchi kuwa wajinga kwa kutuaminisha uongo
 
Kwani nyumbani kwa mbunge mteule hakuna cctv camera? Chunguzeni hizo camera kisha mtoe tamko kuwa waliokamatwa ni hao waliotaka kuchoma hiyo choo ya nje ya Katambi, kama hakuna camera polisi na huyo Katambi wao waache kutufanya wananchi kuwa wajinga kwa kutuaminisha uongo
 
Kura zilizopigwa tayari kwa rais na wabunge wa ccm ndani ya mabegi walokutwa nayo maeneo mengi siyo ushahidi tosha?!

You know, election fraud is a crime punishable by law. Kuna watu wamekamatwa wakiwa na hayo mabegi na sasa wako mikononi mwa polisi?

Kumbuka, upo uwezekano wa mpinzani wako kutengeneza fake ballot papers zinazoenesha kura zako ili kujenga mazingira ya kuhoji ushindi wako. Hiyo ni style ya kijasusi!
 
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio la jaribio la kuchoma moto nyumba ya Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi (CCM) iliyopo mtaa wa Ushirika Mjini Shinyanga huku likiwatafuta na kuwakamata Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA Salome Makamba na mdogo wake Timoth Makamba wakihusishwa na tukio hilo.

Akitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari leo Oktoba 30,2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa sita na dakika 45.

“Majira ya saa saba kasorobo, Mbunge Mteule Patrobas Katambi akiwa amelala nyumbani na ndugu zake walisikia kishindo juu ya paa la choo cha nje ambacho kipo katika eneo la uzio wa nyumba hiyo ndipo walipotoka nje na kuona moto ukiwaka juu ya paa la choo pamoja na dumu lenye mafuta aina ya petroli”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

“Wakati wakiendelea kuzima moto huo waliona gari aina ya Toyota Klugger lenye rangi ya silver likikimbiliwa na watu wawili na kisha watu wale waliingia ndani ya gari lile na kutoweka”,amesema Kamanda Magiligimba.

Kamanda Magiligimba amesema baada ya kufanikiwa kuzima moto huo waliona gari lile lile likipita barabara ya lami ya Shinyanga – Mwanza ndipo walipoamua kulifuatilia na dereva wa gari hilo baada ya kugundua anafuatiliwa aliamua kuingia hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na kuliacha gari hilo kisha kukimbia.

“Wakati wa kuwaweka chini ya ulinzi watu hao ilitokea purukushani ndani ya uzio wa hospitali na gari ya polisi iliyokuwa doria ilifika mapema na kufanikiwa kuwakamata watu wawili ambao ni Wilson Mhando Suluti (30) mkazi wa Bugweto na Jackson Raphael Peter (27) mkazi wa Bugweto wakiwa ndani gari hilo lenye namba za usajili T.729 DFP aina ya Toyota Klugger rangi ya Silver mali ya Salome Makamba aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA”,amefafanua Kamanda Magiligimba.

“Ilibainika kuwa watu hao tuliowakamata wao ndiyo waliokuwa kwenye eneo la tukio kulingana na mavazi waliyovaa. Baada ya mahojiano, watu hao walikiri kuwa gari hilo ni la Salome Makamba na dereva aliyetoroka ni Timoth Makamba ambaye ni mdogo wake Salome Makamba”,ameongeza Kamanda Magiligimba.

Amesema polisi walifika nyumbani kwa Salome Makamba na kufanya upekuzi kisha kuwakamata watu wengine wawili ambao ni Justine Owesiga (35) Mkazi wa Ndala Shinyanga na Gibson Mkongwa (31) mkazi wa Iringa waliokutwa kwenye nyumba hiyo.

“Juhudi za kuwatafuta na kuwakamata Salome Makamba na Timoth Makamba ambaye ndiye dereva wa gari hilo lililotelekezwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga zinaendelea. Gari husika linashikiliwa na watuhumiwa hao wanne na watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika”,amesema.

Amesema Salome Makamba aliachiwa jana kwa dhamana baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi Oktoba 28,2020 kwa tuhuma za kumshambulia msimamizi wa uchaguzi kituo cha kupigia kura cha Bugweto B, Farida John na kumuumiza ambapo aliomba aone matokeo na baada ya kutoridhika nayo aliyachana na kuanza kumshambulia msimamizi huyo wa uchaguzi akiwa na wafuasi wake.

“Natoa wito kwa wanasiasa na wafuasi wao kuacha mihemko ya kisiasa inayopelekea uvunjifu wa amani badala yake wafuate sheria,kanuni na taratibu z auchaguzi na Jeshi la polisi halitasita kamwe kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu au watu au kikundi chochote chenye nia ya kuvuruga amani nchini”,amesema Kamanda Magiligimba.

Malunde
Safi sana
Sema walitakiwa waanze kumtia kiberiti huyo fala aliyebebwa
 
Making a sweeping claim ain’t enough to bring anyone to your corner. Give us a very specific reason to believe your version of the story instead of that of our Police Force!
Blaming me for telling you the truth you don't wanna hear that the police forces in Tanzania are simply the puppets of CCM, and you don't want to take it coz you believe they are "proffesionals" ryt?!

Coz they simply helped your party to win the election pretending your vote did it while the whole world see the true picture, lots of videos and all that...but for yourself you didnot see them!

Hypocrisy of the highest degree.
 
Kumbuka, upo uwezekano wa mpinzani wako kutengeneza fake ballot papers zinazoenesha kura zako ili kujenga mazingira ya kuhoji ushindi wako. Hiyo ni style ya kijasusi!
Na wale mawakala wa upinzani waliokamatwa na policcm wakapelekwa rumande kwa muda ili kutoa nafasi kwa kura feki kuingizwa, utetezi wenu Ni upi?!
 
Unaposema hujawahi kusoma kesi yoyote... maana yake umeshangaa.

Kama hukushangaa, you wouldn’t have invoked your past experience!
Kwahiyo nikisema leo nimelala kuliko jana hapo nimeshangaa?

Hebu nikumbushe tena. Ni lini ulikabidhiwa cheo cha Muamuzi Mkuu na Mshauri wa Maswala ya Kushangaa Mitandaoni?
 
Kwahiyo nikisema leo nimelala kuliko jana hapo nimeshangaa?

Hebu nikumbushe tena. Ni lini ulikabidhiwa cheo cha Muamuzi Mkuu na Mshauri wa Maswala ya Kushangaa Mitandaoni?

Hii ni debate isiyokuwa na tija yoyote. Chapter closed!
 
Do you have any evidence in support of your “fake mandate” claim?

While you’re entitled to your own opinion, you aren’t entitled to your own facts. I voted for them and the results reflect my will. If you didn’t vote for them, that’s fine. Ultimately, the voice of the majority must be respected!
It was a masquerade, not an election but a mock election.

We urge the UN Secretary General to launch a full audit into this shameful election and after findings are presented to him come out with a decisive solution that will serve as a deterrent to such barbaric and shameful acts in future.

This bogus election if left unpunished will go a long way to present a bad precedent to this continent that might keep on being repeated by uncouth and repressive rulers like the one we currently have in this country.
 
Back
Top Bottom