Nyumba ya kulea wazee kwa Dar iko/ziko wapi?

Habari wakuu. Naulizia nyumba ambazo wazee watu wazima wanatunzwa. Nahitaji kwenda kuwasalimia na kuwashika mkono kidogo
ipo kigamboni kijiji kinaitwa tungi, siyo mbali sana na darajani , kuna kambi ya wazee wa enzi na enzi nadhani tangu zama na nyerere, na pia ni kutuo cha watoto wa mtaani!
 
Nyingine Iko Msimbazi Centre. Afadhali unawaza kwenda kusupport maana kama ni wazazi tuwatunze sisi wenyewe. Narudia Tuwatunze sisi wenyewe!
 
UMEWAZA JAMBO JEMA SANA, sio lazima kutoa kanisani au msikitikini,,,,, hata huko ni vema......ukiweza kwenda tunaomba mrejesho mkuu.
 
Habari wakuu. Naulizia nyumba ambazo wazee watu wazima wanatunzwa. Nahitaji kwenda kuwasalimia na kuwashika mkono kidogo
Habari mpendwa,
Heshima kwako hata kwa kukumbuka uwepo wa hili kundi maalum. Nakutia moyo, nenda kawaone. Kituo cha zamani sana ( Wazee na wenye Ukoma) kipo Kigambani, maeneo ya Vijibweni. Ukivuka kwa kutumia daraja lile la kulipia, uliza Vijibweni kituo cha kulelea wazee na wakoma. Utaonyeshwa.
 
Kuuliza kituo si kwamba watu hawatunzi wazazi wao, ni vyema vituo kama hivyo kuvifahamu na kwenda kuvitembelea na kupeleka chochote, hata mtu anavyoulizia vituo vya watoto yatima si kwamba hatunzi watoto wake. Acha kuandika msg bila kufikiri.
Naomba tuwasamehe wote wanaoandika kwa namna isiyopendeza. Katika hili tunaweza chuma dhambi au baraka, mwenzetu ameomba njia ya kufika kituoni, kama huijui piga kimyaa.
 
Habari mpendwa,
Heshima kwako hata kwa kukumbuka uwepo wa hili kundi maalum. Nakutia moyo, nenda kawaone. Kituo cha zamani sana ( Wazee na wenye Ukoma) kipo Kigambani, maeneo ya Vijibweni. Ukivuka kwa kutumia daraja lile la kulipia, uliza Vijibweni kituo cha kulelea wazee na wakoma. Utaonyeshwa.
Asante sana mkuu wa taarifa hii
 
ipo kigamboni kijiji kinaitwa tungi, siyo mbali sana na darajani , kuna kambi ya wazee wa enzi na enzi nadhani tangu zama na nyerere, na pia ni kutuo cha watoto wa mtaani!
Asante kwa maelekezo mkuu
 
Msimbazi centre wapo wazee, ukienda watakupa utaratibu wa kuwatembelea na vitu vya kupeleka.
Barikiwa mkuu kwa moyo wako mzuri.
 
Unataka kwenda kuwatunza au unataka umpeleke dingi yako? Wazo lako linanipa ukakasi ina maana hapo mtaani hakuna wazee waliofulia au kwenye ukoo wako hakuna wahitaji mpaka uanze kuwatafuta kwa tochi.
Kwanini una mawazo hasi ?
 
Back
Top Bottom