Nyumba ya kulala wageni Morogoro nimepata changamoto hapo

Hahaha, tena wapo hivi hao matapeli. Wakiona muonekano wa ki dokita, profesa. Oyaaa Dkt vipi, nipo hapa mtu wangu, tax ipo, za masiku. Kuna tapeli mwingine dar wa mgahawa anapika vyakula asili, ukifika Bhageshi vipi, karibu hahaha yaani watz hawaishi vituko


ccm ndo wamesababisha.
 
Nimefika jioni pale Msamvu (stendi). Akatokea jamaa mmoja, .....aaah ticha vipi habari ya siku, najua unanikumbuka nilikuwa agent (wa basi hilo nililosafili nalo). Ulikuwa unakuja nakukatia tiketi pale, ticha bwana. Anaongea maneno mengiii
NIKAMJIBU WEWE NI MWONGO, MIMI NDIO KWA MARA YA KWANZA NIMEPANDA BASI HILO.
Jamaa, basi nitakuwa nimekuchanganya. Tunaemdelea kutembea, ticha mimi nina tax hapo niunge mkono, hiyo sio shida.
Tukazunguka sana mjini bila mafanikio kwa muda mrefu. Baadae nilipata nyumba fulani.

SASA NINACHOTAKA MPATE HAPA NI HIKI. ASUBUHI NINAPOONDOKA (KUHAMA KWENDA GUEST NYINGINE)MHUDUMU WA GUEST HOUSE (HII NINAYOIACHA) ALIJUA NINA HAMA HAPO KUTOKANA NA GHARAMA, YAANI BEI KUBWA.
AKANIMBIA, .......Kaka unajua wanaotuharibia biashara ni hawa watu wa tax na bodaboda, yaani wakikufikisha hapa hata kama chumba kwetu ni elfu 20 wao wanakutajia 25 ili wapate shilingi 5000 wao. Lakini sisi bei yetu ni shilingi elfu 20 tu.....
Namuuliza, sasa kwa nini na wewe mnakubaliana kuiba, ........akajibu...huwezi kataa kwa sababu hawatakuletea wateja tena.

Nimepanga kukusanya namba kadhaa za simu kwa nyumba za kulala wageni.

Chukua tahadhali
hii Morogoro ipo sana tena hasa hasa kwenye lodge zile za karibu na Msamvu.
 
tafuta gest zipo paka za buku tano....kuna Kiminyio guest house, Bonyeza rest house buku tano swadakta.
Sema maji ya kuoga watakuuzia sh 500
 
Unaweza nipatia namba zao za simu wakaniwekea booking ya chumba
Bahati mbaya sina ila mtaa huo ziko nyingi. Ni mara chache zinajaa. Jirani na Baobab kuna Marimoto lodge. Hii hapa
AF1QipMs3-IcBkgNsvk2UNFIYH8lKrBBv9-Cp2gyErpZ=s1600-w1600.jpg
AF1QipNo_LsY-5YRMXf2CpuoY__r_eMv5F5wn4rMGwA6=s1600-w1600.jpg
images-8.jpg

Tofauti na Baobab, Marimoto vyumba vyenye AC ni vya 30,000 tu na vyumba vyao vya 25,000 ni vidogo. Baobab vyote vina AC na hata vya 20,000 ni vikubwa kabisa.
 
Back
Top Bottom