Nyumba ya kulala wageni Morogoro nimepata changamoto hapo

Wakati mwengine ni sisi tu tunaopenda kuingia gharama sasa sijui ni hatujui kuzitumia vizuri hizi simu zetu janja au vipi?

Tanzania kwa hii miji inayoonekana kuendelea karibu kila kitu chao kipo mtandaoni,ukitumia Google maps popote unafika hasa itumie kujua nyumba za wageni zilizo karibu na uliposhuka gari,angalia ziko umbali gani kama ni 1,2,3 Km unahisi utapotea kufika ita sijui tax au bodaboda mwambie nipeleke maeneo ilipo nyumba hii na akisema bei kubwa utakuwa na uwezo wakum-challenge mbona karibu tu hapo unasema bei kubwa hivyo hii itakufanya uonekane siyo mgeni na mkifika mpe chake aondoke.

Ukishaanza kuwauliza sijui nitapata wapi guest nzuri ndo unapowapa nafasi ya kukupiga mkifika anajifanya kukupeleka reception ooh huyu jamaa yangu mpeni chumba kizuri kumbe kuja pale nikumfahamisha muhudumu kuwa hiki ni kichwa changu nitaijia ganji yangu.
Mkuu hiyo google map ishawahi kunipotezea mtu Zenji namsubiri dream of zanzibar yeye google map imempeleka chwaka bay huko !
 
Jamani naomba kufahamu in average bei za guest zilizopo around msamvu. Kwa master bedrooms na kwa kawaida
 
Kama kuna kitu kinatuponza Watanzania ni kutokuheshimu kile mtu alichonacho!

Ana machungu kagundua kapoteza jasho lake isivyo halali, tunamkebehi!!

Fanya kuheshimu coz hujui kaipata vipi!? Kama we ni mjanja wa kutia sign na kupokea hela basi heshimu ya yule anayeingia shimoni anakaa wiki jua halioni anaitafuta hicho kidogo!! Not fair
Watanzania tunajifanyafanya na kuigiza maisha sana ndugu. Mimi mwenyewe nawashangaa
 
Hahaha, tena wapo hivi hao matapeli. Wakiona muonekano wa ki dokita, profesa. Oyaaa Dkt vipi, nipo hapa mtu wangu, tax ipo, za masiku. Kuna tapeli mwingine dar wa mgahawa anapika vyakula asili, ukifika Bhageshi vipi, karibu hahaha yaani watz hawaishi vituko
😁😀😁😀 Dah, unajua nilikuwa na peni Mfuko wa Shari, halafu nimeshika funguo. Naona akajua huyu ticha😀
 
Hahaha, tena wapo hivi hao matapeli. Wakiona muonekano wa ki dokita, profesa. Oyaaa Dkt vipi, nipo hapa mtu wangu, tax ipo, za masiku. Kuna tapeli mwingine dar wa mgahawa anapika vyakula asili, ukifika Bhageshi vipi, karibu hahaha yaani watz hawaishi vituko
Ukifika Morogoro nyosha mtaa wa Vibandan njia ya SUA kuna lodge kama zoteee
 
Mkuu hiyo google map ishawahi kunipotezea mtu Zenji namsubiri dream of zanzibar yeye google map imempeleka chwaka bay huko !
Mkuu ndo maana hapo juu nikasema kama Google maps unaona huielewi angalia tu umbali wa sehemu husika ili uchukue usafiri upelekwe.

Muhimu ukijue kituo chako na kina umbali gani ili ulipe hela sawa inayoshabihiana na safari yenyewe.
 
Bagheshi msukuma huyo
Hahaha, tena wapo hivi hao matapeli. Wakiona muonekano wa ki dokita, profesa. Oyaaa Dkt vipi, nipo hapa mtu wangu, tax ipo, za masiku. Kuna tapeli mwingine dar wa mgahawa anapika vyakula asili, ukifika Bhageshi vipi, karibu hahaha yaani watz hawaishi vituko
 
Hili suala hata Mwanza,Nyegezi lipo.Ila hawatozi kiasi kikubwa sana
Pale Nyegezi iko hivi, kama ni mgeni ukifika kuna gari mbali mbali ziko pale stendi zinazoshughulika na guest house. Wakipata mteja wanajaribu kukushawishi uende kwao na wanakushawishi na wanakupeleka kwa gari yao huko na asubuhi wanakurudisha stendi kwa ajili ya safari yako. Mara nyingi hawa wanakuwa wanahusika moja kwa moja na guest hiyo. Sijapata taarifa ya namna gani upigaji inafanyika hapa. Vinginevyo, kuna vijana wako pale wakikuona mteja watakushawishi uende kwenye zile gari au guest fulani bila Shaka wanalipwa, (mara nyingi ni kwa guest house za jirani na stendi). Hizi za mbali kidogo ni hawa wenye magari.
 
Hii kitu nimeikuta Dodoma
Nitajifunza, bado sijaona. Sijajua kwa kuwa guest ni nyingi, kuna muda unafikia anayekusafirisha anakosa majibu kwamba tumekosa huku sasa twende wapi. Yule wa Morogoro alikuwa na majibu sana, na almost alijua baada ya kuzunguka mwishowe tunaishia wapi. Kuna muda nilishuka kwenda kuhakiki alichoniambia mudi yake ilibadilika sana Ila sikujua sababu ni hiyo exactly
 
Back
Top Bottom