Nyumba ya kisasa inapangishwa kimara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nyumba ya kisasa inapangishwa kimara

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Kireka1980, Jul 15, 2010.

 1. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2010
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nyumba ina vyumba vinne ikiwemo master (chumba kimoja kikubwa kimefungwa taa maalumu za kusomea), sitting na dinning jiko na store yake, public toilet, full tiles (jikoni na vyoo full hadi kuta), AC master na sitting ipo ndani ya fence in banda la mbwa, kisima cha ku-drill (depth 100 metres) ina eneo la wazi ndani ya fence (20 square metres). Bei ni USD700 kwa mwezi kama upo interested ni-pm at vantde2000@hotmail.com
   
 2. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Pelekea mafisadi, mie askari magereza nitazitolea wapi hizo USD700? hata JK alisema yupo radhi kuukosa usaisi kwa Tshs 350000 sembuse na hiyo je?
   
 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Mkuu tatazo hapo ni location. Sijui kama utapata mtu kwa bei hiyo kwa maeneo hayo!
   
 4. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2010
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Mkuu hizi taa maalumu za kusomea ndio zipi? Unamaana zimefungwa karibu na kitanda au mezani au ni bulb maalumu za kusomea? Nifungue macho!!
   
 5. k

  kukuna Member

  #5
  Jul 17, 2010
  Joined: May 26, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ah jamani kweli watu mnaniacha hoi yaani nimecheka hizo taa maalum za kusomea!mie hoi,eti dola mia saba bongo kuna wazimu hivi mshahara wa nurse,mwalimu na wengineo kweli utapanga nyumba dola mia saba utazitoa wapi?si ndio mambo ya kupalilia wizi na ufisadi jamani!!!!
   
 6. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,958
  Likes Received: 21,122
  Trophy Points: 280
  kwani ni walimu/manesi pekee ndio wapangaji??
   
 7. m

  matambo JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  free market inapotumiwa vibaya, ina maana hizo ni milioni moja kwa mwezi kwa ajili ya nyumba pekee,ambayo inatakiwa isizidi 20% ya mshahara ,mh ok wakurugenzi wapo wengi atakula nao
   
 8. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Inaboa hata kurudia....WEKA PICHA!
   
 9. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu Kireka,

  Kwanini Kodi inakuwa quoted in terms of dollars? Kuna sababu za msingi za kufanya hivyo? Kwa exchange rate ya sasa hivi ya dollar kodi ya nyumba hiyo ni Tshs. 1,046,500 are you serious kwamba mnapangisha hiyo nyumba? Yaani Kimara na matatizo ya eneo hilo tunayoyajua mtapata mpangaji kweli? Nina wasiwasi mwenye nyumba hiyo hayuko serious au inawezekana madalali wameweka cha juu na hivyo uenda wakasababisha nyumba hiyo ikose wapangaji.

  Hebu tuwe realistic jamani!!! Hiyo bei kwa Kimara ni too much!!!!

  Tiba
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  day dreaming
   
 11. D

  Diana-DaboDiff JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2010
  Joined: Jul 13, 2009
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukubwa wa nyumba na details ulizotoa nyumba inastahili laki 5 kwa sababu ya location-Kimara.Nyumba ya namna hiyo some parts of Mikocheni, Msasani,Upanga,SeaView na town centre ungepata Im per month.Location ni muhimu sana tunapojenga nyumba kwa ajili ya kukodisha.Kuna rafiki yangu kajenga nyumba nzuri ya 3bedrooms Buza lakini imebidi akubali laki 1 kwa mwezi baada ya kukosa wapangaji kwa muda mrefu kwa bei aliotaka yeye.Pole sana lakini ndio ukweli wenyewe.
   
 12. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tatizo hapa ni madalali ambao wanawadanganya landlords kiasi cha pesa ya kupangisha, huyu jamaa unaweza kukuta hajawai hata kugusa Midola (Mi-USD).

  Hili Tatizo sijui litaisha lini.............yaani watanzania tumepoteza imani na pesa yetu kabisa...........hadi inafikia watu wanajisikia sijui niite kinyaa/aibu ku-quote kwa madafu yetu
   
 13. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  Kwa Kimara itakuwa ngumu
   
 14. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2010
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ahsante kwa ushirikiano wadau, nyumba imepata mpangaji imechukuliwa na watu wa kanisa moja though bei ilipungua kidogo (1m).
  thanks na tuendelee kushirikiana.
   
Loading...