Nyumba ya kiongozi wa CCM Igunga yachomwa Moto

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,151
1,427
Nyumba ya kiongozi wa ccm Igunga KATIBU KATA yachomwa moto,na ujumbe unao wataja wana CDM kuwa ndio wahusika wa hujuma hiyo waonekana ukiwa na ujumbe huu CHADEMA SISI NI WAJANJA,

Lakini pia hebu angalia picha hapo chini yajieleza nayo hiyo ni hujuma nyingine huko IGUNGA

490702.jpg

Mmoja watu waliotoa kadi zao, Chiristina Kaloli, mkazi wa Iborogero alikiri kuwa kadi yake imeishaandikishwa mjumbe wa CCM huku kusisitiza kuwa hiki ni kipindi cha mavuno kwao.

source: Wavuti - Habari
 
joseeY

Senior Member
Nov 4, 2010
108
17
MATUKIO ya hujuma yanazidi kulitikisa Jimbo la Igunga safari hii watu wasiojulikana wamechoma moto nyumba ya Katibu wa CCM, Kata ya Nyandekwa usiku wa kuamkia juzi.Tukio hilo linahusishwa na wafuasi wa Chadema kutokana na ujumbe wa maandishi uliokutwa umechomekwa katika nyumba hiyo ukisomeka: “Chadema sisi ni wajanja”.Katibu huyo, Hamis Makala alimweleza Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama aliyemtembelea jana kumpa pole kuwa, kwa muda mrefu amekuwa akiwindwa na wafuasi hao wa Chadema.

Alidai kuwa sababu ya kuwindwa na wafuasi hao inatokana na kukasirishwa na kampeni anazozifanya katika kata hiyo zinazoifanya CCM ikubalike kwa wananchi na kukiacha Chadema kikikosa watu kinapokwenda kufanya mikutano ya hadhara. Nyumba iliyoteketezwa kwa moto ilikuwa ikitumiwa na katibu huyo kwa shughuli za jiko na kuhifadhia kuku.

“Niliposhtuka na kutoka nje nilikuta moto mkubwa unawaka nikapiga yowe kuomba msaada. Lakini majirani walishindwa kuuzima kwa kuwa ulikuwa umesambaa… kuku 15 kati ya 21 waliokuwamo ndani wamekufa,” alisema.

Alisema baada ya kushindwa kuuzima moto huo na nyumba hiyo kuteketea, aliamua kulala na asubuhi majirani walipofika tena kumjulia hali ndipo walipogundua karatasi ikiwa na ujumbe wa Chadema kuhusika.

Alidai kuwa mbali na ujumbe huo, upo mwingine wa maandishi ambao ulipenyezwa katika Ofisi ya CCM ya kata hiyo unaosisitiza kuwa Chadema hawahitaji bendera za CCM katika kata hiyo. Alisema kuwa karatasi zote hizo mbili zimechukuliwa na polisi.

Mukama alaani
Akizungumzia tukio hilo, Mukama amesema alisema ni lazima lilaaniwe na kila Mtanzania mpenda amani wakiwamo wananchi wa Igunga na akavitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinawasaka na kuwakamata waliohusika.

“Ni lazima lilaaniwe kwa sababu halitoi taswira na maana halisi ya kuwa na vyama vingi ambavyo vinapaswa kushindana kwa ubora na sera… hatushindani kwa vitisho, uhuni na hata kumwagiana tindikali,” alisema.

Alisema ameshangazwa na mwenendo wa Chadema kuendesha siasa za chuki hususan katika Jimbo la Igunga na kutoa mfano wa Kenya ambako vyama vingi ni vya kikabila lakini hakuna matukio ya aina hiyo.

Alitumia fursa hiyo kupiga kampeni akisema matukio yanayotokea Igunga hivi sasa yanawasaidia Watanzania kukielewa Chadema ni chama cha aina gani na kuwataka Wana-Igunga kukiadhibu hicho kwa kukinyima kura Oktoba 2 ,mwaka huu.

“Demokrasia haiwezi kuanishwa kwa matukio ya kihuni na wale wanaotaka kuipa demokrasia taswira ya hovyo ni lazima waadhibiwe. Njia pekee ya kuwaadhibu watu wa aina hiyo ni kuwanyima kura,” alisema.

Katibu Mkuu huyo alimpa kiongozi huyo msaada wa Sh100,000 ili azitumie kuirejesha nyumba hiyo katika hali iliyokuwapo kabla ya tukio.

CUF waungana na CCM

Mwenyekiti wa CUF Kata ya Nyandekwa, Emmanuel Ezekiel ambaye alifika eneo la tukio mata tu baada ya Mkama na msafara wake kufika, alisema tukio hilo ni la kihuni na linapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.

“Unajua kwenye mji unaweza kuwa na watoto watatu wa baba mmoja, mama mmoja lakini akatokea mmoja akawa kichaa msipomdhibiti atawaharibia ule mji,” alisema Ezekiel bila kufafanua kauli yake hiyo.

Mwenyekiti huyo alitahadharisha kuwa kampeni katika Jimbo hilo la Igunga ni za mwezi mmoja tu lakini, kama zisipofanyika kwa ustaarabu zinaweza kuzaa uhasama utakaodumu kwa miaka mingi.

Polisi wanena

Mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji na tathmini kutoka makao makuu ya Polisi, Naibu Kamishna, Isaya Mngullu alisema polisi wanaendelea na upelelezi.

“Ni kweli hilo tukio lipo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia jana (juzi) na sisi tumeanzisha upelelezi, nipeni muda tukusanye taarifa halafu nitawaita (waandishi) niwapeni taarifa kamili,” alisema Mngullu.

Chadema waruka
Lakini Kamanda wa Operesheni za Kampeni wa Chadema, Benson Kijaila jana alikanusha chama chake kuhusika na tukio hilo na kukigeuzia kibao CCM kuwa wao ndicho kilichoshiriki katika tukio hilo.

“Matukio haya wanayapanga wao wenyewe halafu wanasingizia vijana wetu… kama ni kuchoma hiyo nyumba wameichoma wenyewe ni mpango wao huo,” alisema.

Kamanda huyo alisema hata tuhuma za tindikali zinazoelekezwa kwa Chadema ni mipango iliyosukwa na CCM na kwamba kama ni watu wenye tindikali, basi CCM ndiyo walionazo.

Tukio hilo la juzi la kuchomwa moto nyumba ya kada huyo wa CCM ni mwendelezo wa matukio ya kihalifu yanayotokea Igunga na wakati wote, matukio hayo yamehusishwa na wafuasi wa Chadema.

Mwanzoni mwa wiki hii, wabunge wawili na kada mmoja wa chama hicho walishtakiwa mahakamani kwa makosa manne likiwamo la kumdhalilisha na kumwibia Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.

Septemba 9 mwaka huu, kijana mmoja anayedaiwa ni mwanachama wa CCM, Mussa Tesha (25) alimwagiwa tindikali usoni na watu anaodai kuwatambua kuwa ni wanachama wa Chadema.

SOURCE: Mwananchi 

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,467
1,164
Nyumba ya kiongozi wa CCM Igunga yachomwa Moto Send to a friend
Wednesday, 21 September 2011 21:03
0digg
Daniel Mjema, Igunga
MATUKIO ya hujuma yanazidi kulitikisa Jimbo la Igunga safari hii watu wasiojulikana wamechoma moto nyumba ya Katibu wa CCM, Kata ya Nyandekwa usiku wa kuamkia juzi.Tukio hilo linahusishwa na wafuasi wa Chadema kutokana na ujumbe wa maandishi uliokutwa umechomekwa katika nyumba hiyo ukisomeka: "Chadema sisi ni wajanja".Katibu huyo, Hamis Makala alimweleza Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama aliyemtembelea jana kumpa pole kuwa, kwa muda mrefu amekuwa akiwindwa na wafuasi hao wa Chadema.

Alidai kuwa sababu ya kuwindwa na wafuasi hao inatokana na kukasirishwa na kampeni anazozifanya katika kata hiyo zinazoifanya CCM ikubalike kwa wananchi na kukiacha Chadema kikikosa watu kinapokwenda kufanya mikutano ya hadhara. Nyumba iliyoteketezwa kwa moto ilikuwa ikitumiwa na katibu huyo kwa shughuli za jiko na kuhifadhia kuku.

"Niliposhtuka na kutoka nje nilikuta moto mkubwa unawaka nikapiga yowe kuomba msaada. Lakini majirani walishindwa kuuzima kwa kuwa ulikuwa umesambaa… kuku 15 kati ya 21 waliokuwamo ndani wamekufa," alisema.

Alisema baada ya kushindwa kuuzima moto huo na nyumba hiyo kuteketea, aliamua kulala na asubuhi majirani walipofika tena kumjulia hali ndipo walipogundua karatasi ikiwa na ujumbe wa Chadema kuhusika.

Alidai kuwa mbali na ujumbe huo, upo mwingine wa maandishi ambao ulipenyezwa katika Ofisi ya CCM ya kata hiyo unaosisitiza kuwa Chadema hawahitaji bendera za CCM katika kata hiyo. Alisema kuwa karatasi zote hizo mbili zimechukuliwa na polisi.

Mukama alaani
Akizungumzia tukio hilo, Mukama amesema alisema ni lazima lilaaniwe na kila Mtanzania mpenda amani wakiwamo wananchi wa Igunga na akavitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinawasaka na kuwakamata waliohusika.

"Ni lazima lilaaniwe kwa sababu halitoi taswira na maana halisi ya kuwa na vyama vingi ambavyo vinapaswa kushindana kwa ubora na sera… hatushindani kwa vitisho, uhuni na hata kumwagiana tindikali," alisema.

Alisema ameshangazwa na mwenendo wa Chadema kuendesha siasa za chuki hususan katika Jimbo la Igunga na kutoa mfano wa Kenya ambako vyama vingi ni vya kikabila lakini hakuna matukio ya aina hiyo.

Alitumia fursa hiyo kupiga kampeni akisema matukio yanayotokea Igunga hivi sasa yanawasaidia Watanzania kukielewa Chadema ni chama cha aina gani na kuwataka Wana-Igunga kukiadhibu hicho kwa kukinyima kura Oktoba 2 ,mwaka huu.

"Demokrasia haiwezi kuanishwa kwa matukio ya kihuni na wale wanaotaka kuipa demokrasia taswira ya hovyo ni lazima waadhibiwe. Njia pekee ya kuwaadhibu watu wa aina hiyo ni kuwanyima kura," alisema.

Katibu Mkuu huyo alimpa kiongozi huyo msaada wa Sh100,000 ili azitumie kuirejesha nyumba hiyo katika hali iliyokuwapo kabla ya tukio.

CUF waungana na CCM

Mwenyekiti wa CUF Kata ya Nyandekwa, Emmanuel Ezekiel ambaye alifika eneo la tukio mata tu baada ya Mkama na msafara wake kufika, alisema tukio hilo ni la kihuni na linapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.

"Unajua kwenye mji unaweza kuwa na watoto watatu wa baba mmoja, mama mmoja lakini akatokea mmoja akawa kichaa msipomdhibiti atawaharibia ule mji," alisema Ezekiel bila kufafanua kauli yake hiyo.

Mwenyekiti huyo alitahadharisha kuwa kampeni katika Jimbo hilo la Igunga ni za mwezi mmoja tu lakini, kama zisipofanyika kwa ustaarabu zinaweza kuzaa uhasama utakaodumu kwa miaka mingi.

Polisi wanena

Mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji na tathmini kutoka makao makuu ya Polisi, Naibu Kamishna, Isaya Mngullu alisema polisi wanaendelea na upelelezi.

"Ni kweli hilo tukio lipo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia jana (juzi) na sisi tumeanzisha upelelezi, nipeni muda tukusanye taarifa halafu nitawaita (waandishi) niwapeni taarifa kamili," alisema Mngullu.

Chadema waruka
Lakini Kamanda wa Operesheni za Kampeni wa Chadema, Benson Kijaila jana alikanusha chama chake kuhusika na tukio hilo na kukigeuzia kibao CCM kuwa wao ndicho kilichoshiriki katika tukio hilo.

"Matukio haya wanayapanga wao wenyewe halafu wanasingizia vijana wetu… kama ni kuchoma hiyo nyumba wameichoma wenyewe ni mpango wao huo," alisema.

Kamanda huyo alisema hata tuhuma za tindikali zinazoelekezwa kwa Chadema ni mipango iliyosukwa na CCM na kwamba kama ni watu wenye tindikali, basi CCM ndiyo walionazo.

Tukio hilo la juzi la kuchomwa moto nyumba ya kada huyo wa CCM ni mwendelezo wa matukio ya kihalifu yanayotokea Igunga na wakati wote, matukio hayo yamehusishwa na wafuasi wa Chadema.

Mwanzoni mwa wiki hii, wabunge wawili na kada mmoja wa chama hicho walishtakiwa mahakamani kwa makosa manne likiwamo la kumdhalilisha na kumwibia Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.

Septemba 9 mwaka huu, kijana mmoja anayedaiwa ni mwanachama wa CCM, Mussa Tesha (25) alimwagiwa tindikali usoni na watu anaodai kuwatambua kuwa ni wanachama wa Chadema.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

[h=4]Comments [/h]

http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#0#9 Kwanama 2011-09-22 08:43
Wakati mwingine ni vema CCM kukukmbuka kuwa jamani zama za zamani zilishapita mbinu za ki[NENO BAYA]kama hizi acheni mtajiaibisha bure.
Gazeti la mwananchi nanyi komeni kuandika habari kwa mwelekeo wa kukituhumu Chadema, kwanini mhariri usitoe habari kama zilivyo kuliko kuanza kujenga mwelekeo wa kuonyesha uhalifu wowote unafanywa na chadema?
Quote

http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#0#8 Ally 2011-09-22 08:31
Jamani wa-TZ kama kuna kuchafuliana kwa jinsi hii basi huu ni utoto kabisa. Mbona hawajalaani Mh. Mwingulu Mbunge wa Iramba na Meneja wa Kampeni wa CCM Igunga alipofumaniwa na mke wa kada mwenzake wa CCM huko huko Igunga? Sidhani kama kweli CHADEMA ilihusika vinginevyo wasingeacha ujumbe wa maandishi. Na iweje banda la kuku pamoja na kuku 15 vyote viteketee kwa moto halafu karatasi yenye ujumbe iwe salama? Ni kipi rahisi kuungua moto. Hizi ni mbinu zilizopitwa kabisa na wakati na Polisi sio [NENO BAYA] kiasi hicho uchunguzi wao utadhihirisha mbichi na mbivu. Huwezi ukamfanyia mtu uhasama mkubwa hivyo halafu umwandikie jina lako umwachie. CCM acheni mambo ya ki[NENO BAYA] namna hiyo. Pambaneni kwanza na Mafisadi na hao wazinzi walioibuka kwenye kamoeni zenu.
Quote

http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#0#7 Amwesiga 2011-09-22 08:27
Unajua inafikia muda hata uwezo wa kufikiria unaisha sasa unaamua hata kujidanganya mwenyewe? CHADEMA ndio mti wenye matunda Igunga na Tanzania nzima kwa ujumla kwa hautacha kutupiwa mawe, tusiwe na jazba tuendelee kuiunga mkono CHADEMA kadri tuwezavyo na tutashinda. Unajua ccm kwa wanauza ng'ombe kwa kesi ya kuku, hawajui wanachofanya, haina haja ya kupoteza muda kuwajadili sana na badala yake tutumie muda wetu kuiweka CHADEMA mahali sahihi. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA.
Quote

http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#+3#6 Bakari 2011-09-22 06:43
CCM imeishiwa... ikishinda Igunga itakuwa kwa mtaji wa UJI-NGA wa wananchi. Haiingii akilini:-

1) Chadema kuchoma BANDA LA KUKU badala ya nyumba ya makazi kisha kuhacha ujumbe kuwa ni wao (lazima watakuwa wendawazimu),

2) Mkama kutoa 100,000/= kwa kada kuunguliwa BANDA LA KUKU, ilhali walishindwa kuwasaidia wakazi wa Gongo la Mboto,

3) Kada kuunguliwa nyumba kisha kurudi kuuchapa usingizi,

4) licha ya majirani kushindwa kuuzima moto kwa kusambaa, karatasi yenye ujumbe wa Chadema kuhusika imesalimika,
Quote

http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#+2#5 Mwalimu 2011-09-22 04:55
Hiyo ni janja ya nyani kula mahindi mabichi, Hivi kwa mtu mwenye akili zake anaweza kwenda kuchoma bamnda la kuku na kuandika kuwa mimi Chadema nimechoma , ila cha msingi ni kuwa makini, kama ingekuwa ni kuchoma basi wangechoma nyumba sio banda la kuku,
Quote

http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#+2#4 rostow prof 2011-09-22 04:33
wasomaji wengi wa gazeti hili la mwananchi ni wapenda mabadiliko, kwa hiyo gazeti la mwananchi isipojiangalia litajimaliza lenyewe kama halitaacha kushabikia mambo ya hovyo yanayofanywa na ccm kwa kuichafua chadema, hakika wasubiri kiama chao cha kupoteza biashara na heshima zao walizojizolea siku zilizopita kwa kuwaongoza watanzania ktk kujenga fikra za mabadilko, lakini sasa na nasikitika kuona hata wenyewe wamiliki wa mwanananchi wanataka kupotoka tena sijui wanawaogopa ccm? watanzania watawapeni tuzo lenu!
Quote

http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#+2#3 rostow prof 2011-09-22 04:13
Bila shaka ccm ndiyo wanahusika na hayo matukio ili wawachafulie chadema ionekane inaleta vurugu ktk kampeni hizo ili kupandikiza chuki kwa kuwaaminisha wananchi wa igunga ili wasipigie chadema kura, hiyo ni kampeni chafu za ccm kule igunga.
pia mimi nimeamini kuwa gazeti la mwananchi sasa hivi inatumika kupiga kampeni za ccm, kwani mwandishi huyo ana remba kuandika hiyo habari ya uwongo hasa hiyo aya ya mwisho eti matukio hayo yote yaliyotokea yanahusishwa na chadema....ana mantiki gani ktk jambo hilo? anataka kuwaaminisha wasomaji wa mwananchi kuwa chadema ndiyo iliyohusika km wanavyo sema wa ccm? wandugu wapenda haki sasa tuna kila sababu ya kususia gazeti la mwananchi hakika haindiki habari nzuri km zamani, sasa hivi inaipigia debe ccm ishinde igunga. nawabashiria gazeti la mwananchi na ccm yao watashindwaviba ya sana hapa tanzania na hawatakuwepo tena ktk siku za usoni. tuwe imara tupende chadema yetu, chama bora kuliko vyama vyote tanzania.
Quote

http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#+4#2 ahmed00 2011-09-22 04:09
@ Mwongozo, Msema kweli, malaria sugu na Makada wote wa ccm naomba mjibu haya maswali
1)Kama CDM walitaka kumkomoa, walishindwa nini kuchoma moto nyumba anayoishi huyo Katibu? Hii inatokana na tuhuma za Tindikali, kumkata mapanga kada wa ccm, hivyo wasingeshindwa kulipua hiyo nyumba.
2)Soma hii "Alisema baada ya kushindwa kuuzima moto huo na nyumba hiyo kuteketea, aliamua kulala mpaka asubuhi"
Hivi kweli watu wanataka kukuua kwa kuchoma moto nyumba yako, unaweza kwenda kulala mpaka asubuhi? Busara angesema alilinda nyumba yake pamoja na majirani mpaka asubuhi na sio kulala.
3)Hiyo karatasi haikuungua? haikupeperuka kwa upepo usiku kucha? Je ni [NENO BAYA] gani hasa vijijini anayeweza kuacha ujumbe? Hizo karatasi zipo mbili tuu nyumbani na ofisini kwake tuu?
4)Mukana katumia hilo janga kufanya kampeni, then kampa Shs100,000 kujenga kibanda kingine. Hiyo 100,000 ni rushwa na kitendo cha Mukama kufanya mkutano wa kampeni kama hawakuwa na ratiba ni kosa kisheria. Je kwanini Mukama hakukamatwa kwa kufanya kampeni bila kibali?
5)Tunajua Igunga ni ngome ya Rostam, watu wengi walichukizwa kwa ccm kumsakama mpaka kuachia ngazi. Kwanini haya matukio yasihusishwe na hujuma za mafisadi dhidi ya ccm?
Quote

http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#http://mwananchi.co.tz/component/co...ya-kiongozi-wa-ccm-igunga-yachomwa-moto.html#+3#1 Beano 2011-09-22 01:21
Kama kuna wakati CCM inafanya mambo ya kitoto ni sasa. Hivi kama CHADEMA kweli walikuwa wana nia ya kufanya hujuma wangeweka jina lao kwenye karatasi? Huu ni u t a a h i r a wa mchana wa kutaka kuwadanganya watu kuwa CHADEMA ni wavunjifu wa amani. Kudhihirisha ni kamchezo ka-k i j i n g a, wamechoma banda la kuku na jiko. Huyo mwenyekiti wa CCM ame-sacrifice kuku wake ili kuipaka matope CHADEMA na bila kutumia busara CUF nao wameitikia ngoma ya mashetani na kuanza kucheza.

Wanatumia fursa ya elimu ndogo waliyonayo watu wa vijijini kuwarubuni na mambo ya kutunga laiti kama ingekuwa ni huku mjini tungewaadhibu vikali siku ya kupiga kura. Wana wa Igunga msidanganyike na propaganda za CCM ambao mazungumzo ya maendeleo wameishiwa na wanataka kuficha uozo wa ufisadi nyuma ya "amani" ambayo wao wenyewe ndio wa kwanza kuivunja kwa wizi wa mali za umma.
Quote

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,467
1,164
Nyumba ya kiongozi wa CCM Igunga yachomwa Moto Send to a friend

Wednesday, 21 September 2011 21:03
0digg

Daniel Mjema, Igunga
MATUKIO ya hujuma yanazidi kulitikisa Jimbo la Igunga safari hii watu wasiojulikana wamechoma moto nyumba ya Katibu wa CCM, Kata ya Nyandekwa usiku wa kuamkia juzi.Tukio hilo linahusishwa na wafuasi wa Chadema kutokana na ujumbe wa maandishi uliokutwa umechomekwa katika nyumba hiyo ukisomeka: “Chadema sisi ni wajanja”.Katibu huyo, Hamis Makala alimweleza Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama aliyemtembelea jana kumpa pole kuwa, kwa muda mrefu amekuwa akiwindwa na wafuasi hao wa Chadema.

Alidai kuwa sababu ya kuwindwa na wafuasi hao inatokana na kukasirishwa na kampeni anazozifanya katika kata hiyo zinazoifanya CCM ikubalike kwa wananchi na kukiacha Chadema kikikosa watu kinapokwenda kufanya mikutano ya hadhara. Nyumba iliyoteketezwa kwa moto ilikuwa ikitumiwa na katibu huyo kwa shughuli za jiko na kuhifadhia kuku.

“Niliposhtuka na kutoka nje nilikuta moto mkubwa unawaka nikapiga yowe kuomba msaada. Lakini majirani walishindwa kuuzima kwa kuwa ulikuwa umesambaa… kuku 15 kati ya 21 waliokuwamo ndani wamekufa,” alisema.

Alisema baada ya kushindwa kuuzima moto huo na nyumba hiyo kuteketea, aliamua kulala na asubuhi majirani walipofika tena kumjulia hali ndipo walipogundua karatasi ikiwa na ujumbe wa Chadema kuhusika.

Alidai kuwa mbali na ujumbe huo, upo mwingine wa maandishi ambao ulipenyezwa katika Ofisi ya CCM ya kata hiyo unaosisitiza kuwa Chadema hawahitaji bendera za CCM katika kata hiyo. Alisema kuwa karatasi zote hizo mbili zimechukuliwa na polisi.

Mukama alaani
Akizungumzia tukio hilo, Mukama amesema alisema ni lazima lilaaniwe na kila Mtanzania mpenda amani wakiwamo wananchi wa Igunga na akavitaka vyombo vya dola kuhakikisha vinawasaka na kuwakamata waliohusika.

“Ni lazima lilaaniwe kwa sababu halitoi taswira na maana halisi ya kuwa na vyama vingi ambavyo vinapaswa kushindana kwa ubora na sera… hatushindani kwa vitisho, uhuni na hata kumwagiana tindikali,” alisema.

Alisema ameshangazwa na mwenendo wa Chadema kuendesha siasa za chuki hususan katika Jimbo la Igunga na kutoa mfano wa Kenya ambako vyama vingi ni vya kikabila lakini hakuna matukio ya aina hiyo.

Alitumia fursa hiyo kupiga kampeni akisema matukio yanayotokea Igunga hivi sasa yanawasaidia Watanzania kukielewa Chadema ni chama cha aina gani na kuwataka Wana-Igunga kukiadhibu hicho kwa kukinyima kura Oktoba 2 ,mwaka huu.

“Demokrasia haiwezi kuanishwa kwa matukio ya kihuni na wale wanaotaka kuipa demokrasia taswira ya hovyo ni lazima waadhibiwe. Njia pekee ya kuwaadhibu watu wa aina hiyo ni kuwanyima kura,” alisema.

Katibu Mkuu huyo alimpa kiongozi huyo msaada wa Sh100,000 ili azitumie kuirejesha nyumba hiyo katika hali iliyokuwapo kabla ya tukio.

CUF waungana na CCM

Mwenyekiti wa CUF Kata ya Nyandekwa, Emmanuel Ezekiel ambaye alifika eneo la tukio mata tu baada ya Mkama na msafara wake kufika, alisema tukio hilo ni la kihuni na linapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.

“Unajua kwenye mji unaweza kuwa na watoto watatu wa baba mmoja, mama mmoja lakini akatokea mmoja akawa kichaa msipomdhibiti atawaharibia ule mji,” alisema Ezekiel bila kufafanua kauli yake hiyo.

Mwenyekiti huyo alitahadharisha kuwa kampeni katika Jimbo hilo la Igunga ni za mwezi mmoja tu lakini, kama zisipofanyika kwa ustaarabu zinaweza kuzaa uhasama utakaodumu kwa miaka mingi.

Polisi wanena

Mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji na tathmini kutoka makao makuu ya Polisi, Naibu Kamishna, Isaya Mngullu alisema polisi wanaendelea na upelelezi.

“Ni kweli hilo tukio lipo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia jana (juzi) na sisi tumeanzisha upelelezi, nipeni muda tukusanye taarifa halafu nitawaita (waandishi) niwapeni taarifa kamili,” alisema Mngullu.

Chadema waruka
Lakini Kamanda wa Operesheni za Kampeni wa Chadema, Benson Kijaila jana alikanusha chama chake kuhusika na tukio hilo na kukigeuzia kibao CCM kuwa wao ndicho kilichoshiriki katika tukio hilo.

“Matukio haya wanayapanga wao wenyewe halafu wanasingizia vijana wetu… kama ni kuchoma hiyo nyumba wameichoma wenyewe ni mpango wao huo,” alisema.

Kamanda huyo alisema hata tuhuma za tindikali zinazoelekezwa kwa Chadema ni mipango iliyosukwa na CCM na kwamba kama ni watu wenye tindikali, basi CCM ndiyo walionazo.

Tukio hilo la juzi la kuchomwa moto nyumba ya kada huyo wa CCM ni mwendelezo wa matukio ya kihalifu yanayotokea Igunga na wakati wote, matukio hayo yamehusishwa na wafuasi wa Chadema.

Mwanzoni mwa wiki hii, wabunge wawili na kada mmoja wa chama hicho walishtakiwa mahakamani kwa makosa manne likiwamo la kumdhalilisha na kumwibia Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario.

Septemba 9 mwaka huu, kijana mmoja anayedaiwa ni mwanachama wa CCM, Mussa Tesha (25) alimwagiwa tindikali usoni na watu anaodai kuwatambua kuwa ni wanachama wa Chadema.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments

0#9 Kwanama 2011-09-22 08:43
Wakati mwingine ni vema CCM kukukmbuka kuwa jamani zama za zamani zilishapita mbinu za ki[NENO BAYA]kama hizi acheni mtajiaibisha bure.
Gazeti la mwananchi nanyi komeni kuandika habari kwa mwelekeo wa kukituhumu Chadema, kwanini mhariri usitoe habari kama zilivyo kuliko kuanza kujenga mwelekeo wa kuonyesha uhalifu wowote unafanywa na chadema?

Quote

0#8 Ally 2011-09-22 08:31
Jamani wa-TZ kama kuna kuchafuliana kwa jinsi hii basi huu ni utoto kabisa. Mbona hawajalaani Mh. Mwingulu Mbunge wa Iramba na Meneja wa Kampeni wa CCM Igunga alipofumaniwa na mke wa kada mwenzake wa CCM huko huko Igunga? Sidhani kama kweli CHADEMA ilihusika vinginevyo wasingeacha ujumbe wa maandishi. Na iweje banda la kuku pamoja na kuku 15 vyote viteketee kwa moto halafu karatasi yenye ujumbe iwe salama? Ni kipi rahisi kuungua moto. Hizi ni mbinu zilizopitwa kabisa na wakati na Polisi sio [NENO BAYA] kiasi hicho uchunguzi wao utadhihirisha mbichi na mbivu. Huwezi ukamfanyia mtu uhasama mkubwa hivyo halafu umwandikie jina lako umwachie. CCM acheni mambo ya ki[NENO BAYA] namna hiyo. Pambaneni kwanza na Mafisadi na hao wazinzi walioibuka kwenye kamoeni zenu.

Quote

0#7 Amwesiga 2011-09-22 08:27
Unajua inafikia muda hata uwezo wa kufikiria unaisha sasa unaamua hata kujidanganya mwenyewe? CHADEMA ndio mti wenye matunda Igunga na Tanzania nzima kwa ujumla kwa hautacha kutupiwa mawe, tusiwe na jazba tuendelee kuiunga mkono CHADEMA kadri tuwezavyo na tutashinda. Unajua ccm kwa wanauza ng'ombe kwa kesi ya kuku, hawajui wanachofanya, haina haja ya kupoteza muda kuwajadili sana na badala yake tutumie muda wetu kuiweka CHADEMA mahali sahihi. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CHADEMA.

Quote

+3#6 Bakari 2011-09-22 06:43
CCM imeishiwa... ikishinda Igunga itakuwa kwa mtaji wa UJI-NGA wa wananchi. Haiingii akilini:-

1) Chadema kuchoma BANDA LA KUKU badala ya nyumba ya makazi kisha kuhacha ujumbe kuwa ni wao (lazima watakuwa wendawazimu),

2) Mkama kutoa 100,000/= kwa kada kuunguliwa BANDA LA KUKU, ilhali walishindwa kuwasaidia wakazi wa Gongo la Mboto,

3) Kada kuunguliwa nyumba kisha kurudi kuuchapa usingizi,

4) licha ya majirani kushindwa kuuzima moto kwa kusambaa, karatasi yenye ujumbe wa Chadema kuhusika imesalimika,

Quote

+2#5 Mwalimu 2011-09-22 04:55
Hiyo ni janja ya nyani kula mahindi mabichi, Hivi kwa mtu mwenye akili zake anaweza kwenda kuchoma bamnda la kuku na kuandika kuwa mimi Chadema nimechoma , ila cha msingi ni kuwa makini, kama ingekuwa ni kuchoma basi wangechoma nyumba sio banda la kuku,

Quote

+2#4 rostow prof 2011-09-22 04:33
wasomaji wengi wa gazeti hili la mwananchi ni wapenda mabadiliko, kwa hiyo gazeti la mwananchi isipojiangalia litajimaliza lenyewe kama halitaacha kushabikia mambo ya hovyo yanayofanywa na ccm kwa kuichafua chadema, hakika wasubiri kiama chao cha kupoteza biashara na heshima zao walizojizolea siku zilizopita kwa kuwaongoza watanzania ktk kujenga fikra za mabadilko, lakini sasa na nasikitika kuona hata wenyewe wamiliki wa mwanananchi wanataka kupotoka tena sijui wanawaogopa ccm? watanzania watawapeni tuzo lenu!

Quote

+2#3 rostow prof 2011-09-22 04:13
Bila shaka ccm ndiyo wanahusika na hayo matukio ili wawachafulie chadema ionekane inaleta vurugu ktk kampeni hizo ili kupandikiza chuki kwa kuwaaminisha wananchi wa igunga ili wasipigie chadema kura, hiyo ni kampeni chafu za ccm kule igunga.
pia mimi nimeamini kuwa gazeti la mwananchi sasa hivi inatumika kupiga kampeni za ccm, kwani mwandishi huyo ana remba kuandika hiyo habari ya uwongo hasa hiyo aya ya mwisho eti matukio hayo yote yaliyotokea yanahusishwa na chadema....ana mantiki gani ktk jambo hilo? anataka kuwaaminisha wasomaji wa mwananchi kuwa chadema ndiyo iliyohusika km wanavyo sema wa ccm? wandugu wapenda haki sasa tuna kila sababu ya kususia gazeti la mwananchi hakika haindiki habari nzuri km zamani, sasa hivi inaipigia debe ccm ishinde igunga. nawabashiria gazeti la mwananchi na ccm yao watashindwaviba ya sana hapa tanzania na hawatakuwepo tena ktk siku za usoni. tuwe imara tupende chadema yetu, chama bora kuliko vyama vyote tanzania.

Quote

+4#2 ahmed00 2011-09-22 04:09
@ Mwongozo, Msema kweli, malaria sugu na Makada wote wa ccm naomba mjibu haya maswali
1)Kama CDM walitaka kumkomoa, walishindwa nini kuchoma moto nyumba anayoishi huyo Katibu? Hii inatokana na tuhuma za Tindikali, kumkata mapanga kada wa ccm, hivyo wasingeshindwa kulipua hiyo nyumba.
2)Soma hii "Alisema baada ya kushindwa kuuzima moto huo na nyumba hiyo kuteketea, aliamua kulala mpaka asubuhi"
Hivi kweli watu wanataka kukuua kwa kuchoma moto nyumba yako, unaweza kwenda kulala mpaka asubuhi? Busara angesema alilinda nyumba yake pamoja na majirani mpaka asubuhi na sio kulala.
3)Hiyo karatasi haikuungua? haikupeperuka kwa upepo usiku kucha? Je ni [NENO BAYA] gani hasa vijijini anayeweza kuacha ujumbe? Hizo karatasi zipo mbili tuu nyumbani na ofisini kwake tuu?
4)Mukana katumia hilo janga kufanya kampeni, then kampa Shs100,000 kujenga kibanda kingine. Hiyo 100,000 ni rushwa na kitendo cha Mukama kufanya mkutano wa kampeni kama hawakuwa na ratiba ni kosa kisheria. Je kwanini Mukama hakukamatwa kwa kufanya kampeni bila kibali?
5)Tunajua Igunga ni ngome ya Rostam, watu wengi walichukizwa kwa ccm kumsakama mpaka kuachia ngazi. Kwanini haya matukio yasihusishwe na hujuma za mafisadi dhidi ya ccm?

Quote

+3#1 Beano 2011-09-22 01:21
Kama kuna wakati CCM inafanya mambo ya kitoto ni sasa. Hivi kama CHADEMA kweli walikuwa wana nia ya kufanya hujuma wangeweka jina lao kwenye karatasi? Huu ni u t a a h i r a wa mchana wa kutaka kuwadanganya watu kuwa CHADEMA ni wavunjifu wa amani. Kudhihirisha ni kamchezo ka-k i j i n g a, wamechoma banda la kuku na jiko. Huyo mwenyekiti wa CCM ame-sacrifice kuku wake ili kuipaka matope CHADEMA na bila kutumia busara CUF nao wameitikia ngoma ya mashetani na kuanza kucheza.

Wanatumia fursa ya elimu ndogo waliyonayo watu wa vijijini kuwarubuni na mambo ya kutunga laiti kama ingekuwa ni huku mjini tungewaadhibu vikali siku ya kupiga kura. Wana wa Igunga msidanganyike na propaganda za CCM ambao mazungumzo ya maendeleo wameishiwa na wanataka kuficha uozo wa ufisadi nyuma ya "amani" ambayo wao wenyewe ndio wa kwanza kuivunja kwa wizi wa mali za umma.

Quote

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,990
4,500
.......watu wasiojulikana wamechoma moto nyumba ya Katibu wa CCM, Kata ya Nyandekwa usiku wa kuamkia juzi......... ujumbe wa maandishi uliokutwa umechomekwa katika nyumba hiyo ukisomeka: "Chadema sisi ni wajanja".
Alisema baada ya kushindwa kuuzima moto huo na nyumba hiyo kuteketea, aliamua kulala
Eti mtu kachomewa nyumba akashindwa kuuzima moto akaenda kulala akauacha moto unawaka kesho yake akakuta karatasi kwenye hiyo hiyo nyumba ambayo moto wake alishindwa kuuzima inamtaja aliyechoma, hii inaingia akilini kweli? Hizi cheap politics CCM wameingia choo cha kike zinawashusha badala ya kuwapandisha.
 
mashikolomageni

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
1,568
185
Dunia ya leo mhalifu anafanya uhalifu na anaacha signature!! Hii inanikumbusha kipindi cha mahoka!!!!!!!!!!!! Eti sisi cdm ni wajanja katika hali ya kwaida hakuna criminal anaye acha signature ya wazi, huacha signature complicated inayo hitaji kufikiri sana sasa hiyo iliyo achwa inabidi ifikirishe watu
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
yaani mtu amechoma nyumba motto halafu akapachika karatasi akasema kuwa ni sisi chadema ndio tumechoma doesn't that smell so fish.
nilishasema huko nyuma CCM baada ya kuzidiwa hoja itatumia matukio kwa ajili ya kutafuta huruma za wapiga kura na kuwapaka matope
wapinzani wake kwani tukianza ku deal kwa hoja kwa maana ya umeme, maji, sukari ugumu wa maisha na huduma za jamii CCM haina cha
kuwaeleza wananchi. matukio yote haya yanapangwa na CCM na ndio maana ktk matukio mengi haya hakuna anayekamatwa na wategemee
mengine zaidi CCM kitaendelea ku ya stage natabiri kuwa CCM inaweza hata kufikia kupanga mauhaji ili kuonyesha ubaya wa chadema

chadema endeleeni kuwaelilisha wananchi kuwa hizo zote ni mbinu za CCM za kutafuta huruma za wapiga kura na matukio haya yote yanatengezwa na huyu muhusika atakuwa ameshahaidiwa kujengewa nyumba nyingine na hawa mafisadi wa ccm.
 
Dullo

JF-Expert Member
Oct 24, 2009
251
64
Huu ni usani wa kitoto ambao hauna maana yeyote na unawashushia heshima!1
 
andrewk

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
3,102
484
CCM bado wamelala, wanatunia mbinu zilizopitwa na wakati kwawachafua chadema, sijua kama watafaninkiwa,

ukiangalia kwa makini sana hiyo nyumba iloungua, utaweza ona na kukubaliana na mimi kuwa ilichomwa na CCM wenyewe na mwenyummba alihusika
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,340
38,978
Wakati mwingine unapojaribu kuwazuga watu basi angalau ujitahidi kidogo wazugike. Yaani kama mwanamazingaombwe akifanya mazingaombwe na kila anayeangalia akijua yanavyofanyika hayo si mazingaombwe ni kichekesho. Unajua tusipoangalia hawa watu kweli watauana ili washinde uchaguzi? Hizi ni mbinu mbaya sana za voters suppression ambazo tunazosishuhudia. This is rather pathetic.
 
shegaboy

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
213
34
Chadema waendekuchoma nyumba ya kulala kuku kwanini wasichome nyumba yake ya kuishi kwa kuwa wanamtuumu. jamani tuwena ujanja wa kujieleza au kutafuta sababu amabyo mwingine awezi kutoka lakini hii nasema ni choo cha kike wamaingia hawa jamaa. Inaonyesha ni jinsi gani mmekamatwa huko Igunga . kweli Viongozi wa chadema wawatume na kisha waambie muache ujumbe ili wajue ni sisi kwani kama ingechomwa na kubaki bila ujumbe si mngesema ni chadema wamechoma jamani
 
HISIA KALI

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
694
108
Hizi siasa za hujumu zinatumiwa sana na viongozi wa CCM. Wakati mwingine zinatumika hata ndani ya chama chenyewe. Tunakumbuka wakati wa mchakato wa CCM wa kumpata Rais wa kumridhi Mkapa jinsi wanamtandao walivyotumika kuwa husisha wagombea kama akina Sumaye kuwa na hela nyingi sana nje ya nchi na Dr Salum kuwa sio mzanzibar. Hiyo yote inilikuwa ni siasa uchwara ambazo hata Rostam Aziz mwenyewe alisema zipo CCM na ndiyo chanzo cha yeye kujizulu nafasi za uongozi CCM. Hata hivyo watu wenye akili zao walimshangaa pale alipoenda tena kwenye mkutano wa ufunguzi wa kampeni kuwataka wanapiga kura wake kuchagua chama hicho hicho chenye siasa uchwara. Sasa CCM wameseleta hizi siasa kwenye uchaguzi wa Igunga. Nia ni kuwaadaa wananchi wa Igunga ili waone kuwa CHADEMA ni watu wa vurugu.

Sasa kama hicho kibanda kimeungua inakuwaje hiyo karatasi haikuungua?

CHADEMA wanatakiwa kujibu hizi tuhuma kwenye kila mkutano wa kampeni kuanzia sasa la sivyo wapiga kura watazichukuwa kuwa ni za ukweli.
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
33,126
37,276
CCM wanafikiri wanaibomoa Chadema kumbe ndiyo wanajimaliza, usanii huu hata mtoto wa chekechea ataustukia, yaani ni upuuzi kupita maelezo.
 
mwaJ

JF-Expert Member
Sep 27, 2007
4,074
2,939
Magamba wameishiwa mbinu kilichobaki ni kutunga alfu lela ulela ili kuichafua Chadema. Nawahurumia wana Igunga wakishindwa kutofautisha mbichi na mbivu wataendelea kuwa watumwa wa magamba milele! Huyo gamba hakuchomewa nyumba wala nini! Yeye mwenyewe, katia kiberiti banda lake la kuku akaenda kulala.
 
The Invincible

JF-Expert Member
May 6, 2006
6,000
3,251
Usanii mwingine wa CCM bwana! But it may have potentially disastrous consequences to Chadema especially for simple minded personalities
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
CCM wameishiwa mbinu za kampeni sasa wanapandikiza mbegu ya chuki kwa wananchi.
Kama kweli chadema wanahusika kufanya tukio hilo kwanini waache karatasi hapo!
Na kama suala ni kuchoma nyumba kwanini chadema wachome jiko badala ya nyumba anayolala huyo kiongozi!
Hizi siasa uchwara, ambazo hazina budi kupigwa vita na wapenda maendeleo wa Igunga kupitia sanduku la kura!
Mpaka sasa naona ccm hawajagundua kuwa mbinu wanazozitumia zinazidi kuwaharibia!
HAKI HAIJAWAHI KUSHINDWA HATA SIKU MOJA!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom